25 June 2012


Monday, 25 June 2012

WAIMBAJI NYOTA WA GOSPEL NCHINI WAKUTANA VIWANJA VYA JANGWANI JIJINI DAR ES SALAAM


Askofu mkuu wa E.A.G.T Dkt. Moses Kulola akihubiri hapo jana viwanja vya Jangwani.

Waimbaji nyota wa muziki wa gospel nchini na nchi jirani ya Kenya ni miongoni mwa waimbaji na kwaya mbalimbali zinazohudumu kwenye mkutano mkubwa wa injili uitwao ''JUNE CRUSADE''unaofanyika katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam ulioandaliwa na kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT).

Baadhi ya waimbaji hao wanaoshirikiana  bega kwa bega na muhubiri mkuu wa mkutano huo askofu mkuu wa kanisa hilo Dkt. Moses Kulola ni pamoja na Rose Muhando, Bahati Bukuku, Flora Mbasha, Martha Mwaipaja, J'sisters,Bonny Mwaitege na waimbaji wengine kutoka nchini Kenya wapo Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa pamoja na Faraja Ntaboba kutoka nchini Congo ambaye kwasasa yupo nchini Tanzania,pia kwaya mbalimbali kutoka makanisa ya E.A.G.T jijini huku askofu Kulola akiwa ameambatana na kwaya ya Bugando kutoka jijini Mwanza.

Mkutano huo ulioanza jana unatarajia kuihitimishwa Julai mosi unarushwa mojamoja na Wapo Radio Fm  ambayo unaweza kuisikiliza kupitia ndani ya blog hii. Licha ya mkutano huo pia askofu Kulola jumamosi alizindua rasmi kanisa la Jesus Village lililo chini ya jimbo la Kinondoni la kanisa hilo tukio ambalo lilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo.


Jacqueline Mshama pamoja na mdogo wake Jesca hapo jana waliwakilisha wenzao kwakusimama kama J'sisters kumsifu Mungu viwanjani hapo. 

Baadhi ya umati wa watu uliojitokeza viwanjani hapo.

Mchungaji Florian Katunzi  wa E.A.G.T City Centre, ambaye ndiye muongozaji wa mkutano huo akiangalia mambo yanavyoendelea.

Askofu wa jimbo la Kinondoni E.A.G.T akiwa katika hali ya maombi.


 UFUNGUZI WA KANISA LA JESUS VILLAGE ULIOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI ILIYOPITA.CHANGANYIKENI DAR ES SALAAM.
Askofu Dkt. Moses Kulola akizindua rasmi kanisa hilo huku mchungaji Mgonja akishuhudia na maelezo yakitolewa na mchungaji Katunzi.

Mchungaji PrayGod Mgonja akisoma Risala kwa askofu mkuu Moses Kulola.

Mke wa askofu Kulola akitoa ahadi yake ya laki tano kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa kanisa hilo.

Brigedia jenerali mstaafu Hemed akiombewa baraka na askofu Kulola.



Kutoka kushoto mchungaji Marego, askofu Willy Matingisa na askofu Bruno Mwakibolwa wakifurahia


MAELFU WAJITOKEZA TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU MKOANI KIGOMA


New Life Band wakimsifu Mungu viwanja vya mwanga community mkoani Kigoma hapo jana.

Bendi kongwe katika muziki wa gospel nchini New ya Life Band yenye makao makuu yake jijini Arusha,  hapo jana iliweza kubariki maelfu ya wakazi wa mkoa wa Kigoma waliohudhuria tamasha lao la kusifu na kuabudu lililofanyika katika viwanja vya Mwanga Community mkoani humo.

Band hiyo kama ilivyopania kuweka mabadiliko na kuamsha huduma ya uimbaji na kuwaeleza waimbaji kiwapasacho kutenda, imezishirikkisha kwaya mbalimbali  na wachungaji kutoka makanisa ya mkoani humo hali ambayo ilileta umoja na kuujenga mwili wa Kristo. Baadhi ya kwaya zilizohudhuria tamasha hilo ni pamoja na Kasulu Vijana kwaya FPCT a.k.a Mke mwema, Eden kwaya KKKT Kigoma, kwaya Katoliki ya mtakatifu Joseph pamoja na kwaya nyingine.

