PASTOR BENJAMIN DUBE ASHEREHEKEA MIAKA 50 YA KUZALIWA KWAKE KWA KUBARIKI WATU
Mkongwe wa muziki wa injili nchini Afrika ya kusini pastor Benjamin Dube wiki hii alibariki wengi kama ilivyokawaida yake kupitia huduma yake ya uimbaji pale alipoamua kusherehekea miaka 50 ya kuzaliwa kwake kwa kufanya kipindi maalumu kwenye kituo cha SABC2 cha nchini kwake kupitia kipindi maarufu cha gospel, kiitwacho gospel time kilichorushwa siku ya jumapili usiku.
Mkongwe huyo ambaye alizaliwa tarehe 23 mwezi wa kwanza mwaka 1962 aliweza kuwakumbusha mashabiki wake alipoamua kuimba nyimbo za zamani pamoja na mpya kutoka katika DVD yake aliyoitoa mwezi wa pili akishirikiana na familia yake, huku mashabiki wakionyesha ni kwajinsi gani mtoto wake aitwaye Buhle alivyowabariki kwa kipaji chake cha uimbaji,pia alizungumzia safari yake ya muziki.
Mmoja wa watu waliokuwa wanatizama kipindi hicho ni Nqubeko Mbatha ambaye ni kati ya wanamuziki wanaovutiwa na upigaji piano pamoja na uimbaji wa Pastor Dube ambapo alishindwa kuvumilia na kuamua kuandika vichwa kama vitatu kumkubali pastor Dube kwakile alichokuwa akikifanya.Pastor Dube ambaye alianza safari yake ya muziki mwaka 1986 kwa kurekodi wimbo Holy Spirit ambao uliotokea kupendwa sana na watu wengi kuununua,miaka 13 baadaye alikwenda nchini Marekani ambako alirekodi album yake ya kwanza live ikifahamika kama ''I Feel Like Going on'' chini ya Epic record ambayo iliweza kufanya vyema na kuuzwa kiwango cha Platinum.
Pastor Dube akiwa na familia pamoja na wafanyakazi wa kituo cha SABC2 mara baada ya kipindi. |
Pastor Dube ambaye safari yake ya muziki mpaka sasa akiwa na miaka 50 ni ndefu na yenye mafanikio ni mmoja kati ya waimbaji ambao waliweza kuutambulisha vyema muziki wa gospel nchini kwake,tayari ametoa zaidi ya matoleo 15 pia akimiliki kampuni yake ya muziki iitwayo Dube connection chini ya Sony BMG na Spirit Music ambapo kutokana na kazi yake nzuri ya kukuza vipaji na kurekodi, imeingia ubia na makampuni makubwa ya muziki kama Sony,Spirit,BMG,Gallo,Samro na makampuni menginepia ameshirikiana na waimbaji mbalimbali maarufu wa gospel duniani akiwemo Kirk Franklin,Bishop TD Jakes,Israel Houghton,Bishop John Francis,Andrae Crouch na wengine wengi.kwa upande wa familia Mungu amembariki kwa zawadi ya watoto wanne akiwa na mkewe Thabile wakiwa wanaishi kusini mwa jiji la Johannesburg Afrika ya kusini.
WIMBO WA KWANZA KUREKODIWA NA PASTOR DUBE ''I FEEL LIKE GOING ON''
TAZAMA WIMBO NGIYAKUTHANDA
Pastor Dube akiwa na mkewe pamoja na Bishop TD Jakes. |
wakati wa recording ya DVD mpya ya Pastor Dube. |
Pastor Dube na watoto wake. |
Pastor Dube akipiga kinanda huku watoto wake na kundi zima wakiimba,hii ni ndani ya DVD mpya. |
Cover la CD mpya ya Pastor Dube. |
No comments:
Post a Comment