24 April 2013

Mchaka Mchaka wa Africa Gospel Music Awards 2013 Yaanza Rasmi

Kwa Mara ya nne mfululizo Africa Gospel Music Awards imechukua Mkondo wake.
Ule Mchakato ambao Mwaka Jana Bloggers Wa Tanzania waliubebea Bango wa Africa Music Awards baada ya Mwanamuziki Christina Shusho Kuingia katika Kinyang'anyiro hicho mwaka huu umeanza rasmi.

Taarifa kupitia tovuti ya Africa Gospel Music Awards na Facebook Page Wametoa Press Release kutaarifu Jamii Kuwa Mchakato huo umezinduliwa rasmi kwa ajili ya kusaka Wanamuziki Bora wa Injili Africa kuanzia tarehe 22 April, 2013.

Utaratibu Uko Kama Ifuatavyo.

Tarehe 22 April Mpaka tarehe 13 May, 2013 Kila Mwananchi anaruhusiwa kupendekeza Jina ambalo anaona linafaa kuingia katika kinyang'anyiro hicho. Njia ni rahisi tu unatuma email kwenda nominations@africagospelawards.com  unaandika jina unalodhani linafaa.

Kuanzia tarehe 1 June mpaka 30 June Kutakuwa Kuna Kupiga Kura kwa Majina yatakayokuwa yameingia katika Kinyang'anyiro hicho ili kupata Washindi katika Categories zifuatazo.


1.DISCOVERY OF THE YEAR
2.ARTISTE OF THE YEAR EUROPE
3.ARTISTE OF THE YEAR EAST AFRICA
4.ARTISTE OFTHE YEAR WEST AFRICA
5.ARTISTE OF THE YEAR NORTH AFRICA/MIDDLE EAST
6.ARTISTE OF THE YEAR SOUTHERN AFRICA
7.ARTISTE OF THE YEAR CENTRAL AFRICA
8.ARTISTE OF THE YEAR USA/CANADA
9.ARTISTE OF THE YEAR AUSTRALIA/ASIA PACIFIC
10.SONG OF THE YEAR
11.ALBUM OF THE YEAR      
12.MALE ARTISTE OF THE YEAR
13.FEMALE ARTISTE OF THE YEAR
14.MUSIC PRODUCER OF THE YEAR
15.RADIO PROGRAM OF THE YEAR
16.MUSIC VIDEO OF THE YEAR
17.  EVENT OF THE YEAR
18.  AFRO JAZZ/INSTRUMENTAL MUSICIAN OF THE YEAR
19.GOSPEL RADIO PRESENTER OF THE YEAR
20.GOSPEL TV PROGRAM OF THE YEAR
21.GOSPEL TV PRESENTER OF THE YEAR
22.GROUP /CHOIR OF THE YEAR

Mwaka Juzi na Mwaka Jana Mwanamuziki Christina Shusho aliingia katika Kinyang'anyiro hicho. Ambapo Kampeni hiyo Ilipewa jila na "Viva Shusho, Viva Tanzania"
Mwaka Jana Wakati Wa Campaign za Shusho ndani Ya Clouds Radio

Bloggers nza Shusho Ndani Ya Clouds FM

Campaign Manager Ze Blogger akiwa na Shusho

Kaka Mkubwa Pastor Harris Kapiga akiwa na Kikosi Kazi.
Mwaka huu Nani Kuiwakilisha Tanzania??

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...