Baada ya kumalizika kwa tamasha hilo, bendi hiyo inatarajia kuanza kambi ya vijana itakayofanyika kuanzia kesho tarehe 26 hadi julai mosi, Bigabiro Mission Kigoma ambapo mwimbaji Upendo Nkone, Mariamu Nkwabi wataungana na bendi hiyo katika huduma ya uimbaji huku kambi hiyo ikiongozwa na neno ''Kijana na ulimwengu wa mabadiliko'', wakihitimisha kambi hiyo bendi hiyo itakwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya tamasha kubwa la kusifu na kuaabudu wakishirikiana na kwaya mbalimbali za mkoa huo.


Wana kwaya wa Kasulu vijana (Mke mwema) wakiimba kwenye tamasha hilo.

Baadhi ya wachungaji na watumishi mbalimbali waliofika katika tamasha hilo wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea.

Wanakwaya wa Mt. Joseph katoliki Kigoma wakimsifu Mungu wakati wa tamasha hilo.

wapiga ala wa kwaya ya Mt. Joseph kanisa katoliki wakiwajibika.

Eden Choir kutoka Lutheran Kigoma wakimsifu Mungu.





Monday, June 25, 2012

Papaa Kumuwakilisha Christina Shusho Nchini Uingereza



Zikiwa zimebaki Siku 5 tu yaani tarehe 30 June, 2012 Ili kufikia tamati ya upigaji kura kwa ajili ya Kumuwezesha Mwanamuziki Pekee wa Kike Tanzania Christina Shusho kushinda katika Category mbili alizochaguliwa kuingia. Mwanamuziki huyo amefunguka katika Radio Ya Watu Clouds FM, na Kueleza kuwa Yamkini akatuma Mwakilishi siku ya Kugawiwa tuzo hizo siku ya tarehe 7 Mwezi 7, 2012 nchini Uingereza.


Christina Shusho Mwanamuziki Pekee wa Tanzania aliyechaguliwa kuingia katika Category 2. Zikiwa kama ifuatavyo.


1.  Mwanamuziki Bora Kutoka Africa Mashariki
2. Mwanamuziki Bora Wa Kike Barani Africa.
              Shusho Kushoto, Papaa Ze Blogger Katikati na Kulia ni Mtangazaji Pastor Harris Kapiga


akihojiwa na Mtangangazaji mahiri Pastor Harris Kapiga katika Kipindi cha Gospel Track  hivi karibuni kupitia Radio ya Clouds FM yenye kusikika ulimwengu Mzima Mwanamuziki huyo amefunguka na kusema, kutokana na Majukumu yanayomkabiri kwa sasa huenda akamtuma Mwakilishi ambaye ni Papaa Ze Blogger kwenda Kumuwakilisha katika Tuzo hizo katika nchi ya Uingereza.

Watanzania tunayo sababu ya Kumpigia Kura Mwanamuzi huyu wa Injili ili kuweza Kutwaa tuzo hizo 2.

Ili kuweza Kumpigia Kura Shusho Sasa hivi Bonyeza ...http://www.ballotbin.com/voterReg.php?b=29492

21 June 2012


Thursday, 21 June 2012

KWA TAARIFA YAKO- JE UNAJUA MWIMBAJI NGULI WA HILLSONG AUSTRALIA ALIHAMA KANISA?

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina ukweli utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


Darlene Zschech.  
KWA TAARIFA YAKO kama hujui ni kwamba mwanamama ambaye amekuwa katika huduma kwa muda mrefu na kundi la gospel la Hillsong Australia aitwaye Darlene Zschech alijitoa ndani ya kanisa hilo yeye na mumewe Mark na kuhamia kanisa jipya huko huko nchini Australia liitwalo Church Unlimited ambalo lipo nje kidogo ya mji wa Sydney.

