Tuesday, February 21, 2012
Umetenda Mema – Kambua Shooting si Ya Kitoto
Kambua |
Kambua ni muimbaji wa nyimbo za Injili mwenye jina kubwa nchini Kenya, alianza kuimba na kupenda nyimbo za Injili alipokuwa mdogo na watu wengi waliona kilichokuwa ndani yake, baadaye mwaka 2005 akaenda kusomea Muziki nchini Canada chuo cha Kikristo, Calgary. Na katika maisha yake chuoni, alijiunga na band ya chuo Legacy Youth Conference (LYC). Anasema alipokuwa Canada, hawezi kusahau alipochaguliwa kuimba na Angelique Kidjo kwenye tamasha moja.
Kambua ambaye mama yake ni mchungaji, mbali na nyimbo zake kupigwa redioni na kuonekana kwenye TV pia na tuzo alizopokea haachi kusema kwamba maisha yake ameyatoka kwa Bwana Yesu na kusoma Neno lake mara nyingi.
Muimbaji huyu amekuwa akifanya huduma aliyonayo kwa kushirikiana na waimbaji wengine na kuuinua muziki wa Injili kwa kuiwakilisha nchi ya Kenya na hata Afrika mashariki.
Wakati wa Shooting Ya
Ametamani kuwa sauti ya wanawake na watoto katika kujenga maendeleo ya nchi zinazoendelea, mbali na shughuli za jamii na uimbaji Kambua pia ni mtangazaji wa Citizen TV, kipindi cha Rauka.
Kambua Akiwa anafanya Shooting.
Pozz la Ukweli.
Kazi Ya Shooting si Mchezo, chini kushoto ni redio ya kusikilizia mziki huku ukienda sawa
Uzuri Unachangia Muonekano.
Kambua akiwa mbele ya KinandaKambua akituma Vocal
Kitu Quality
Shooting si Mchezo, hapa akiwa na Backer wake.
Kazi nzuri ya Kambua.
Baadae Mpango Mzima Ukakamilika Ukawa namna hii.
No comments:
Post a Comment