06 June 2012

NYOTA ALIYEJITOA MAKOMA KUJIFUNGUA MTOTO WA KWANZA, AOMBEWA ARUDI KWA MUNGU

Nathalie katika pozi.
                         
Aliyekuwa mwimbaji nyota wa kundi lililojipatia umaarufu barani Afrika na kwingineko duniani la Makoma, Nathalie Makoma anatarajia kujifungua mtoto wake wa kwanza mwaka huu katika ndoa yake na bwana JC Atamboto ambaye pia anajihusisha na mambo ya muziki.

Mwimbaji huyo ambaye aliachana na ndugu zake na kuamua kuimba muziki wa nje ya kanisa toka mwaka 2004 kutokana na kile alichodai kutaka kufanya kazi nyingine, huku ikidaiwa kuwa ni ugomvi baina yake na kaka yake mkubwa ambao amekuwa akiuzungumza sana kwenye vyombo vya habari hadi kufikia mashabiki kumtaka binti huyo ambaye alikuwa ni mwanzilishaji tegemewa wa takribani nyimbo zote za kundi hilo, kuacha kufanya hivyo kwani hata iweje yule ni kaka yake pia wanatakiwa kuzungumza masuala yao kifamilia na sio kuanika kwa kila mtu.

Mwimbaji huyo ambaye alishika nafasi ya pili katika shindano la kutafuta mwimbaji maarufu kama Netherlands Idol 4 2008 na kupewa jina la Tina Turner, amekuwa akiandika jumbe mbalimbali katika ukurasa wake wa facebook kutokana na ujauzito wake ambao kwa madai yake amesema unamfanya apoteze rangi yake nyeusi ya mng'ao aipendayo na kuwa mweupe hivyo atafurahi kurudia rangi yake ya awali pale atakapojifungua mtoto wake huyo ambaye tayari ameshampa jina la Giovanni Claudio II alipotangaza rasmi kwamba ni mjamzito kwenye ukurasa wake wa facebook mwezi march mwaka huu.
Nathalie katika picha aliyopiga mwezi wa nne mwaka huu, viatu hivyo na hali hiyo mwe!
                           
Mashabiki wa kundi la Makoma wamekuwa wakimuombea mwimbaji huyo ili arudi kumtumikia Mungu pia kurudisha mahusiano na ndugu zake ambao pia walikosa hata kuhudhuria sherehe za uvalishwaji pete ya uchumba ambayo iligubikwa na utata baada ya kuonekana kwa viny hadi harusi na kusababisha maswali mengi kama ilikuwa ndoa ya kweli aliyokuwa akiifanya mwimbaji huyo ambaye pia ameshirikishwa na Papa Wemba katika moja ya nyimbo za mwimbaji huyo mkongwe nchini Congo.
Photo: Yes i'm prégnant my first Baby Giovanni Claudio II
Nathalie katika picha yake ya kwanza kujitambulisha kwamba ni mjamzito katika Facebook.         

Album mpya ya Makoma.

Kwasasa kundi la Makoma limekuwa likijitangaza haswa katika ujio wao kupitia album yao iitwayo ''EVOLUTION'' ambayo ni ya kwanza tangu waungane tena mwaka jana na kutengeneza album hiyo ambayo imeanza kupatikana mwanzoni mwa mwaka huu, huku baadhi ya nyimbo zao zilizomo kwenye album hiyo kama'' Sosola,Yo Ozal na nyimbo nyingine zikiwa zikifanya vizuri kwenye vituo vya radio nchini kwao walikozaliwa Congo pamoja na nchini nyingine duniani bila kusahau Afrika ya mashariki.

ANGALIA VIDEO HII WAKATI AKIVISHWA PETE YA UCHUMBA, VIDEO AMBAYO ILIIBUA MASWALI KWA MASHABIKI WAKE NA WATU WALIOMFAHAMU AWALI KWA HUDUMA YAKE KANISANI.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...