Mwimbaji huyo ambaye ametumika kwa miaka 25 ndani ya kanisa la Hillsong Australia lililochini ya mchungaji Brian Houston na mkewe Bobbie Houston, alijiunga rasmi na kanisa hilo jipya mnamo mwezi January 23 mwaka jana na kuanza kazi rasmi pamoja na mumewe kama mchungaji kiongozi wa kanisa hilo ambalo liko chini ya Australian Christian Churches(ACC) ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Assemblies of God. Akizungumzia kuhamia katika kanisa jipya mwimbaji huyo alisema ''Our aim was to find God’s choice, those who would lead us into the incredible destiny God has for our house,” the church stated. “God is faithful! 

Kwa upande wa mchungaji Brian Houston wa mega church Hillsong Australia alikaririwa akiwatakia utumishi mwema mwimbaji huyo na mumewe Mark ''I feel good about it ... and our church leaders and elders feel good about it because Mark and Darlene have really sown into our church for a long, long time,'' alisema Brian

Darlene akizungumza alipotembelea jijini London kanisa la HTB mwishoni mwaka jana.
Hata hivyo licha ya mwimbaji huyo na mumewe kuhama imeelezwa kwamba bado watakuwa wakishiriki katika matukio ya sifa na kuabudu zikiwemo recording za kundi la Hillsong kutokana na mchango wake alioutoa ndani ya kundi hilo ambalo kwasasa linawaimbaji lukuki akiwemo mtoto wa mchungaji huyo aitwaye Joel Houston anayesimamia tawi la kanisa hilo jijini New york nchini Marekani, waimbaji kama Brooke Fraser, Annie Garrett na wengineo, ambapo kundi la The Sowers la nchini lilipofanya ziara nchini Australia mwanzoni mwa mwaka jana waliweza kufika mpaka kanisa linaloongozwa na mwimbaji huyo. Wimbo ''Shout to the Lord'' uliotungwa na Darlene ndio ulioanza kulitangaza jina la Hillsong kwenye medani ya muziki wa injili duniani. 



Darlene akikumbatiana na mwimbaji wa The Sowers.

Darlene Zschech akizungumza jambo wakati wa tamasha la The Sowers group toka Tanzania.

The Sowers wakiwajibika kumsifu Mungu walipotembelea kanisa linaloongozwa na Darlene.

Baadhi ya umati wa watu waliohudhuria tamasha hilo lililofanywa na The Sowers group kanisani kwa Darlene.
           DARLENE AKIANZISHA MOJA YA NYIMBO NDANI YA HILLSONG AUSTRALIA.

HAPA HILLSONG ILIWASHIRIKISHA WAIMBAJI NYOTA KAMA RON KENOLY KATIKA RECORDING YAO, HAPA WAKIIMBA SHOUT TO THE LORD.


Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tuonane wiki ijayo

Thursday, June 21, 2012

Ndani Ya Loyola High School Weekend Hii

Time ni Saa 3 asubuhi Mpaka Saa 10 Jioni.

20 June 2012

Kanisa lina Mengi ya kujifunza baada ya DNA kutangaza kurudi kufanya secular Music


DNA
Kwa afrika Mashariki na kati jina DNA(Denis Kagia) sio geni masikioni mwa wafuatiliaji wa muziki, DNA ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya aliyetambulika na kupata sifa nyingi baada ya kutoa nyimbo yake ya BANJUKA,mwaka juzi DNA alitangaza kuwa ameokoka.Kwa waliokuwa wanamfatilia kwa kina utagundua DNA alisema wazi kuwa baada ya kuokoka anayafurahia maisha ya wokovu kwa kuwa yamemtenganisha na Pombe na sigara vitu ambavyo alishindwa kuachana navyo hadi alipookoka.Baada ya kuokoka DNA alianza kufanya muziki wa injili huku akifanya kazi ya utangazaji katika moja ya vituo vya redio vya kikrsto nchini Kenya.

Wiki iliyopita DNA akiongea na waandishi wa habari alitangaza rasmi kuwa ameamua kurudi na kufanya muziki wa DUNIA yaani aliokuwa akiufanya mwanzo kabla ya kuokoka na atabase kufanya all clubbing heats na tayari ameshafanya nyimbo mmoja iitwayo “Maswali ya Polisi”.Sehemu kubwa ya wakenya waimbaji na wafuatiliaji wa muziki wa injili nchini humo wameonekana kuuponda uamuzi huo na wengine kuubeza au kumbeza DNA mwenyewe.
Kwa Kanisa, suala la DNA linatoa uwanja mpana wa kujikagua na kujikumbusha kuwa wokovu ni NEEMA,leo DNA ameamua alichoamua na kanisa linasonga mbele sio kwa sababu mimi na wewe{Kanisa} ni wasafi sana kuliko yeye bali KWA NEEMA ya Bwana tunasonga mbele.

