05 June 2012

WAKRISTO UINGEREZA WAFURAHI PAMOJA KWA MTOKO

Umati wa watu ukimsifu Mungu katika Big Church day out.
Mamia ya wakazi wa nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita waliweza kukusanyika pamoja kwa siku mbili katika kambi maarufu ifahamikayo kama Big Church day out ambayo hufanyika mara moja kila mwaka maeneo ya West Sussex katika viwanja vya Winston House.

Kambi hiyo ambayo iko tofauti na kambi nyingine za kikristo za nchini humo ambazo huwa na mafundisho ya neno la Mungu, michezo, vipindi vya kusifu na kuabudu, shopping, pamoja na maombi, kambi hii ni vitu viwili vikubwa hufanyika ni kusifu na kuabudu toka asubuhi hadi jioni pamoja na vipindi vya maombi katika mahema tofauti yanayopatikana viwanjani hapo.

Ambapo kwa mwaka huu imeshuhudia waimbaji maarufu wakihudumia kwa uimbaji, waimbaji hao ni pamoja na Israel Houghton, Tim Hughes, Matt Redman, Phil Wickham, Newsboys, LZ7, Casting Crowns, Muyiwa, Martin Smith, Gungor, UCB stage Artists, Lou Fellingham na waimbaji wengine bila kusahau Watoto Children Choir kutoka Uganda ambao waliweza kubariki wengi katika hema la Oasis ambalo liliandaliwa maalum kwa ajili ya watoto pamoja na wazazi wao.

Kambi hiyo imefanyika wakati ambao malikia wa Uingereza Elizabeth alikuwa akisherehekea miaka 60 tangu awe malikia wa nchi hiyo sherehe ambazo zimeanza wiki iliyopita, zinatarajiwa kuhitimishwa hii leo kwa malikia huyo kushiriki ibada ya shukrani katika kanisa la St.Paul lililopo jijini London.




Kijana LZ7 akimsifu Mungu na kundi lake katika main stage.



Watoto Children Choir kutoka Uganda wakiwa katika hema la Oasis wakimsifu Mungu.



Mtoto Lidya mwenye njano ambaye alimkumbatia Malkia Elizabeth akicheza.



MC wa hema akimtambulisha Lidya kwa umati wa watazamaji tabasamu iliyomfanya malkia naye kutabasamu.



Watoto Children Choir Uganda.





Mdau wa blog Beatrice Irungu akipozi na watoto.




Ikabidi nami niweke pozi pamoja nao kutokana na kazi yao njema.





Hawa wazee nao walikuwa wakiburudisha watu eneo la chakula



Main stage, Israel na kundi lake waliwasha moto wa injili kisawa sawa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...