Pastor Chriss aelezea alivyokutana mara ya kwanza uso kwa uso na TB Joshua
Pastor Chriss oyakhilome |
Pastor Chriss oyakhilome ni raia wa Nigeria na mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Christ Embasy.Hapa anaelezea namna alivyokutana na Prophet TB Joshua kwa mara ya kwanza.
“Nilikutana na TB Joshua kwa mara ya kwanza mwaka 2001 baada ya TB.Joshua Kunipigia simu, yeye pamoja na baadhi ya wageni wake walikuwa wakiangalia moja ya Program zangu za Television na katika programu hiyo kulikuwa na episode moja ambayo nilikuwa ninamuombea binti ambaye tangu amezaliwa alikuwa kipofu na alipokea uponyaji,TB Joshua alinambia aliguswa na muujiza huo hivyo akaamua kunipigia, na hiyo ilikuwa mara yetu ya kwanza mimi na yeye kuwasiliana”.
Baada ya hapo tuliendelea kuongea mara nyingi kwa njia ya simu,hadi kufikia kipindi hicho kupitia Television nilikuwa nimeshaangalia program zake(TB) mbili au tatu.Sikuwa najua mengi kuhusu yeye na aliponipigia tulikuwa tukibadilishana mawazo kwa kile tulichokuwa tukikifanya.Wiki kadhaa baada ya kuwa tukiongea kwenye simu, alinipigia simu na akaniomba niungane naye atakapokuwa akimfanyia maombi mgonjwa mmoja aliyeletwa kutoka nchini Holland.
Aliponiambia nilimwambia kuwa siku hiyo kanisani kwangu tutakuwa na ibada,TB Joshua aliniambia Ibada yao itakuwa ni ya usiku mzima na mimi nilikuwa namaliza ibada saa 3:00 usiku hivyo nilimkubalia.Nilimuuliza ni muda gani itanichukua hadi kufika hapo alipo akasema ni kama dakika 30, nikasema sawa kwa kuwa nikimaliza ibada hapa saa 3:00 usiku ntafika hapo ulipo saa 3:30 usiku hivyo nitajitahidi niwepo.
Pastor Chriss aliendelea kusema,nilienda kanisani kwa TB Joshua nikiwa na watu kadhaa na hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kukutana na TB Joshua uso kwa uso.Tuliingia kanisani nikalisalimia kanisa, na wengi wao walikuwa tayari wameshaniona kwenye Television na walifurahi kuniona.Kifupi baada ya kuwasalimia tulienda moja kwa moja kwenye section ya maombezi.
Alianza kwanza kuwafanyia huduma watu mbalimbali wakati mimi nikiwa nasubiri kwa kuwa nilienda pale kwa ajili ya kushirikiana naye kufanya maombezi kwa kwa raia kutoka nchi ya Holland kama alivyoniomba kwa njia ya simu.Kwa pamoja tulimuombea mtu yule aliyekuwa na magonjwa mbalimbali (multiple sclerosis) jina lake alikuwa akiitwa Jan
No comments:
Post a Comment