Kanisa linapozidi kukaa chini na kumhukumu DNA pasipo kumuombea huku ni kupoteza FOCUS ya safari yetu ya wokovu.Kwa kuwa kimsingi DNA sio wa kwanza kufanya hivyo na hatakuwa wa mwisho ila uamuzi wake unatupa wasaa wa kuangalia vitu gani ambavyo vinatusababisha wewe na mimi(kanisa) tuendelee na wokovu na kisha kuzidi kuvishikilia.
Kanisa halina budi kulichukulia suala la DNA kama darasa, na hapa ninamaanisha wapo wanamuziki wengi NGULI nchini na duniani ambao KRISTO atawaokoa,kuteleza kwa DNA kunatoa darasa huru katika kuwaelekeza hao Maceleb watakaookoka namna ya kudumu katika wokovu na nini wakiepuke ili wasirudi nyuma. Leo hii kuna namba kubwa ya maceleb waliookoka na mpaka leo wanaendelea na wokovu wakiwemo K-Basil,Renee Lamira,Chuck Norris (filamu),Cosmas Chidumule,Mzee Makasy,Mc Hummer,Stara Thomas na wengine wengi.

Mwisho ni vizuri Kanisa endapo litatumia muda mrefu katika kuwafundisha waongofu wapya namna ya kuliishia NENO na kudumu katika maombi, hii itasaidia katika kujenga internal strength ya mtu wakati anatoka na kujitangaza.Kwa uzoefu wangu nimegundua watu wengi maarufu ambao baada tu ya kuokoka na kukaa muda mfupi kwenye wokovu (i mean sio chini ya miaka miwili), wanapofanya kanisani kile walichokuwa wakikifanya huko duniani huwa hakina nguvu, na hii ni kwa kuwa vita yake ni kubwa kuliko nguvu ya Mungu aliyoiunda katika kulifanikisha hilo jambo      VICTOR-HOSSANAINC

Wednesday, June 20, 2012

Alichokisema Mch Piter Msigwa Bungeni jana



Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji  Peter Msigwa
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji  Peter Msigwa amejibu pendekezo la Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba la kutaka wapinzani waombewe, akisema hakuna kanuni yoyote ya uchumi inayosema Serikali ikiendesha mambo isivyo yanafanyika maombi.Badala yake, alisema yeye ambaye ni mchungaji huwa wanaombea wazinzi na watu waotembea na wake za watu, na si matatizo ya kiuchumi.

“Inashangaza sana kuona watu wanaunga mkono bajeti…, kila mwaka deni la taifa linaongezeka na sasa limefika Sh20 trilioni, fedha ambazo ukizigawanya kila Mtanzania atakuwa anadaiwa Sh400,000” alisema Msigwa.“Nilivyokuwa naona wabunge wamevaa suti na wanachangia hoja bungeni nilipenda jambo hilo na kutamani siku moja niwe mbunge, lakini baada ya kuingia bungeni nimegundua kuwa hakuna kitu.”

Alisema bunge hilo hivi sasa halieleweki na kwamba mbunge mwenye elimu ya kutosha akisimama kuchangia hoja huwezi kumtofautisha na mtoto wa darasa la pili.“Yaani mbunge profesa akisimama kuchangia hoja huwezi kumtofautisha na mtoto wa darasa la pili, watu wenye akili, akili zao wameziweka mfukoni na kuweka ushabiki wa vyama mbele, tumekuja bungeni kumaliza matatizo sio kuongeza matatizo” alisema Msigwa.

Huku akitumia mifano ya wanasaikolojia mbalimbali Msigwa alisema ni aibu kuona Watanzania wanazidi kuwa maskini harafu kila mwaka yanayozungumzwa ni tofauti na yanayotendeka.“Ufikie wakati wabunge tutambue kuwa tumekuja hapa bungeni kuwatumikia wananchi, Watanzania waliotuchagua wanateseka na wabunge hapa bungeni mnazungumza maneno ya khanga tu,” alisema Msigwa.

