Mwl Mwakasege ahudumu katika Ibada ya jumapili katika kanisa la TAG
Mama Diana Mwakasege akiwa na Mch Kimaro na Nyuma ni mtumishi wa Mungu Mwl Mwakasege |
Kanisa la Calvary Temple lililo chini ya TAG,Jumapiliyaleo tarehe 4/03/2012 limebarikiwa kwa kutembelewa na Mwalimu Christopher Mwakasege aliye hudumu ibada zote tatu na kutumiwa na Mungu sana katika kuleta mafunuo mapya ndani ya waamini. Mwalimu ametoa ujumbe wake wenye kichwa kinachosema Panua mahali pa hema yako ili upako uzidi katika maisha yako. Ujumbe huu katika biblia ulikusudiwa kwa mwanamke mjane tena aliyekuwa kijana lakini ndani yake akiwa na ndoto ya kuwa na familia kubwa.
Baada ya mume wake kufa alipunguza ukubwa wa hema uake akijua kwamba hakuna jinsi tena ya kuifanikisha ndoto yake.
Ukisoma vizuri katika ujumbe huu kutoka Isaya 54: 3-6 utaona kwamba Mungu alimwambia mjane huyu asiogope maana yeye ndiye Mume wake kama sote tunavyojua yeye ni mume wa wajane na hivyo akamwambia PANUA MAHALI PA HEMA YAKO NA WAYATANDAZE MAPAZIA YA MASKANI YAKO; USIWAKATAZE, Ongeza urefu wa kamba zako, vikaze vigingi vya hema yako, kwa maana utaenea upande wa kuume na kushoto, na wazao wako watamiliki mataifa.
Yapo mafunuo mengi zaidi yaliyo ambatana na ujumbe huu ambayo mwalimu alifunuliwa na kuongea nasi. ukitaka kubarikiwa zaidi fika kanisani ujipatie DVD yenye ujumbe huu.Kwa ufupi ni kwamba kuna mahali ulitakiwa kufika na bado hujafika na kuna kiwango cha hatua ya kimaisha haya ya mwili au kihuduma ulitakuwa kufika lakini bado hujafika, kwasababu hema yako umeikunja badala ya kupanua mahali pake ili iwepo nguvu ya kukufikisha mahali unapopaswa. You are not the real you! you do miss something. Consider fore to extend the place for your tent for God to increase you.
No comments:
Post a Comment