23 March 2012

Sipho na Mercy Wapunguza Machungu Kambi Ya Joyous Celebration

Mercy pamoja na Sipho katika pozi wote ni waimbaji wa Joyous kwasasa ni wachumba.

Wakati Ntokozo na mumewe Nqubeko Mbatha wakiwa wamewaachia maumivu mashabiki wao ndani ya kundi la Joyous kwa upande mwingine wa shilingi hapo jana jioni mashabiki hao walianza kupoa mioyo yao angalau kwa kutabasamu baada ya waimbaji wa kundi hilo mwana kaka Sipho Manqele pamoja na Mercy Tintswalo Ndlovu kuvalishana pete ya uchumba ikiwa ni maalum kwa mwanadada huyo akisherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa.

Mkono wa Mercy ukiwa umevikwa pete ya uchumba(


Mercy akiwa jukwaani na Joyous akiimba kibao cha Xikwembu Xa Hina katika Joyous 15 part 1

Sipho Menqele ambaye yupo kwa kipindi kirefu sasa na kundi la Joyous akiwa mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kwenye toleo la 15 part 1 alitoka na kibao I'm grateful,amekuwa mwenye furaha baada ya kumvisha pete ya uchumba mwanadada Mercy na kuweka picha kwenye facebook yenye ujumbe she said yes! huku Mercy naye akiweka picha ileile kwa maelezo Birthday present ambapo wote wawili wamekuwa wakipokea pongezi kutoka kwa mashabiki wao na waimbaji wenzao wa Joyous.

Sipho akiimba


Sipho pamoja na Mercy.


Yawezekana kuvalishwa pete kipindi hiki kikamuongezea furaha zaidi mwimbaji huyo hasa ukizingatia pongezi zinazotolewa kwake kutokana na alivyoweza kuimba vyema wimbo Hi hanya mahala katika toleo jipya la Joyous,ambapo mashabiki wake wanasema anawakilisha vyema kabisa kabila tsonga kwakuimba kwa kiwango nyimbo kutoka kabila hilo,pongezi hizo zimekuwa zikimiminika katika ukurasa wa facebook wa kundi hilo na wengine wameamua kumpa a.k.a yake Pfotlo, waimbaji wengine wanaofuatia kupewa sifa ni Mahalia Buchanan pamoja na Mhululi tangu nyimbo zao ziwekwe kwenye mtandao wa youtube. No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...