You might also like:

19 June 2012

Tuesday, June 19, 2012

Jifunze Kumiliki Majibu Ya Maombi Yako


Yoshua 13:7
Utangulizi,Katika dunia ya leo  watu wengi sana wamekuwa wakitumia muda wao mwingi ikiwa ni pamoja na kufanya maombi ya kufunga na kuomba ili kumuomba Mungu awabariki, awaponye, awalinde kwa kifupi awajibu mahitaji yao waliyonayo mbele zake siku zote. Wapo waliokuwa hawazai wamezaa, vipofu wameona, wasioajiliwa wameajiliwa, biashara za wengi zimefanikiwa, ndoa nyingi Mungu ameziponya, wapo waliotaka kuolewa au kuoa na Mungu amewapa waume na wake wazuri.


Sasa hao hao watu ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika kuomba Mungu awatendee miujiza katika maisha yao, imefika mahali wanaona yale ambayo yalikuwa ni majibu ya Moambi yao shetani ameyavamia na kuleta balaa zaidi na limekuwa pigo kubwa sana  kwa wana wa Mungu. Na kwa sababu hiyo wamejikuta wakimlalamikia Mungu kama vile wana wa Israeli na imefika mahali  pa wengine  kuona kama Mungu  hawezi na hivyo kumuacha.

Tatizo  la haya yote ni kwamba wakristo wengi hawana tabia ya au mazoea ya kumiliki mujibu ya maombi yao toka kwa Mungu. Huenda ulikuwa huna mtoto na Mungu amekupa kuzaa mtoto, sasa  huyo mtoto ndiyo jibu lenyewe kutoka kwa Mungu. Sasa ni lazima ujifunze kumiliki  huo muujiza wa mtoto, sasa si mtoto tu bali ni pamoja na ajira, ndoa, uponyaji, kanisa, Nchi, Biashara nk.

Kusudi la waraka huu mfupi ni kukufundisha njia zitakazokusaidia kumiliki majibu ya maombi yako na kukupa maarifa yatakayokusaidia kuwa makini na majibu ya Mungu katika maisha yako.Tafsiri ya Kumiliki, Neno kumiliki linapozungumziwa kibiblia lina maana ya kukiweka kitu au jambo fulani chini ya utawala wako, maana yake unakuwa na nguvu au umri juu ya hicho kitu. 

Una hakikisha  hakiwezi kutoka kwako. Kumiliki siku zote kunahusisha mapambano makali Sasa mimi sijui Mungu amekutendea nini? Ila ninachojua kwa namna moja au nyingine lazima kuna mambo ulikuwa unamuomba Mungu  akufanyie na mengine tayari ameshakufanyia na mengine ndiyo anayafanya na bado kuna mengi atafanya.sasa katika hayo aliyokwisha kufanya huenda amekupa mke au mme mtarajiwa, huenda ameiponya ndoa yako, nafsi yako, mwili wako, Afya yako, Huenda amekupa mtaji, amekupandisha cheo, amekupa mtoto, amepanua  mipaka ya huduma yako .

Katika lolote ambalo amekufanyia unatakiwa kulimiliki kwa maombi. Kama shetani alikuwa hataki uzae usidhani atamfurahia mtoto uliyemzaa. Kama alishindwa kumzuia asizaliwe usidhani atakubali aendelee kuishi. Shetani atafanya kila  analoweza kuua huyo mtoto au kuharibu chochote kile ambacho Mungu amekutendea kama jibu. Sasa kwa sababu hiyo ni lazima uzijue njia za Kibiblia zitakazokusaidia kumiliki hayo majibu ya maombi yako kutoka kwa Mungu.

Huenda zipo njia nyingi zifuatazo ni sehemu na ni za msingi kati ya hizo nyingi.
Njia ya kwanza, kumiliki kwa kuupigania na kuujenga huo muujiza au jibu lako toka kwa Mungu.

