21 May 2012

Ahadi Ni Deni...Mhe. Joshua Nassari atoa Sadaka Ya Shukrani


Mheshimwa Joshua Nassari akitoa shukurani yake jana kanisani.

Mbunge wa jimbo la Arumeru mashariki kupitia chama cha demokrasia na maendeleo(Chadema) mheshimiwa Joshua Nassari hapo jana ametoa shukurani ya pekee kwa Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kuwatumikia wananchi wa jimboni mwake,ibada hiyo imefanyika katika kanisa la Pentekoste Kilinga huko Arumeru.

Akizungumza ibadani wakati wa shukurani mh.Nassari amewataka wana wa Arumeru kuwa na maono ili kuleta maendeleo jimboni humo, huku akirudia msemo wake kwamba kwakuwa ubunge wake kapewa na Mungu kupitia wana wa Arumeru mashariki ndio maana akaamua kumtolea skukurani ya pekee pia akasema kuwa ubunge alionao alikuwa na maono hayo kwa muda mrefu na kuwataka wana Arumeru kuwa na maono kwakuwa kama hakuna maono ya watayafanyia nini mashamba hayo kwa maendeleo kama ujenzi wa shule na mambo mengine inaamaana mashamba wanayoyadai hawawezi kuyapata.

Aidha akawaomba watu wote aliotofautiana nao kipindi cha kampeni kuacha tofauti zote na kufanya kazi kwa pamoja ili kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo,huku akitania kwamba wale wote waliombeza kwamba hajaoa wakienda kwake hawawezi kupata chai,cha msingi ni kwenda ofisini kwake kwani bajeti ya chai ipo,akaongeza kuwa ana katibu wake msomi mwenye digrii mbili kulinganisha na yeye mwenye digrii moja,hivyo ofisi yake itakuwa wazi kwa mtu atakayefika kujadili mandeleo na sio kwenda kumuomba pesa.Zaidi alisema atakuwa mkali kwa yeyote atakayekwenda kinyume cha taratibu hata kama ni wa chadema.

Alimalizia kwa kuwashukuru wananchi wa jimbo lake waliofika kanisani hapo kumsindikiza katika shukurani yake na kuwataka ushirikianao zaidi hasa wakati huu ambao anaanza kazi rasmi ya kutembelea vijiji vyote vilivyomo jimboni mwake ili kuongea na wananchi wake,kwakuwa tayari ameshamshukuru Mungu na kuhitimisha kwa kauli ''Tulianza na Mungu tuko na Mungu na tutamaliza na Mungu''.

Katika tendo hilo la shukurani mheshimiwa Nassari alisindikizwa na muasisi wa chama cha Chadema mzee Edwin Mtei, Mbunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia chama hicho mheshimiwa Simon Peter Msigwa,wazazi wake, ndugu,wageni mbalimbali wakiwemo madiwani wa chama hicho Arusha mjini pamoja na wanachi wa jimbo la Arumeru Mashariki.
Mheshimiwa Nassari, Msigwa, Mzee Edwin Mtei pamoja na waumini wengine wakiwa ibadani.
Mheshimiwa Joshua Nassari akifurahia jambo ibadani.
Mheshimiwa Nassari akizungumza wakati wa ibada.
Mchungaji Samuel Nassari baba mzazi wa mheshimiwa Joshua akiwa ibadani.
Mama mzazi wa mheshimiwa Joshua Nassari akiwa ibada.        
generali mstaafu Sarakikya na wageni wengine wakifuatilia ibada.
Sadaka za waumini na wageni waliomsindikiza mheshimiwa Joshua Nassari.
Mheshimiwa Joshua Nassari akizungumza na wananchi pamoja na wageni kwenye chakula maalumu baada ya shukurani kanisani.
Madiwani wa Arusha mjini kupitia Chadema wakiwa katika pozi baada ya kuiona kamera.
Mheshimiwa Nassari akifungua pazia la kupata chakula.
Foleni ya kupata chakula iliendelea kama inavyoonekana.
Wazazi wa mheshimiwa Joshua Nassari wakipata chakula, kuzaa kuzuri jamani mwe!
Nyumbani alipozaliwa mheshimiwa Joshua Nassari.
Source Gospel Kitaa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...