MAZISHI YA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA UINGEREZA MARGRET THATCHER YAFANYIKA MJINI LONDON
VIONGOZI na watu maarufu katika nchi 170 kote duniani wako mjini London kuhudhuria mazishi ya waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Margret Thatcher maarufu kama Iron Lady.
Bendera kote nchini humo zimepeperushwa nusu mlingoti kutoa heshima kwa mwendazake Margret Thatcher aliyekuwa akiugua kiharusi na kufariki tarehe 8 mwezi huu akiwa na umri wa miaka 87.
Sio wote wanaoomboleza kifo cha Thatcher
Hata hivyo sio wote nchini Uingereza wanaoomboleza kifo cha bibi wa
Chuma-Iron Lady, Mamia ya wapinzani wa kisiasa wamesema watanyamaa kimya
kwa dakika moja na kulipa mgongo jeneza hilo litakapopitishwa.Takriban dola milioni 15 zimetumika katika mazishi hayo.
Jeneza la Margret Thatcher kwa sasa linapitishwa kutoka katika majengo ya bunge, kupelekwa katika kanisa la St. Clement Danes, kisha kuwekwa katika msafara wa farasi na kuanza kusafirishwa tena pole pole hadi katika kanisa katoliki la St Paul ambako wageni waalikwa takriban 2300 akiwemo Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza watakuwepo kupokea mwili huo.
Usalama waimarishwa.
Polisi takriban 4000 wamesambazwa kote mjini humo kuimarisha usalama.
Kiongozi huyo wa zamani ambaye alipewa jina hilo la Bibi wa Chuma- Iron
Lady aliibadilisha Uingereza katika kipindi cha miaka 11 alichoongoza
kama waziri mkuu wa nchi hiyo kuanzia mwaka wa 1979 hadi 1990. Wageni maarufu waliotoa udhuru wa kutohudhuria mazishi hayo ni kiongozi wa zamani wa kisovieti Mikhail Gorbachev na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel atawakilishwa waziri wake wa mambo ya nje.
Hata hivyo familia ya Bill Clinton na George Bush zilikataa kuhudhuria mazishi hayo.
No comments:
Post a Comment