Yoshua 13:1-7, 2 Samwel 2:1-7.Ule mstari wa kwanza wa kitabu cha Yoshua katika kitabu Yoshua 13 unasema “Basi Yoshua alipokuwa mzee na kuendelea sana miaka yake BWANA akamwambia wewe umekuwa mzee na kuendelea sana miaka yako, kisha inasalia nchi  nyingi sana bado kumilikiwa” Kumbuka katika ile sura ya kwanza  ya kitabu cha Yoshua Mungu anamwambia Yoshua uwe Hodari na moyo wa ushujaa maana ni wewe utakayewarithisha watu wa nchi hii. Na ukisoma vizuri kitabu chote cha Yoshua unaona kabisa Yoshua alitekeleza agizo la kuwarithisha wana wa Israel nchi ya ahadi.

Wakati Mungu anamwambia Yoshua bado inabaki nchi yaani maeneo mengi sana ambayo bado hayajamilikiwa tayari Yoshua alikuwa ameshapiga zaidi ya wafalme 32 na kuiteka miji yao, lakini bado Mungu anamwambia bado nchi nyingi inasalia. Kitu gani Mungu anataka tujifunze hapa? Sikiliza Yoshua alipewa kuwarithisha wana wa Israel nchi hii lakini sio kuwamilikisha. Suala la kumiliki lilikuwa kwa yule aliyekabidhiwa nchi  au mji lakini sio kwa Yoshua. Sasa ndiyo maana Mungu akamwambia Yoshua kwa sababu wewe  ni mzee igawanye  hiyo nchi kwa wana wa Israeli kwa kufuata kabila zao ili waweze kumiliki. Maana yake waingie kwenye mapambano ya kile ambacho Mungu amewapa kupitia Yoshua.


Niseme hivi chochote unachokipata kwa njia ya maombi kinamilikiwa kwa njia ya maombi, jifunze kukipigania na kukijenga yaani kuendelea kukiri uwepo wa hicho kitu siku zote. Mfano kama uliomba mke au mme na Mungu amekupa usipunguze kuomba maana shetani usidhani anafurahia ndoa au uhusiano wenu. Ukiendelea  kusoma zile  sura zinazofuata za kitabu cha Yoshua ndipo utakapoona makabila yalivyopambana ili kumiliki jibu lao toka kwa Mungu la nchi.

Njia ya Pili; Miliki majibu yako kwa kutafuta maarifa zaidi ya kutunza huo muujiza.
Hosea 4:6a inasema “Watu wangu wanaangamizwa  kwa kukosa maarifa”.Sikiliza  muujiza au jibu lolote lile ambalo Mungu amekujibu au amekutendea una maarifa yake ya kuutunza. Maarifa hayo yanaweza kuwa ndani ya Biblia na hata katika vitabu vingine nje ya Biblia. Mfano umemwomba Mungu akupe mtaji uanze biashara na Mungu amekupa, sasa huo mtaji una namna zake za kuuendesha ili uweze kuzaa kwa faida. 

Kuna namna fulani ambayo ukiwekeza utapata faida nzuri. Sasa maarifa hayo ya kuwekeza yapo mengine kwenye Biblia lakini mengine ni kupitia watu wenye uzoefu katika hilo eneo, vyombo vya habari, kuna semina za kiserikali kuhusu biashara nenda huko ufuatilie ili  ujue zaidi, maana apendaye mafundisho hupenda maarifa. Huenda ulikuwa hujaoa au kuolewa na sasa uko kwenye ndoa. Hudhuria semina za ndoa na kusoma vitabu husika ili upate maarifa yatakauokusaidia kuishi katika ndoa vizuri.

Umezaa watoto wengi wanakufa kwa malaria halafu watu wanasema ni shetani tu wakati mwingine si shetani  ila ni wewe ulimweka mwanao katika mazingira  ya  kuumwa  na mbu vizuri ndio maana akafa. Soma habari za matumizi ya ngao, chandarua yanayotolewa na serikali hujui kwamba serikali yoyote ile imewekwa na Mungu. Kwa kifupi muujiza wowote amabo Mungu amekutendea una maarifa yake ya kuutunza na chanzo kikubwa cha maarifa ni neno la Mungu. Hivyo lisome likae kwa wingi ndani yako.

