31 May 2012

RAIS WA UMOJA WA MAASKOFU AFRIKA MASHARIKI ACHARUKA HATUA KUTOCHUKULIWA SUALA LA ZANZIBAR

Askofu Mkuu wa kanisa Anglikana Tanzania Dkt. Valentino Mokiwa.picha by libeneke blog
                
Rais wa Umoja wa Maaskofu Afrika Mashariki na Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu Dk Valentino Mokiwa amesema waumini Wakristo hawaridhishwi na utendaji kazi wa Polisi ukiwemo ufuatiliaji wa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa visiwani Zanzibar.

Akizungumza katika kikao kilichokutanisha viongozi wa Dini na Serikali katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais jana, Dk Mokiwa alisema Polisi imeshindwa kufuatilia matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuchomwa kwa makanisa hayo.

Alisema tangu mwaka jana zaidi ya makanisa 25 yamechomwa moto na hakuna kesi iliyofikishwa mahakamani. “Matukio mengi ya kuchomwa moto kwa makanisa yamejitokeza Zanzibar tangu mwaka jana lakini hakuna kesi iliyofikishwa mahakamani au mtu aliyekamatwa,” alisema Dk Mokiwa.

Aidha, alisema hadi sasa wafuasi Wakristo wanafanya kazi zao kwa hofu na wasiwasi kwani baadhi ya watu bado wanashambulia nyumba za ibada ikiwa ni pamoja na kurusha mawe. “Hadi sasa wafuasi wetu wanafanya kazi zao kwa wasiwasi mkubwa hata katika nyumba za ibada kwani wafuasi wenye siasa kali wanarusha mawe katika nyumba za ibada,” alisema.

Dk Mokiwa alisema hakubaliani na kauli za baadhi ya watu kwamba wanaofanya vitendo hivyo ni wahuni, bila hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao. Alifafanua, kuwa kama ni suala la Muungano kwa nini watu hao wachome moto makanisa na wasisubiri Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba ili wawasilishe hoja zao kuhusu Muungano. “Sisi hadi sasa hatuamini kwamba wanaofanya fujo ni wahuni, kama ni wahuni kwa nini wanachoma moto makanisa na kama ni Muungano kwa nini wasisubiri Tume ya Katiba? “Alihoji Askofu Mokiwa.

Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akijibu baadhi ya hoja za Baraza la Maaskofu Tanzania, alisema tayari Serikali imeweka ulinzi wa kutosha kwa makanisa yote visiwani hapa. “Tumeweka ulinzi katika sehemu zote za nyumba za ibada ikiwamo makanisani na Serikali itahakikisha hakuna fujo zitakazojitokeza kwa sasa,” alisema Aboud.

Aliahidi kuwasilisha kwa Rais Dk Ali Mohamed Shein malalamiko yao yote kuhusu vitendo vya kuwadhalilisha Wakristo visiwani huku Tanzania ikiwa nchi isiyo na dini isipokuwa wananchi. Mapema viongozi hao walitaka kuonana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ) kuzungumzia matukio hayo yenye kuashiria uvunjifu wa amani na utulivu.

Hata hivyo Aboud alikiri akisema wapo watu wanatumia vibaya taasisi za kidini kama mwamvuli wa kisiasa katika kuwasilisha hoja zao mbalimbali, yakiwamo masuala ya Muungano na marekebisho ya Katiba.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa akimweleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud (kulia) maazimio ya viongozi wa dini wa madhehebu ya kikristo juu ya hali ya vurugu, kuchomwa moto na kuvunjwa kwa makanisa visiwani humo. Viongozi hao walipeleka msimamo huo katika Ofisi ya Waziri Abood mjini Unguja, jana. Kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Ernest Kadiva. Picha na Edwin Mjwahuzi
                                 
source--gazeti Habari leo.

