01 May 2012

Tuesday, May 1, 2012

Albam Ya Mwamba Mwamba Yampa Tuzo Solly Mahlangu Kwenye South Africa Music Awards


Usiku wa leo tarehe 30 April, 2012 Katika Ukumbi wa Sun City, Mwanamuziki Solly Mahlangu ametwa tuzo katika South Africa Music Awards alimaarufu kama SAMA. Albam Ya Mwamba Mwamba aliyoimba wimbo wa Kiswahili Umempaisha Mwanamuziki huyo na Kuwashinda Wanamuziki Wakongwe katika "Category" ya "Best Traditional Faith Music Album" ambapo katika kundi hilo alikuwepo Kgotso, Ngubheko Mbatha na Soweto Spiritual Singer.


Mwanamuziki Bora wa Kiume kwa mwaka 2012 ni AKA na albam yake ya "Altar Ego". Wakati huo huo Mwanamuziki wa Kike aliyepata tuzo nyingi zaidi usiku wa leo ni Zahara na Albam yake yake ya "Loliwe". Mwanamuziki huyo wa kike amenyakua tuzo zaidi ya tatu usiku wa leo ingawa vazi lake la usiku wa leo halikuwa zuri kama ambavyo wengi walitarajia wanamuziki wa south africa wanavyojitutumua katika mavazi.


Tuzo hizo zenye mchanganyiko tofauti tofauti kama zile huku Tanzania Kills Awards ambapo kuna Category ya Gospel, ndiyo iliyompa Ushindi Solly Mahlangu. Mwaka Jana Mwanamuziki huyu wa Gospel alishinda tuzo hizo kwa  Wimbo wake wa Obligado

Hii ni Exclusive Interview Wakati akizindua Albam Yake Ya Mwamba Mwamba.
Huu ni Wimbo Unaopendwa sana South Africa wenye jina la "Wa Hamba Nathi" yaani "Tembea Nasi" wimbo huu uko kwenye albam ya Mwamba Mwamba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...