21 June 2012


Thursday, 21 June 2012

KWA TAARIFA YAKO- JE UNAJUA MWIMBAJI NGULI WA HILLSONG AUSTRALIA ALIHAMA KANISA?

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina ukweli utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


Darlene Zschech.  
KWA TAARIFA YAKO kama hujui ni kwamba mwanamama ambaye amekuwa katika huduma kwa muda mrefu na kundi la gospel la Hillsong Australia aitwaye Darlene Zschech alijitoa ndani ya kanisa hilo yeye na mumewe Mark na kuhamia kanisa jipya huko huko nchini Australia liitwalo Church Unlimited ambalo lipo nje kidogo ya mji wa Sydney.

Mwimbaji huyo ambaye ametumika kwa miaka 25 ndani ya kanisa la Hillsong Australia lililochini ya mchungaji Brian Houston na mkewe Bobbie Houston, alijiunga rasmi na kanisa hilo jipya mnamo mwezi January 23 mwaka jana na kuanza kazi rasmi pamoja na mumewe kama mchungaji kiongozi wa kanisa hilo ambalo liko chini ya Australian Christian Churches(ACC) ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Assemblies of God. Akizungumzia kuhamia katika kanisa jipya mwimbaji huyo alisema ''Our aim was to find God’s choice, those who would lead us into the incredible destiny God has for our house,” the church stated. “God is faithful! 

Kwa upande wa mchungaji Brian Houston wa mega church Hillsong Australia alikaririwa akiwatakia utumishi mwema mwimbaji huyo na mumewe Mark ''I feel good about it ... and our church leaders and elders feel good about it because Mark and Darlene have really sown into our church for a long, long time,'' alisema Brian

Darlene akizungumza alipotembelea jijini London kanisa la HTB mwishoni mwaka jana.
Hata hivyo licha ya mwimbaji huyo na mumewe kuhama imeelezwa kwamba bado watakuwa wakishiriki katika matukio ya sifa na kuabudu zikiwemo recording za kundi la Hillsong kutokana na mchango wake alioutoa ndani ya kundi hilo ambalo kwasasa linawaimbaji lukuki akiwemo mtoto wa mchungaji huyo aitwaye Joel Houston anayesimamia tawi la kanisa hilo jijini New york nchini Marekani, waimbaji kama Brooke Fraser, Annie Garrett na wengineo, ambapo kundi la The Sowers la nchini lilipofanya ziara nchini Australia mwanzoni mwa mwaka jana waliweza kufika mpaka kanisa linaloongozwa na mwimbaji huyo. Wimbo ''Shout to the Lord'' uliotungwa na Darlene ndio ulioanza kulitangaza jina la Hillsong kwenye medani ya muziki wa injili duniani. 



Darlene akikumbatiana na mwimbaji wa The Sowers.

Darlene Zschech akizungumza jambo wakati wa tamasha la The Sowers group toka Tanzania.

The Sowers wakiwajibika kumsifu Mungu walipotembelea kanisa linaloongozwa na Darlene.

Baadhi ya umati wa watu waliohudhuria tamasha hilo lililofanywa na The Sowers group kanisani kwa Darlene.
           DARLENE AKIANZISHA MOJA YA NYIMBO NDANI YA HILLSONG AUSTRALIA.

HAPA HILLSONG ILIWASHIRIKISHA WAIMBAJI NYOTA KAMA RON KENOLY KATIKA RECORDING YAO, HAPA WAKIIMBA SHOUT TO THE LORD.


Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tuonane wiki ijayo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...