A TRUE DISCIPLE
Wise Man Harry delivered the message on Sunday morning. He introduced his sermon by saying there are two sides to life – the spiritual and physical. The title of his message was “A TRUE DISCIPLE”, and the proof text was taken from Mark 10:46-52. The blind man in the story called Jesus the “Son of David”, which is a Messianic title; it is given from above. Though physically unable to see, the blind man could see more than others; he had clearer vision though his enemies had good eyesight. On hearing Jesus’ pronouncement, he cast aside his garment and threw away anything which would hinder him. His garment was symbolic of his old self and all stagnating forces that held him down; he was in his moment of regeneration and renewal.
Wise Man Harry said if every sinner would cast aside his sinful nature like Blind Bartimaeus cast aside his garment, we would have fewer delays in conversion. According to him, Christ is looking for full-time followers, not part-time followers. If you say you are born again or you are a disciple of Christ and you are not, you will never be. It is the mind of God to answer prayers but Christ will not answer prayers until He sees in you a true disciple – a faithful follower, a willing servant and a man of great perception. You must show in your manner that Christ lives in you, he concluded.
Image
 Wise Man Harry 
Prophet T.B. Joshua later spoke on the essence of Christianity, saying that it is a relationship. He said every Christian should understand, “your contribution to others is an assignment from God”. He continued that we cannot afford to fail God and that our contribution to others in trouble will always solve a problem. To emphasize the importance of giving, some clips of Emmanuel TV Partners engaging in charitable projects were shown.
 Image
Prophet T.B. Joshua

EMMANUEL TV PARTNERS IN ZIMBABWE
The first video clip was of the efforts of the Emmanuel TV Partners in Zimbabwe, especially Mr John Chibwe. Inspired by the humanitarian activities he had witnessed on Emmanuel TV, Mr Chibwe purchased a bus for the less privileged community and has been devotedly assisting the visually impaired in their thousands as well as distributing wheelchairs and walking aids to the physically challenged. He was seen in the video distributing bags of rice and maize meal to the needy and helpless.
Mr Chibwe was personally in the service and shared his experience with the congregants. “It is a privilege to be able to give those in need,” he said. “You are a success when you can impact the lives of others”.email mabisatz@yahoo.com    phone no 255717025328.

Biblia hamsini zilichomwa moto Zanzibar – Askofu Kaganga

VIONGOZI wa makanisa wa Zanzibar wametoa malalamiko yao ya vitendo vya uchomaji na uharibifu wa makanisa kisiwani humo na kutaja vitendo 23 huku wakiitaka Serikali kuingilia kati, Katibu wa umoja wa Wachungaji wa Zanzibar Jeremiah Kobero alisema kuwa licha ya makanisa matatu yaliyochomwa na kubomolewa katika vurugu za sasa, kuna matukio 23 ya uchomaji moto makanisa yametokea tangu mwaka 2001.

Aliyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na uchomwaji moto wa makanisa ya The Church of God na Siloam yaliyofanyika mwaka 2011, makanisa mawili yaliyoko Masunguni yote mwaka huo huo, Kanisa la EAGT la Fuoni mwaka huo, kanisa la Pefa mwaka 2009, kanisa la Mwera mwaka 2012, kanisa la Redeemed lililiopo Dilikane mwaka 2001 yote ya mkoa wa Mjini Magharibi.

Alitaja pia makanisa yaliyochomwa katika mkoa wa Kaskazini kuwa kanisa la Tunguu, Unguja Ukuu, kanisa la CMF, Chukwani na Manyanya. Alitaja pia kuwepo kwa tabia hiyo kisiwani Pemba akisema kuwa imekuwa ni tabia kwa wakristo kusumbuliwa.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la TAG Kariakoo Zanzibar Dickson Kaganga aliwataka Viongozi wa serikali kuchukua tahadhari mapema kabla vurugu hazijatokea.

“Wakristo tumewafundisha kuvumilia…juzi walipovamia hapa walichoma moto biblia 50, ingekuwaje sisi tungechoma japo kitabu kimoja cha Kurani? Hayo makanisa yote yaliyochomwa, taarifa ziko polisi, lakini ukienda kutoa taarifa unaulizwa, una kibali? Yaani wanakutafutia tena kosa” alisema Askofu Kaganga.