Njia ya Tatu; Miliki majibu yako kupitia shukrani, sadaka au utoaji wa aina  yoyote ile.
2Wafalme 5:17”Naamani akasema kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili, kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa BWANA.

Hizi  ni  habari za Namani Jemedari  wa jeshi la shamu alikuwa na Ukoma. Alipokwenda Istraeli  kwa nabii Elisha ili aombewe kuhusu tatizo la ugonjwa wake Elisha alimpa maagizo ya kutekeleza kuwa akajichovye / akajizamishe ndani ya mto Yordani mara saba na ndipo atapona. Baada ya Namani kutii maagizo Biblia inasema alipona na ngozi yake ikatakasika ikawa kama ya mtoto mchanga.Baada ya jibu  hilo kwanza Namani alimshukuru Mungu wa Elisha na kisha akasema tangu siku ile hatatoa tena sadaka kwa miungu yao kule shamu isipokuwa kwa Mungu wa Elisha pekee.

Unapomshukuru Mungu kwa lile alilokutendea ni ishara ya kupokea kwa kuonyesha kujua nani aliyekutendea hilo jambo na  hivyo kumrudishia yeye utukufu. Pia unaweza kumiliki majibu ya maombi yako kwa njia ya kutoa sadaka kwa yatima, wajane na pia unaweza kumshukuru Mungu kwa kushuhudia kwa wengine nini Mungu kakutendea au kutoa sadaka ya shukrani au utoaji kwa makundi mengine yasiyojiweza  katika jamii.

Na Mwl Patric Sanga

17 June 2012

Sunday, June 17, 2012

Baada Ya Facebook na Tweeter, Viva Shusho Viva Tanzania Campaign Yahamia Redioni

Baada ya effort kubwa wiki inayoisha kuelekezwa katika Social Media, weekend hii nguvu iliekezwa katika Radio mbali mbali hapa nchini kwa ajili ya Campaign ya kufanikisha Mwanamuziki Pekee Wa Injili Tanzania aliyeingia katika Tuzo za Mwanamuziki Bora wa Injili kuweza Kutwaa tuzo hizo.

Mwanamuziki huyo Christina Shusho ambaye mpaka sasa amefanya Interview na Radio Ushindi FM yenye makazi yake Mkoani Mbeya, ameshafanya Interview na WAPO Radio, na leo Campaign zimeendelea ndani ya Clouds FM na Praise Power FM.

Nia na Madhumuni ya Campaign ni kuhakikisha Mwanamuziki Christina Shusho kutwaa tuzo ya "Mwanamuziki Bora wa Kike Barani Africa" na "Mwanamuziki Bora Kutoka Africa Mashariki"

Ili Kumpigia Shusho Kura, bonyeza www.africagospelmusicawards.com , then bonyeza "Nominees 2012" Kisha Fuata Maelekezo.
 blogger Victor wa www.hossanainc.blogspot.com akiwa amepoz leo kwenye Ofisi za Clouds kabla ya Kuingia kwenye Interview ya Shusho.
 Papaa Ze Blogger akiwa anasoma soma nondoz kabla ya kuingia kwenye interview ya Clouds FM
 Shusho Kushoto, Victor Kulia wakiwa ndani ya Clouds FM asubuhi ya leo
 Kulia ni shusho, Kati ni Victor na kushoto ni Papaa Ze Blogger ndani ya Clouds FM.
 Pastor Harris Kapiga akiwa Kikazi zaidi asubuhi ya leo ndani ya GT ya Clouds FM.
 Nimetoka Mbali sana na hawa Kigoma People aiseee
 Bloggers ndani ya Clouds FM asubuhi ya leo tukiwa kikazi zaidi
 Hapa Timu iliamia Praise Power FM Mchana wa leo, Kushoto ni Uncle Jimmy Temu na Kulia ni Blogger Victor 
 Ndani ya Praise Power tuikuwa na Double E Sisters hapa liliachiliwa Sebene la Ukweli.
 Uncle Jimmy ya Victor wakichambya mambo ya Viva Shusho Viva Tanzania
 Double E Sisters ndani ya Praise Power Fm
Wametokezeleaje??

