Safari Bado Ndefu.........Muziki Wa Injili Umekuwa Wadunia?? a.k.a Gospesecular?
Kila
Jumapili ambayo Mungu atakuwa anatujalia uzima tutakuwa tunatazama
mambo ambayo yanatupa mawazo ya kila iitwapo leo na kuona kabisa Safari
Bado Ndefu. Kumekuwa na mambo mengi katika Wana Wa Mungu ambayo haya
tukiyatazama kwa kina ni kuona "Bado Safari Ndefu" Kuelekea tunakopaswa
kuelekea. Kumekuwa na Controversial za kutosha zinazotokana na mitazamo
ya Watu.
The Glorious Wakiwa Jukwaani Wakati Wa Gospel Music Awards.
Nia
ya Segment hii kwenye Blog ni Kuibua Mawazo ama mitazamo ya watu ambao
watawasilisha Mawazo yao Mbadala katika kuona mambo yanavyokwenda ndivyo
yanavyopaswa nia kubwa ni Kupunguza Umbali wa Safari kwa Kuleta mawazo
mapya ndani ya Jamii yetu Kupitia Blog hii.
Hakuna
shaka kwamba sasa Tanzania Muziki wa Injili unakua na kuongezeka kwa
kiwango cha kushangaza kama sio cha kazi kubwa. Kumekuwa na matamasha
kila iitwapo leo, kumekuwa na events za uimbaji zenye majina tofauti
tofauti, huku amplified Praise and Worship, Huku Aflewo, Huku Maximum
Praise and Worship, Huku Next Level, Huku Gospel Music Awards, Huku
Tamasha la Pasaka, huku Gospel Star Search na majina kadha wa kadha.
Samuel Rodin Akiwa kwenye Event Ya Next Level
Kwenye
Televisions na Radio vipindi vya Gospel Tracks na kadha wa kadha mpaka
kwenye radio za Secular wamekuwa na vipindi maalum vya muziki wa Injili.
Kila mtu amekuwa na jitihada binafsi za kutaka kukuza Muziki huu wa unaoitwa Muziki wa Wa Injili.
Kyala Dee Mwanamuziki Wa Kitanzania Anayefanya Muziki Ughaibuni
Katika
kasi hii wameibuka waimbaji wengi sana katika tasnia hii ya unaoitwa
Muziki Wa Injili. Wanamuziki hawa kutokana na utashi wao wamekuwa
wakiandaa albam zao either kwa kiwango cha chini ama kueshindwa
kuendelea ku hit kwenye gospel music kwa sababu moja ama nyingine
kutokana na matokeo wanayoyapata kutoka kwa wasambazaji wa Kazi za
Muziki wa Injili.
Christina Shusho Mshindi Wa Tuzo za "Grooves Awards" 2011-2012 Nchini Kenya.
Ukienda
kwenye Maharusi, Kitchen Parties, Misiba kila mahali Muziki wa Injili
umekuwa ukitumika kama ndicho kuburudisha muafaka wa tafrija hizo katika
nchi yetu ya Tanzania.
Kutokana
na Kukua kwa "Gospel Music Industry" na Sio Gospel Music Ministry
kumepelekea Muziki wa Injili Kuibua Maswali mengi kama Kweli Muziki huu
unapaswa kuendelea Kuitwa Muziki Wa Injili.
Emmanuel na Flora Mbasha Wanamuziki ambao Kwa Kipindi hiki wako Marekani hapo walipokuwa "Voice Of America".
Maneno yanayoimbwa kwenye nyimbo hizo yameendeleea kuleta maswali kama ni Muziki wa Injili, Uvaaji wa Wanamuziki Umeendelea Kuwa ni Utata katika Majukwaa na kuondoa hadhi ya Injili, Uchezaji katika Majukwaa umeibua mijadala mizito na kukosa mwelekeo kwa kutaka kufahamu bado kama kuna hadhi ya Kuwa na Muziki wa Injili Tanzania.
Kumekuwa na mijadala ya kila siku kuwa Muziki wa Injili Tanzania Umevamiwa na Watu wasio wa Injili. Kuna Maswali yameibuliwa ambayo yanatafuta majibu katika Jamii yetu.
Gee and Seth Wanaofanya Muziki Wa Hip Pop Walipokuwa ndani ya Event Ya Riot.
1. Muziki wa Injili ni Upi, how can we clearly define Gospel Music, kwa maana vigezo gani vinaufanya wimbo fulani kutokuwa wa injili na fulani ni wimbo wa injili.
2. Unaitwa Wimbo wa Injili Sababu unaimbwa wimbo na Mkristo ama mtu yeyote anaweza kuimba kwa kuimba maneno ya Mungu "Kikristo".
3. Kwa Watu Wasiomjua Mungu kwenye Maisha yao kama Waandaaji wa Matamasha, Waandaaji wa Tuzo za Muziki wa Injili, Wasambazaji wa Kazi za Muziki wa Injili, Waandaaji Wa Kazi za Muziki wa Injili, Mameneja wa Kazi za Injili na Watangazaji wa Radio na TV ni sahihi kwao "Ku-Promote" muziki wa Injili???
4. Je Ni sahihi Mwanamuzi wa Injili kutaja "dau" lake na kulipwa kabla ya huduma??
Addo November Rais Wa Shirikisho la Wanamuziki Wa Injili Tanzania.
5. Ni sahihi Kwa Wanamuziki wa Injili Kushirika katika Matamasha yaliyoandaliwa na Wadunia??Kushiriki tuzo zisizo za Kimungu mfn. Kills Music Awards e.tc.
6. Ni Sahihi kumuita Mwanamuziki wa Injili Star??"Nyota Wa Muziki Wa Injili.
Kwa Wiki Kadha zijazo nitakuwa ninajibu maswali haya kadha wa Kadha Kwenye Bloga huku nikipikea mawazo.
Kama una maoni kuhusiana na maswali hapo juu tuma kwenda
1. Email Address....samuelsasali@gmail.com
2. Mobile Number. 0713 494110
3. Facebook Account.. Samuel Sasali
No comments:
Post a Comment