Kaganga ambaye wakati wote alikuwa akibubujikwa na machozi aliwataka Wazanzibar kutambua umuhimu wa muungano kuwa ni pamoja na kuenezwa kwa dini. “Unapoona makanisa yanaenea hapa, ujue na kule bara misikiti inaenezwa na Wapemba ambao ni wajasiri wa biashara. Hiyo ndiyo faida ya muungano ndiyo faida ya kuoleana” alisema.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa askofu wa TAG kitaifa Askofu Magnus Mhiche alihoji kitendo cha wahuni kuvamia makanisa ilihali Serikali ikiwepo madarakani, “Mimi siamini kama ni Waislamu wamefanya haya, ila najiuliza, kama siyo wao basi ni wahuni. Hivi kweli wahuni wanatawala Zanzibar?” alihoji.

Naye Askofu wa kanisa kuu la Anglican Michael Hafidhi aliiomba Serikali kudhibiti mahubiri yanayotukana dini ya kikristo kwa njia ya kaseti akidai kuwa yanachochea vurugu.

“Zipo Kaseti zinazotukana ukristo, zinachochea vurugu, tunaomba serikali idhibiti. Hata ile kamati yetu ya ushirikiano wa dinio nayo imekufa inabidi ifufuliwe.

Kwa upande wake mwakilishi wa ofisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Jongo aliwataka Waislamu kuchukuliwana na Wakristo akisema kuwa hata Mtume (SAW) alifanya hivyo wakati akiitetea dini yake. “Hata Mtume wetu alipopata taabu alipokuwa Madina alikimbilia kwa Wakristo. Mpaka uislamu ulipoenea Makka yote. Hata alipotoka Medina na kwenda Mecca aliyempeleka hakuwa muislamu. Nashangaa leo ninaposikia eti Waislam wanachoma makanisa” alisema Jongo na kuongeza, “Hawa ni waislamu gani, mbona wamechoma hata bendera ya CCM, wamechoma bar na kunywa bia. Nini hasa malengo yao?

WAZIRI wa nchi katika Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohamed Aboud amepiga marufuku mihadhara na maandamano yanayofanywa na vikundi vinavyopinga muungano akisema kuwa watawachukulia hatua kali za kisheria.

Waziri Aboud aliyasema jana hayo baada ya kutembelea kanisa la Assemblies Of God lililopo eneo la Karikoo mjini Zanzibar lililochomwa moto na kubomolewa kutokana na vurugu zilizozuka kufuatia kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa kundi la Jumuiya za mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho). Katika ziara hiyo ambayo aliongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa, Waziri Aboud alisema baadhi ya viongozi wa dini wanatoa maneno ya uchochezi yanayosabaisha vurugu.

“Baadhi ya viongozi wa dini wanatoa maneno ya uchochezi, yanachochea vurugu zote hizi…. Maneno ni sumu, ndiyo tumeiingiza nchi katika machafuko yote haya” alisema Waziri Aboud na kuongeza, “Sisi kama Serikali tumewaita wenye makundi hayo na kuzungumza. Tumewaambia, kama mtu hataki dini aje kwenye majukwaa ya siasa. Tumekosea kuwaachia watu waanzishe vyama na vimesajiliwa kisheria kwa lengo la kueneza dini, lakini sasa wanaleta uchochezi.

“Kuanzia sasa ni marufuku kufanya maandamano na mikusanyiko yoyote ya aina hiyo” alisisitiza Waziri Aboud. Naye IGP Said Mwema alisema kuwa jeshi hilo limeongeza ulizni katika maeneo maalum yenye usalama mdogo hasa makanisa.

“Tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa tunadhibiti maeneo maalum ili yasiendelee kuvamiwa. Tunafanya uchunguzi, ili kuhakikisha nani, kwa nini na wako wapi” alisema IGP Mwema. Alisema jeshi hilo kwa sasa lina kikosi maalum kwaajili ya kuongeza nguvu ya kudhibiti machafuko kisiwani humo na kwamba hadi jana jeshi hilo lilikuwa limekamata watu 46 na kati yao 43 wamefikishwa mahakamani huku wengine watattu wakifanyiwa uchuguzi.

Aidha IGP Mwema alikiri kwamba jeshi hilo limecghelewa kuzuia uhalifu huo na kwamba hatua iliyopo sasa ni kudhibiti usiendelee.

