Wachungaji wamkalia Kooni Obama
Wachungaji
wa Makanisa mbalimbali duniani wamepaza sauti na kumpinga Rais Barak
Obama katika mpango unaoelezwa kama kuiangamiza dunia kimaadili na
kuitenga na Mungu.Imeelezwa kwamba Rais Obama mara baada ya kutoa tamko
la kuhalalisha ndoa za mashoga, alikutana na wachungaji kutoka mabara
mbalimbali wakiwemo kutoka Afrika na kuwabembeleza kwa masaa mawili
akitumia vifungu vya Biblia lakini walimgomea.
Miongoni
mwa makanisa yaliyomgomea ni pamoja na ASSEMBLIES OF GOD(AG)
lililoitisha mkutano na waandishi wa habari jumanne iliyopita na kutangaza msimamo mkali wa kuwa HALIKUBALIANI na Obama kwa kuwa mpango wake unakinzana na maandiko matakatifu ya Biblia.
Jaji aagiza Amri Kumi za Mungu Zipunguzwe
Jaji
Michael Urbanski wa Marekani amesema kilichosalia ni muafaka
utakaopelekea Amri kumi za Mungu kupunguzwa kutoka kumi hadi sita na
lengo kuu ni kuondoa nne za kwanza ambazo ni kikwazo katika umoja wa
ushirikiano kidini bila kuumizana kihisia.Jaji Michael alifikia hatua
hiyo baada ya pande mbili zinazopingana kushindwa kufikia muafaka katika
shauri lililofunguliwa mahakamani na shule moja ya wasichana waliokuwa
wakipinga uamuzi wa bodi ya shule wa kufuta Amri kumi za Mungu zilizobandikwa katika shule ya Narrows High School.
Shauri
hilo ni matokeo ya hatua ya hivi karibuni ya Marekani ya kupitisha
sheria inayokataza Amri kumi za Mungu katika ofisi zote za umma,
mahakamani na hata mashuleni isipokuwa kwa kibali maalumu katika
mazingira maalumu.
Nyakati
Gazeti huru la Kikristo la Kila wiki
Nabii wa Lowasa Afanyiwa Vurugu
Mch
Blasius Mabumba wa kanisa la Faith Ministry lililoko Kinondoni
Hananasif jijini Dar es salaam hivi karibuni alinusurika kupigwa na
aliyekuwa mchungaji wa Kanisa hilo mjini Tanga Mch Jeremiah Mlaki katika
tukio lililopelekea kuvunjika kwa Ibada baada ya waumini kuamua
kuondoka.Mch Mabumba mwaka jana 2011 alitoa unabii kupitia gazeti la
Nyakati kwa kusema Mhe Edward Lowasa ndiye atakuwa rais wa Tanzania
baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowasa
|
Katika
Vurugu hizo zilizotokea mjini katika kanisa hilo mjini Tanga, Mch
Mambumba akiwa ameshikilia kipaza sauti aliwaeleza waumini wa kanisa
hilo kuwa alikuwa amefika kanisani hapo kwa lengo la kuwataarifu kuwa
kuna mabadiliko yanafanywa ambapo mchungaji wa kanisa hilo jijini Tanga
Mch Mlaki ataenda kusomea uchungaji na nafasi yake itachukuliwa na
Mchungaji ambaye Mch Mabumba likuwa maeongozana naye kutoka Dar es
Salaam ambaye alimtambulisha kuwa ni Mch Prosper.
Hapo
ndipo vurugu zilianza kwa Mch Mlaki kuanza kufoka kwa ukali kwa kusema
baadhi ya maneno ambayo siwezi yaandika hapa.Hata hivyo uongozi wa Faith
Ministry unamtuhumu Mch huyo kwa mahubiri ya kuzishambulia dini
nyingine kupitia mahubiri yake ambayo amekuwa akiyarusha katika kituo
cha Television cha Tanga TV.Kanisa hilo limepeleka barua rasmi kwa mkuu
wa wilaya ya Tanga likisema kuwa limemvua uchungaji wa kanisa hilo Mch
Mlaki.
Mch Adaiwa kupigwa kwa kumuita Mzee wa Upako Freemasons
Mhubiri mmoja kutoka nchini Kenya James Mbugua ambaye
amekuwa akihubiri sehemu mbalimbali na kufanya kile kinachodaiwa kuwa
ni kufichua siri za kundi la Freemasons, anadaiwa kujikuta katika
msukosuko mkali maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada kile
kinachoelezwa kumhusisha Mch Anthony Lusekelo ambaye wengi humuita Mzee
wa Upako na kundi la Freemasons.
Mkenya
huyo alijikuta akianza kupigwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa
Mch Lusekelo jambo lililomfanya akimbie bila viatu.Akiongea na gazeti
la Nyakati mtumishi huyo alikana kupigwa ila alikiri kuwa kuna kundi la
watu lililotaka kumletea vurugu mitaa ya Kariakoo.Gazeti la Nyakati
liliongea na Mch Lusekelo na kumuuliza juu ya hilo la waumini wake naye
alisema “huenda ni kweli kwa kuwa watu mbalimbali hufika kanisani kwake
kwa lengo la kuombewa na wengine hata hawajaokoka”.
No comments:
Post a Comment