25 June 2012


Monday, 25 June 2012

WAIMBAJI NYOTA WA GOSPEL NCHINI WAKUTANA VIWANJA VYA JANGWANI JIJINI DAR ES SALAAM


Askofu mkuu wa E.A.G.T Dkt. Moses Kulola akihubiri hapo jana viwanja vya Jangwani.

Waimbaji nyota wa muziki wa gospel nchini na nchi jirani ya Kenya ni miongoni mwa waimbaji na kwaya mbalimbali zinazohudumu kwenye mkutano mkubwa wa injili uitwao ''JUNE CRUSADE''unaofanyika katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam ulioandaliwa na kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT).

Baadhi ya waimbaji hao wanaoshirikiana  bega kwa bega na muhubiri mkuu wa mkutano huo askofu mkuu wa kanisa hilo Dkt. Moses Kulola ni pamoja na Rose Muhando, Bahati Bukuku, Flora Mbasha, Martha Mwaipaja, J'sisters,Bonny Mwaitege na waimbaji wengine kutoka nchini Kenya wapo Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa pamoja na Faraja Ntaboba kutoka nchini Congo ambaye kwasasa yupo nchini Tanzania,pia kwaya mbalimbali kutoka makanisa ya E.A.G.T jijini huku askofu Kulola akiwa ameambatana na kwaya ya Bugando kutoka jijini Mwanza.

Mkutano huo ulioanza jana unatarajia kuihitimishwa Julai mosi unarushwa mojamoja na Wapo Radio Fm  ambayo unaweza kuisikiliza kupitia ndani ya blog hii. Licha ya mkutano huo pia askofu Kulola jumamosi alizindua rasmi kanisa la Jesus Village lililo chini ya jimbo la Kinondoni la kanisa hilo tukio ambalo lilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo.


Jacqueline Mshama pamoja na mdogo wake Jesca hapo jana waliwakilisha wenzao kwakusimama kama J'sisters kumsifu Mungu viwanjani hapo. 

Baadhi ya umati wa watu uliojitokeza viwanjani hapo.

Mchungaji Florian Katunzi  wa E.A.G.T City Centre, ambaye ndiye muongozaji wa mkutano huo akiangalia mambo yanavyoendelea.

Askofu wa jimbo la Kinondoni E.A.G.T akiwa katika hali ya maombi.



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...