01 March 2012

MILCA NDANI YA CANADA AKIIWAKILISHA VYEMA TANZANIA

Milca L. Kakete mtanzania anayemtumikia Mungu nchini Canada



Milca L. Kakete

Leo hapa katika Hosanna Inc hususani kwenye safu ya “watanzania watumikiao Mungu nje ya Tanzania” tunaye Milca Kakete. Milca L. Kakete ni Mtumishi wa Mungu kutoka nchini Tanzania na kwa sasa anamtumikia Mungu nchini Canada.Baada ya kuurekodi na kuutoa wimbo wa NATAMANI,wimbo huu ulimtambulisha vizuri Milca katika vinywa vya watu wengi hapa nchini.

Natamani Kufanana Nawe
Natamani Kufanana Nawe
Sikuzote za Maisha yangu

Hapa Milca anaelezea historia yake na utumishi wake kwa ujumla.

Milca Kakete:Napenda kuchukua nafasi hii kushukuru kwa mwaliko huu wa kushiriki ambayo Mungu ameandaa.

Historia yangu kwa kifupi mimi ni mtoto niliyezaliwa katika familia ya wazazi waliompokea Yesu maishani mwao, nikiwa na umri mdogo sana niliimba Kanisani na hatimaye kuanza kurekodi na kwaya moja ya Nkinga Christian ya huko Tabora nilishiriki kuimbisha nyimbo kadhaa katika album yao mojawapo.

Mwaka 2003 Mungu aliongea nami kutoa kanda ya nyimbo za kuabudu inayoitwa "Yesu niko mbele zako" inayobeba nyimbo kama "Natamani,na Nifinyange"

Nampa Mungu sifa kwa matendo makuu aliyotenda kupitia kanda hiyo, maana nilipokea ushuhuda wa ndugu mmoja aliyekuwa ana maombi juu ya uponyaji wa ugonjwa aliokuwa nao,na akiwa ndani ya chumba chake aliambiwa na Mungu asikilize kanda hiyo baada ya muda alizimia na alipoamka aliambiwa amepona ugonjwa huo ulikuwa ukimwi na akaenda kupima amepona.

Milca L. Kakete akiwa na Mwanaye
kanda hiyo itakuwa madukani kwa mara nyingine tena miezi ya karibuni. pia kuna kanda nyingine ambayo sikuitoa madukani ila ni ya zamani kidogo.
na nyingine itakayokuwa iko sokoni hivi karibuni pia inayoitwa "Mwanangu Njoo". Jumla ni kama kanda 3 ambapo moja iliyokwisha toka na mbili bado hazijatoka na baadaye Mungu alinileta nchi ya Canada ambapo namtumikia Mungu.

Milca Kakete akiwa na Mume wake Kakete Sephan

Hosanna Inc:Kuna tofauti gani  kati ya kumtumikia MUNGU ukiwa nchini Tanzania na uwapo nchini Canada?

Milca:Tofauti nayoiona kati ya utumishi wa nyumbani Tanzania na huku kwa wenzentu ni mambo kadhaa

Moja, ni kwamba hapa hakuna uhuru wa kutoa mashauri kwa mtu binafsi kirahisi hata kama unaona mtu anahitaji msaada tofauti na nyumbani na hii nadhani ni kutokana na "maendeleo" ya teknolojia,teknolojia huja na mambo mengi ambayo hubadilika na kuwa ufungwa uliofichika ambapo adui anatumia maendeleo kuweza kuondoa nafasi ya Neno la Mungu kupenya kirahisi kwa watu.

Pili,ni swala la uthamani na umuhimu wa familia kwa kwa hapa adui kapata nafasi kubwa kufarakanisha familia, na waathirika ni watoto zaidi maana utengano wa familia unapotokea mtoto hana uchaguzi hata kama angependa wazazi wote wawe pamoja ili aendelee kufurahia upendo wa familia na baada ya hapo anaanza kukua akiwa na athari kisaikolojia mpaka huenda kufikia maamuzi mabaya ya maisha yake na hatimaye kuharibu maisha kabisa na hapo ndipo adui anapopataka maana mwisho wake ni kubadili kizazi kutoweza kuwa na maadili mema.

Hosanna Inc: Unaushauri gani kwa watumishi wa Mungu mbalimbali?

Milca:Maoni yangu juu ya watumishi wa Mungu ni kuwa waangalifu jinsi tunavyoipokea teknolojia hii maana inakuja na vishawishi vilivyojificha sana ambavyo adui anavitumia kupungua focus ya huduma zetu na kukalia vitu ambavyo viko nje ya mpango wa Mungu.Ni muhimu sana kuwa katika maombi juu ya huduma zetu zote maana vita tuliyomo inahitaji silaha kubwa zaidi ambayo maombi tu huweza kushindwa yote.




Her  favourite Colour 
 Brown
Her Favourite Hymn(Tenzi) 
 Naupenda Msalaba Huu
Nje ya uimbaji 
 Mimi ni mama ushauri na mwalimu wa wanawake
Her Best Bible verse 
Yeremia 29:11( Maana nayajua mawazo ninayowawazia...)


                                    Mungu awabariki

Milca L.Kakete


You might also like:

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...