“Kuna mifumo mitatu ya ulinzi, kwanza ni kuzuia kabla mambo hayajatokea, kwa hapo sisi tumeshachelewa. Tuko hatua ya kudhibiti yasiendelee na baada ya hapo tutajenga amani iwe endelevu” alisema. Wakati huo huo Chama Cha Mapinduzi CCM kimesikitishwa na vurugu zilizotokea ambazo wanaamini kuwa zimeandaliwa na Jumuiya za Uamsho na kuitaka serikali kuchukua tahadhari kubwa katika suala hilo kwani kama hatua hizio hazijachukuliwa huenda likaleta maafa makubwa.

“Cham cha Mapinduzi kinaalani vitendo hivyo na kuzitaka serikali zote kudhibiti hali ya amani na utulivu tulioizowea na kuwachukulia hatua kali wote waliosababisha vurugu hizi” alisema taarifa yake kwa vyombo vya habari. Kwa upande wake chama cha Chadema kimelaani vurugu hizo zilizofanywa kwa makusudi na vijana ambao wanaonekana wameshapata mafunzo maalumu kwa kusaidiwa na chama kimoja cha kisiasa kinachounda serikali ya umoja wa kitaifa.

“Chadema tunavitaka vyama vya siasa kuandaa makundi ya vijana ambayo mwisho wake wanakosa kuwapatia kazi na hatima yake kuwa vikundi vya kihalifu nchini” ilisema taaifa hiyo iliyotiwa saini na Hamad Yussuf Naibu Katibu Mkuu.
Chama Cha Wananchi CUF kimelaani vurugu hizo na kusema zimesababishwa na chuki binfasi, ukosefu wa hekima, matumizi ya nguvu za dola na uchochezi wa makusudi kwa wale wasiopendeleaq maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar.

“Vitendo vya watu wachache na kuharibu mali za watu ni uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa kizanzibari, uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua bila ya uonevu wala upendele” imesema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Salim Bimani

sosi: zanzibaryetu            

A One Night Seminar-Dar-es-Salaam Workers Christian Fellowship

29 May 2012


Tuesday, May 29, 2012

Kanisa Lingine Lachomwa Zainzibar


Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed  Shein
BAADA ya Kanisa la Assemblies of God kuchomwa moto katika vurugu zilizoanza mwishoni mwa wiki iliyopita, jana Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae nalo limechomwa moto.

Akizungumzia hali hiyo jana, kiongozi wa Kanisa hilo, Ambaros Mkenda, alidai kwamba Kanisa hilo lilichomwa moto na watu wasiojulikana na kusababisha uharibifu mkubwa.

Alidai Kanisa hilo lilichomwa moto jana saa 8.30 mchana na watu wanaohisiwa kuwa wafuasi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho, waliokuwa wakitoka katika Mahakama ya Mwanakwerekwe kusikiliza kesi ya wenzao waliokamatwa juzi.

Mkenda alidai kuwa watu hao waliwazidi nguvu walinzi wawili wa Kanisa hilo na kuvunja lango kuu la kuingilia ndani ya Kanisa na kuchoma moto na waliharibu madirisha na vifaa kadhaa vyenye thamani ya Sh milioni 20.

“Tunasikitika sana na uharibifu mkubwa uliofanywa katika Kanisa letu ambalo lilikuwa tegemeo kubwa kwa wafuasi wapatao 2,000 wa eneo la Parokia ya Mpendae na jirani,” alisema Mkenda.

Mkenda alidai kuanzia juzi, viongozi wa makanisa mbalimbali waliwasilisha maombi yao Polisi kuhusu kupewa ulinzi katika nyumba za ibada, baada ya kupokea vitisho. Hata hivyo, Mkenda alidai ombi lao hilo halikutekelezwa na Polisi na uharibifu mkubwa ukatokea katika Kanisa la Assemblies of God la Kariakoo.

Wafuasi na waumini wa Kanisa hilo walikusanyika nje ya jengo hilo, huku vijana wakishikwa na hasira wakitaka kwenda kulipiza kisasi katika maeneo ya jirani wakidai wanawatambua vijana waliofanya vitendo hivyo.

