Step Up.....Paul Clement Mwakanyamale a.k.a Pastor Paul
Kama
ilivyo ada ya Blog ilimtafuta mwanamuziki wa Gospel anayekuja kwa kasi
katika anga la muziki wa Injili Tanzania ambaye wiki hii anazindua albam
yake ya kwanza kabisa ya Umeniita.
Ze Blogger kama kawa akanyanyua simu kumsaka Pastor Paul....ngriiiiiiiiiiiiiii, ngriiiiiiiiii
Ze Blogger: Hallo, Hallo Paul Bwana asifiwe.
Pastor Paul: Amen, Papaa za Wewe
Ze Blogger: Kwema, Kaka moja kwa moja Uko hewani na Blog, unaweza tujuza Majina yako Kamili??
Pastor Paul: Majina yangu Kamili ni Paul Clement Mwakanyamale… mtoto wa watatu kuzaliwa kati ya wanne katika familia ya Mzee Mwakanyamale.
Ze Blogger:Kwanini kuimba zaidi ya kupiga?
Pastor Paul:Kwanza napenda kuimba Mwanzoni
niliona kama kuimba ni njia ya kujifariji kutokana na matizo mengi
niliyokuwa nayo katika kukua kwangu… lakini baadaye nikagundua kuwa
kuimba ndo huduma hasa Mungu aliyonipa kufanya ili kuwagusa wengi
zaidi
Ze Blogger: Safari ya Maisha ya Muziki kwako ilianzia wapi?
Pastor Paul: Nilifundishwa
kuimba na Ben Paul ambaye ni muimbaji wa bongo fleva… nilipenda sana
anvyoimba, nilikuwa form two by then… nilikuwa naimba mwenyewe nyumbani
kwaajili ya kujifariji.. sikuwa na wazo kwamba kunasiku nitaimba
kanisani na kwenye concert kubwa… hiyo ilikuwa ni kwaajili yangu
mwenyewe. lakini nikaaanza kuimba kwenye matukio ya shule kama
graduation na vikundi vya dini kama casfeta na ukwata. Lakini hakuna mtu
aliyekuwa anatambua hasa ni nini nilichonacho, nikaendelea tu.Mzee
wangu (baba) alikuwa hapendi… ananizuia kufanya mazoezi… nikibeba kinanda toka kanisani kuja nacho nyumbani anazuia.
Nilipofoka
form three mwishoni ndio nikaanza kuimba kanisani.. Calvary kwa
mchungaji Marko (babaake John Marco) kule keko…nikawa najichanganya na
kwenye makanisa mengine kama winners n.k.Nilipomaliza Form four 2010.. ndipo Emmanuel Mabisa aliponitafuta kuniomba nijiunge na kundi la Glorious Celebration. 2o11
kundi la messengers waliniomba kuongeza nguvu kwenye kundi lao kwenye
ziara yao nchini Korea.. Lakini baba yangu alizuia nisiende…
2011
tulifanya álbum ya kwanza na Glorious Celebration "Niguse" ambayo
ililitambulisha Glorious na kunitambulisha mimi pia ambapo niliimba
wimbo wa Juu Ya Mataifa Yote… Mpaka sasa ni mimi ni muimbaji wa Glorious
Worship Team.
Ze Blogger:Kwanini umeamua kufanya Album yako nje ya GWT?
Pastor Paul: Kwanza
ninaaamini kuna kitu Mungu anacho kwa mimi kama Paul(kuna maono ya
kundi lakini kuna maono binafsi pia… lakini na pia huu ndio ulikuwa
wakati sahihi wa album hii kutoka… maana nimekuwa nikistruggle kutoa hii
album kwa miaka minne lakini haikuwezekana… nimeshairekodi hii album
kama mara nne lakini kila mara ilikuwa ikiharibika au files zinapotea au
kuliwa na virus….
Ze Blogger:Albam ya Umeniita Ina jumla Ya nyimbo ngapi?
Pastor Paul: Album
hii ni ya kwanza ina nyimbo 8. Kwanini umeniita?!!!! hahahaa!!! Jina
lenyewe limejielezea… Wimbo huu nimeutunga sio siku nyingi sana
zilizopiata… na niliutunga baada ya kutambua kuwa Mungu mwenyewe
ameniita nimtumikie… Katika yote niliyopitia nilijua kuwa nilipita kwa
makusudi nijifunze ili nimtumikie..
Ze Blogger: Kuna Changamoto ya wanamuziki kujisimamia wewe umejipangaje katika hili.
Pastor Paul: kwanza
ni kweli changamoto ipo… na mie nimeitambua na nikaona sitaweza
kujisimamia mwenyewe…. nikaamua kutafuta kampuni ya kusimamia kazi
yangu. Kazi inasimamiwa na Mancon E.A Ltd. Chini ya Director Prosper
Mwakitalima.
Ze Blogger:Mara nyingi sana nimeona wanamuziki wanavuma miaka michache sana na wanakuwa hawana Malengo ya baadaye wee umejipangaje?
Pastor Paul:kwanza lengo kubwa ni kufikia sio Tanzania peke yake bali ulimwengu mzima… Tanzania ni mwanzo tuu.Pili kuwa na chuo cha muziki, studio ya Audio na video
na pia malengo baadye ni kufanya filamu pia za Gospel… sitaishia kuimba peke yake!
Lakini mwisho kabisa ni kuwa mchungaji…. Nasikia wito saaana!!!
Ze Blogger: :Swali
la kizushi… kuna issue ya wadada maana najua kwa umri wako na anointing
uliyokuwa nayo nadhani una changamoto ya kukabiliana nao unasemaje!!!
Pastor Paul:Kwangu mie hizo ni simple sana… Kikubwa ni kujitambua wewe ni nanai na unafanya nini hivyo vitu haviwezi vikakusumbua. Licha ya hivyo Mungu anatubeba saaana nikimaanisha Mungu anatusaidia….. Ni neema!!!
Ze Blogger: Watu watarajie nini jpili??
Pastor Paul:Najua
wengine wanatarajia Album waisikilize waone wakosoe… lakini mie nina
kitu tofauti na hicho… Naamini Mungu atafanya jambo la tofauti saana
siku hiyo!!
Na yeyote ajaye.. aje amwabudu Mungu na kumsifu Mungu… na kama alikuwa na tatizo lolote Mungu atamtokea katika maisha yake…
Ze Blogger: wanamuzikia unawakubali/wanakuinspire bongo.
Pastor Paul: MpeloKapama na Joel wa Glorious Celebration na Nje ya TZ - Marvin Sapp na Ephraim Sekele
Ze Blogger: Watu wengi wanakufananisha na Detrick Hadon je wewe ni mfuatiliaji sana wa kazi zake ama imetokea tu???
Pastor Paul: kweli ananiispire sana… uimbaji wake na ile kwamba ni mchungaji kijana saana aniispire sana.
Ze Blogger: Wimbo wa "umenifanya ibada" ulioimba na Glorious umegusa mioyo ya wengi saaana… ilikuwaje kuwaje ukatunga wimbo Powerful hivyo??
Pastor Paul:Huo
wimbo Mungu aliongea nami direct kabisa… Nilikuwa kwenye maombi
nikiomba Mungu anifundishe kumwabudu… nikiwa naomba nikasikia sauti
ikiniambia "sitakufundisha namna ya kuniabudu… bali nitakufanya wewe
kuwa mwabuduji" na "sitakufundisha ibada nitakufanya wewe kuwa ibada"…
huo ndo mwanzo wake!!!
No comments:
Post a Comment