03 February 2012

Uche Chukwu Agu mwibaji wa nyimbo maarufu barani afrika iitwayo My GOD is good (Double Double)


Uche Agu ni Mwanamuziki wa nyimbo za injili na raia wa Nigeria anyeishi nchini Afrika ya kusini, moja kati ya mafanikio yake ni kunyakua tuzo ya mwanamuziki bora wa nyimbo za injili barani afrika. Hivi sasa nyimbo yake ya My GOD is good oohh ambayo wengine huiita Double Double aliyoifanya na kundi maarufu la injili nchini afrika ya kusini liitwwalo JOYOUS CELEBRATION imesambaa Afrika nzima na imekuwa gumzo hali iliyomfanya kuwa maarufu kwa muda mfupi.

Uche anastashahada ya Theologia kutoka World Harvest Theological College na huongoza sifa na kuabudu katika huduma iitwayo Halleluya Ministry International yenye makazi yake nchini Afrika ya kusini katika jiji la Johanesbag. Tarehe 7 mwezi wa tatu mwaka huu alialikwa nchini Ghana katika tamasha kubwa la kipekee lililoiywa Independence Praize 2011

                      Everything is Double Double by Atta Boafo;
Atta Boafo ni kijana wa kighana kutoka katika jimbo la Kumasi ambaye amekuja na nyimbo hiyo ya Double Double toka kwa Uche ila kwa staili yake mwenyewe. Kitanzania Tanzania tunaweza iita Remix, Boafo amesomea muziki kwa kipindi kirefu na nyimbo yake hiyo imesambaa sehemu nyingi pia barani afrika. Unaweza kuiona  Everything is Double Double by Atta Boafo kwa kuclick hii video hapo chini

HISTORIA YA MWANAMUZIKI WA INJILI EPHRAIM SEKELETI MUTALANGE;


Ephraim Sekeleti Mutalange ni muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Zambia, alizaliwa Mwaka 1983 katika mji wa Kalulushi nchini Zambia. Alimaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya Kalulushi mwaka 2001.

Ephraim ni mtoto wa pili toka mwisho kati ya watoto sita, aliingia kwenye muziki wa injili tangu akiwa kinda huku alifundishwa kupiga kinanda na mmishonari alipokuwa bado mdogo. Mama yake anasema  “ Ephraim alikuwa ni mtoto aliyekuwa wa kelele nyingi”. Yeye pamoja na dada zake waliimba kanisani wakitumia kinanda na huko alipata uzoefu katika uimbaji na upigaji wa kinanda. Baadaye alijiendeleza katika uimbaji kwenye kikundi kilichojulikana kwa jina la  “Virtue for Christ” na aliimba katika kikundi hicho kwa muda wa miaka miwili.
 Mwaka 2002 akiwa na kiu ya kurekodi album yake, Aliamua kujitoa muhanga kwenda Afrika ya Kusini kwa kutumia kiasi kidogo tu cha pesa alichokuwa nacho, nia ilikua ni kurekodi album yake ya kwanza. Pamoja na jitihada hizo, baada ya kufika nchini Afrika ya Kusini alijikuta anaweza kurekodi nyimbo mbili tu kati ya album nzima. Hivyo akaamua kujiingiza katika Theater ya Pretoria na ndipo akapata fursa ya kuimba mbele ya Rais wa Afrika ya Kusini. Nafasi nyingi ziliendelea kujitokeza zilizomsababishia kutaka kuacha kuendelea na muziki wa injili ili aimbe miziki ya kidunia, lakini akawa muaminifu kuendelea na uimbaji wa injili. Mlango ulifunguka kumruhusu kurekodi album ya kwanza iitwayo Temba Baby“(Mtoto wa Miujiza)”.

Baada ya kurekodi, na kuuza nakala za kutosha za album hiyo ya Temba boy, kwa mafanikio ya hiyo kazi Ephraim aliamua kurudi nyumbani kuwekeza ile fedha. aliona awekeze zaidi kwenye ya album yake ya pili iliyopata mafanikio makubwa iliyoitwa Limo Ndanaka. Hi album imefanya vizuri kwenye chati mbalibali za muziki wa injili. Ephraim akiwa nje ya Zambia ameimba katika nchi mbali mbali zikiwemo Namibia, Afrika ya Kusini, Tanzania, Zimbawe na Australia.

Alisema anafurahi akiona watu wasiokuwa na tumaina la Kristo wakianza kuwa na matumain, Licha ya kufanya muziki wake nchini Zambia amewahi kuja nchini Tanzania na kurekodi album yake nzima kwa Lugha ya Kiswahili. Moja kati ya Nyimbo zake zinazotamba hapa nchini ni pamoja na

                                             1. Uniongoze                                
                                             2. Baraka Zako
                                             3. Huu Mwaka

                  NYIMBO ZAKE CHEKI  VIDEO HAPO CHINI;
                                      Ephraim - Amapalo (chawama)

                                 
                                         Ephraim - Lesa fye Umwine

                                          
                                           Ephraim - Limo ndanaka



 Ephraim hajui Kiswahili fasaha na nyimbo zake hizo alifundishwa kuziimba kwa lugha ya Kiswahili na Mchungaji ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania Ency Mwalukasa. Ephraim amesema ataendelea kuhubiri kwa njia ya uimbaji kwa sababu imempa changamoto zilizomuinua. Licha ya uimbaji Ephraim amefunga ndoa na Faith Chelishe na wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike
                                                     Mtoto wa Ephraim
        ALBUM YAKE MPYA YA KISWAHILI IITWAYO VIGELEGELE
                 
                                NYIMBO MPYA CHEKI  VIDEO HAPO CHINI

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...