Mmoja wa waumini wa Kanisa hilo ambaye ni mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Susan Kunambi alilazimika kuwatuliza wafuasi vijana wa Kanisa hilo waliopandwa na jazba wakitaka kulipa kisasi.

“Hakuna sababu ya kupandisha jazba na kutaka kufanya vitendo ambavyo vitasababisha hasara na uharibifu ... Kanisa siku zote linahimiza amani na upendo na si chuki,” alisema Kunambi

Polisi walifika haraka katika eneo la tukio na kurusha mabomu ya machozi ili kutawanya makundi ya vijana waliojikusanya na wengine kurusha mawe.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alithibitisha kuchomwa moto Kanisa hilo na kusema ulinzi umeimarishwa katika baadhi ya maeneo ya nyumba za ibada yakiwamo makanisa. Baadhi ya mitaa ya Jang’ombe na Mwanakwerekwe njia zimewekwa mawe na vikundi vya vijana waliochoma mipira ya gari na kusababisha moshi mkubwa.

28 May 2012

Kanisa Lililolipuliwa Zanzibar laanza Kujengwa Tena

Baada ya Watu Wasio Julikana Kulipua kanisa la Kariakoo Visiwani Zanzibar usiku wa Kuamkia Jumapili ya Jana, Waumini wa Kanisa hilo siku ya Jana Wametumia kwa Ajili ya Kulikarabati Kanisa hilo kwa Kueleza Kuwa "Watapambana Lakini Hawatafanikiwa".

Siku ya Jana Blog iliwasiliana na baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo na baadhi ya waumini na Kusema pamoja na yote yaliyotokea bado Mtetezi Wao yuko hai. Mmoja wa walioteta na Blog amesema "Tunahitaji Maombi yenu zaidi tukitambua kuwa Vita si yetu ila Vita ni ya Bwana".

Nae Mmoja wa Viongozi Wa Kanisa hilo aliiambia Blog "Pamoja na Kulipua na yale yanayoendelea Watu wamesema wako tayari kujitolea kwa ajili ya Kanisa hilo kurudi katika hali ya Kawaida, na Ibada Zitaendelea kama kawaida wakati Ukarabati ukiendelea, Kwa Ujumla hali si Shwari huku Unguja sababu Leo hii Kanisa Lingine Limeripuliwa, hii ni Vita Ya Uislam dhidi ya Ukristo, Mungu bado yuko Upande wetu".

 Ujenzi Wa Kanisa Lililolipuliwa Ukiwa unaendelea chini ya Waumini Wa Kanisa Hilo
 Waumini wakiziba Mwanga wa Jua ili kuruhusu Ibada Ya Shukrani Kuendelea ndani ya Kanisa

 Gari ya Bishop Dickson Kaganga likiwa katika Muonekano wa sasa
 Ndani Ya Gari
 Waumini Wakiwa Nje kuendelea na shughuli za nguvu Kazi

 Eneo la Mlangoni Pa Kanisa
 Pamoja na Hayo Waumini walianza Kazi Ya Ujenzi Siku Ya Jana
Kazi ya Kuziba Madirisha Kwa Muda Ikiwa Inaendelea.

Lowasa aichangia Upendo Radio Shillingi Milion 10



Rais mstaafu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mbunge wa Moduli Mh Edward Lowasa, jana alikuwa mgeni rasmi katika tamasha maalumu la kuchangia usikivu mzuri wa Radio ya Upendo Fm 107.7 inayomilikiwa na Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT).Tamasha hilo lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubelee liliambatana na harambee ya kuchangia kituo hicho cha redio Mhe Lowasa yeye pamoja na marafiki zake walichangia jumla ya shilingi Millioni kumi.Lengo la kamati iliyoandaa tamasha hilo ilikuwa ni kukusanya jumla ya shillingi Million 220..

Katika Tamasha hilo liliwahusisha nyota wa muziki wa injili kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo Sara k kutoka Kenya,Jenifer Mngendi,Kijitonyama Upendo group na vikundi vingine vingi.

