Thursday, May 10, 2012
Joyous Celebration Kukanyaga Ardhi Ya Tanzania, Yatuma Mwakilishi Namna Ya Kujiunga na JC
Viongozi wa JC
ATOA SIRI ILI KUJIUNGA NA KUNDI HILO.Akijibu swali la ni sifa gani mtu awenazo ili kujiunga na kundi hilo,Pastor Jabu amesema ili kujiunga unatakiwa uwe wewe '' just be yourself'' sio kuiga kuwa kama fulani,wanatafuta mtu wa kujiunga na kundi hilo ambaye anaweza kuonyesha kitu ambacho waimbaji wa kundi hilo hawana,akaenda mbali zaidi na kutolea mfano wa pastor Agu Uche(double double) kwamba Joyous kwasasa imeamua kutafuta ladha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ndio maana wakampata Uche na sasa wanaye Mkhululi kutoka Zimbabwe kama una ndoto za kuimba kundi hilo kwa kugeza waimbaji waliopo katika kundi hilo basi sahau kujiunga nao.
Kiongozi wa Joyous Lindelani Mkhize.
Mfano mwingine amesema ni yeye mwenyewe uimbaji wake ni wakwake binafsi hajamuiga mtu,nao watangazaji wakamtolea mfano choirmaster bwana Lindelani kwamba uongozaji wake ni wakwake yeye mwenyewe,kisha wakamuuliza Jabu ni kwanini kiongozi mwenzake anapenda kuvaa kofia muda wote Jabu akacheka kisha akasema ile ni trade mark ya kwake kwa wataalamu wa biashara wanajua anamaanisha nini, ama kwa lugha nyepesi unaweza kusema kile ni kitambulisho chake.Aidha amesema kwasasa wanatafuta waimbaji kutoka nchi kama Mali,Siera Leone au Cameroon kwakuwa nchi hizo zina uimbaji wao wakipekee na Joyous wamenuia kuwa kundi la Afrika.Sasa kwa Watanzania ambao wana ndoto za kutaka kuimba katika kundi la Joyous fanya mazoezi ya namna yako tumia ujuzi wako na Mungu wako sio ugeze uimbaji wa waimbaji wa kundi hilo kwani ndoto yako haitatimia hasa wakati huu ambao nafasi imeanza kupatikana kwa kundi hilo kufikiria kuja kufanya tamasha la uimbaji mwakani.
Source: Gospel Kitaa
No comments:
Post a Comment