11 April 2012

Rais Obama asema, akumbukapo Ushindi wa Yesu Msalabani, humtia Nguvu akutanapo na magumu katika uongozi wake



Rais Barak Obama akiwa na watumishi wa Mungu ikulu ya Marekani wakati wa Easter Breakfast 2012
Mapema Asubuhi ya Jumatano iliyopita Rais Barak Obama wa Marekani aliwaalika Watumishi wa Mungu mbalimbali walioko nchini humo kwa ajili Easter Prayers Breakfast. Katika asubuhi hiyo Rais Obama aliwaongoza wageni wake katika kupata kifungua kinywa(Breakfast) kwa pamoja kasha watumishi hao wakawa na muda wa kufanya maombi.

Katika tukio hilo Rais Obama aliwaambia watumishi hao umuhimu wa Mapumziko ya Pasaka (Easter Holliday) kwa wakristo. Obama aliendelea kusema Yesu alituletea ukombozi wetu kwa kuwa aliweza kuikabili hofu iliyokuwa ndani yake.Leo tunasherehekea Pasaka kwa kuwa Yesu aliishinda hofu iliyokuwa ndani yake pamoja na maumivu makali yasiyoweza kuelezeka.

Akiongea na watumishi hao Rais Obama alisema yeye ni mmoja kati ya watu ambao hujiuliza nini mpango wa Mungu juu ya Maisha yake, akasema lakini anapokumbuka safari ya Yesu msalabani na namna ambavyo Yesu alivyoshinda Mashaka na woga uliokuwa ndani yake  na kisha kutukumboa msalabani, humtia nguvu hususani kipindi anapokuwa katika wakati mgumu wa uongozi wake.

Huu ni mwaka wa tatu Rais Barak Obama amekuwa na wasaa wa kuandaa Easter Breakfast Prayers ambapo huwaalika watumishi mbalimbali katika Ikulu ya Marekani katika ukumbi wa East Room.

Rais Barak Obama akiwa na watumishi wa Mungu ikulu ya Marekani wakati wa Easter Breakfast mwaka jana 2011


You might also like:

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...