19 February 2014

Step Up.....Hilda Nchunga Mwanamuziki anayewaza Kufika Mbali

Ze Blogger: Wasomaji watatami kusikia majina yako Kamili

Hilda: Majina yangu kamili ni Hilda Nchunga

Ze Blogger: Ulizaliwa wapi na ni Mtoto wa ngapi Kuzakuwa kwenye familia yenu?

Hilder: Nilizaliwa katika Mkoa Wa kigoma na kwa sasa niko Mkoani Morogoro kwa ajili ya masomo. Mimi ni mtoto wa 3 kuzaliwa kati ya watoto wanne wa mzee Isaack Nchunga.

Ze Blogger: Kwenye kizazi chetu cha sasa Vijana wengi sana hawapendi kujishughulisha Kihuduma wanapenda tu kuingia na kuondoka wewe Kanisani unajishughulisha na nini?

Hilda:Nikiwa kanisani nafanya kuduma ya praise team ktk kanisa la TAG Bethel Rivavil Temple mjin morogoro, Mungu ameweka kwangu huduma ya Kusifu na Kuabudua na Kipaji cha Kuimba.

Ze Blogger: Maelezo yako ya awali ulieleza kuwa uko morogoro Kimasomo unasoma wapi?

Hilda: Mimi ni mwanafunzi katika chuo cha St.Augustine branch ya Morogoro.

Ze Blogger: Maisha ni mapambano na achievements and falls je umewahi fanya kitu ukajisikia hapa sasa nimefanikiwa?

Hilda: kitu nimewahi fanya kwenye maisha ni kukamilisha albam yangu ya 1 ya Hosana sababu kwa was expensive but with God help nilifanya, kitu naweza sema katika albam hii ya Hossana, ni albam yenye nyimbo 8 zilizojaa Neno la Mungu ndani yake.

Ze Blogger: Kati ya Changamoto kubwa za Wanamuziki wa Tanzania ni namna ya kusambaza kazi zao je wewe nani anakusambazia zako? na je ni audia ama ni DVD?

Hilda:Albam hiyo ipo katika mfumo wa audio na inapatikana kupitia mimi mwenyewe ninapoenda fanya huduma sehemu mbalimbali, kuhusu kufanya video ninajiandaa kwa kuifanya baada ya kumaliza masomo mwez wa 6.

Mungu akubariki Hilda.

Asante Ubarikiwe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...