Mh Lowasa akiwa na mwanamuziki kutoka Kenya Sarak K katika tamasha la Upendo Radio siku ya jana

Mchungaji George Fute ambaye ni Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT,Askofu Alex Malasusa akitoa shukrani kwa Mgeni wa Heshima katika hafla hiyo ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh.Lowasa

Jenipher Mngendi akihudumu siku hiyo

Joshua Kiongozi wa kundi la Kijitonyama Upendo Group akimsifu Mungu ukumbini hapo

MZEE RWAKATARE NA MAMA RWAKATARE  KWENYE HARUSI YA MTOTO WAO WA MWISHO MUTA....
Pichani anaonekana Mchungaji Dr Getrude Rwakatare kulia akiwa na mumewe wakati wa harusi ya mtoto wao wa mwisho Bw Mutta Rwakatare alipokuwa akifunga ndoa siku ya juzi jumamosi tarehe 26.05.2012.Ndoa ilifungwa katika kanisa la Mikocheni na Harusi ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City.



Maharusi Mr and Mrs Mutta Rwakatare
                   Hapa ni JESCA, MABISA,  HAPPY.                                                                                                                                                                                                                                            ZOEZI LIMEANZA LA KUSAKA WAABUDISHAJI                                                                                         
Judges

Mchakato Wa Kumsaka "Mwabudishaji Bora" Walindima Leo Atriums Hotel

Lile Zoezi la Kuibua Wanamuziki Wapya Wa Injili wa Nyimbo za Kuabudu linafanyika leo katika Hotel Ya Atriums.

Blog ipo eneo la tukio kwa ajili ya Kukujuza kinachoendela

 Venue ikiandaliwa
 Watu wakijiandikisha siku ya leo
 Kama Kawa Kushoto ni meza ya Bloggers
 Watu wakiwa kwenye kuchukua namba zao
Kujiandikisha kukiendelea
 Blogger Rulea Sanga wa Rumaafrica Blog akiwa Kikazi Zaidi
 Papaa Ze Blogger akitoa maelekezo Kwa Washiriki Asubuhi ya Leo
Papaa Ze Blogger ndani ya Uratibu wa Worship Experiance

Stage kwaajili ya waimbaji


 Blogger Samsasali akitupia vitu katika blog yake ya www.samsasali.blogspot.com

 Mchungaji Charles Mbogoma (kushoto) akifuatilia uandikishaji
 Washiriki
Katibu wa TWE, Nasobile 

Upendo Joseph Huyu Ndiye Mshindi namba
Mbeba maono ya Tanzania Worship Experience, Billionaire kulia
Sulemani Ahungu namba 31
Moneila Rafael namba 30
Glory Kameta namba 28

Mchakato Wa Kumsaka "Mwabudishaji Bora" Walindima Leo Atriums Hotel

Lile Zoezi la Kuibua Wanamuziki Wapya Wa Injili wa Nyimbo za Kuabudu linafanyika leo katika Hotel Ya Atriums.

Blog ipo eneo la tukio kwa ajili ya Kukujuza kinachoendela

 Venue ikiandaliwa
 Watu wakijiandikisha siku ya leo
 Kama Kawa Kushoto ni meza ya Bloggers
 Watu wakiwa kwenye kuchukua namba zao
Kujiandikisha kukiendelea
 Blogger Rulea Sanga wa Rumaafrica Blog akiwa Kikazi Zaidi
 Papaa Ze Blogger akitoa maelekezo Kwa Washiriki Asubuhi ya Leo
Papaa Ze Blogger ndani ya Uratibu wa Worship Experiance

Stage kwaajili ya waimbaji


 Blogger Samsasali akitupia vitu katika blog yake ya www.samsasali.blogspot.com

 Mchungaji Charles Mbogoma (kushoto) akifuatilia uandikishaji
 Washiriki
Katibu wa TWE, Nasobile 

Upendo Joseph Huyu Ndiye Mshindi namba
Mbeba maono ya Tanzania Worship Experience, Billionaire kulia
Sulemani Ahungu namba 31
Moneila Rafael namba 30
Glory Kameta namba 28

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...