15 June 2012


Friday, 15 June 2012

MUNGU NI MWEMA KWANGU--ANENA MDOGO WAKE ANGELO BUENAVISTA WA TAMTHILIA YA THE PROMISE

Jodi Santamaria a.k.a Lia Buenavista.

''Ninafuraha sana kwa baraka ambazo Mungu amekuwa akinijalia maishani mwangu, Mungu amekuwa mwema kwangu,hakika ni mwema wakati wote'', hayo ni maneno ya mwigizaji wa nchini Ufilipino mwanadada Jodi Santamaria ambaye hapa nchini anafahamika zaidi kwa jina la Lia baada ya kuigiza kwenye tamthilia iliyojipatia umaarufu nchini ya The Promise akiigiza kama mtoto wa madam Claudia na Eduardo Buenavista ama mdogo wake na Angelo.
Mwigizaji huyu amezungumza hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Buzz cha nchini kwao Ufilipino kuhusiana na kuigiza tamthilia mpya hivi karibuni ''I’m really happy with all the blessings na dumarating. God has been really good to me. He's good all the time'', amesema Jodi ambaye aliachana na mumewe bwana Pampi Lacson miaka miwili iliyopita kutokana na matatizo yao ambayo hawakutaka kuyazungumza hadharani ambapo kwasasa mwanaume huyo anadaiwa kuanzisha uhusiano na msichana anayejihusisha na mambo ya urembo aitwaye Iwa Moto, ingawa kwa upande wake Jodi hataki kuzungumza lolote zaidi ya kubaki na Mungu wake pamoja na kumlea mtoto wake.
Jodi akiwa na mumewe Pampi Lacson pamoja na mtoto wao Thirdy.
                         
Mwigizaji huyo ambaye anatarajia kutimiza miaka 29 ya kuzaliwa hapo kesho, amesema angependa kufanya sherehe ndogo ambayo amesema itakuwa kama kuwashirikisha watu wengine baraka ambazo Mungu amekuwa akimjalia. Waigizaji nchini Ufilipino wengi wao wameonekana kumtanguliza Mungu mbele katika shughuli zao kwakumaanisha na wengine ikielezwa na mashabiki wa nchi hiyo kuwa wanazungumza kwa maneno tu na sio vitendo.

Kati ya wasanii ambao wamekuwa kioo kwa wengine kwasasa na wamekuwa wakipata sapoti ya maombi kutoka kwa mashabiki wenye kumuamini Mungu ni mwanadada Kristine Hermosa(Yna, Ara, Ella) pamoja na mumewe Oyo boy Sotto( Erick) aliyeigiza naye kwenye princess fish port zote zilionyeshwa na TBC wakati huo ikijulikana kama TVT,waigizaji hawa ambao Mungu amewajalia mtoto wa kike mwaka jana wakati wa Krismas pia wana mtoto mwingine wanayemlea baada ya kumchukua kutoka kwenye kituo cha watoto yatima, wamekuwa wakipata sapoti kubwa ya maombi na watu kupenda jinsi walivyowanyenyekevu katika maisha yao.

HAPA JIKUMBUSHE TAMTHILIA YA THE PROMISE KIPANDE AMBACHO UTAMUONA  JODI AKIIGIZA KATIKA TAMTHILIA HII (LUGHA KIFILIPINO)

Kristine na mumewe Oyo walipotoa picha za familia yao rasmi kwa mara ya kwanza kwa gazeti la
WASHIRIKI WA AFRICA GOSPEL MUSIC AWARD

Baadhi ya waimbaji waliongizwa katika kuwania tuzo tuzo malimbali za Africa gospel music awards zinazotarajiwa kutolewa tarehe 7 mwezi july mwaka huu huko jijini London nchini Uingereza.


Christina Shusho - Tanzania


Diana Hamilton - uk


Dena mwana DRC Kongo


Kefee - Nigeria


Gifty-Osei - Ghana



Lam Lungwar - South Sudan

lara george - Nigeria


Ntokozo Mbambo South



Onos Ariyo - Nigeria


Rebecca Arthur - Uk
 
Dawit Getachew - Ethiopia 
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...