17 February 2012

LIVE RECORDING BONDENI


MUNGU ATUKUZWA RECORDING YA NTOKOZO MBAMBO WA JOYOUS CELEBRATION

Joyous Celebration ni Next Level


Ntokozo akimsifu Mungu usiku wa kuamkia leo wakati wa recording



Wapenzi wa muziki wa injili nchini Afrika kusini waliofika katika live recording ya mwanadada Ntokozo Mbambo wa Mbatha iliyofanyika katika ukumbi wa Gold reef city lyric theatre jijini Johannesburg,wamenukuliwa wakisema kwamba recording hiyo ilikuwa level nyingine uwepo wa Mungu ulifunika ukumbi huo kwani kila jambo lilikwenda vyema na watu kupokea kutoka kwa Mungu zaidi wakimpongeza mwanadada huyo sambamba na mumewe Nqubeko kwa kazi nzuri


Ntokozo ambaye toleo lake la kwanza alilitoa mwaka 2007,amekuwa kati ya nyota wa muziki wa injili nchini Afrika ya kusini kutokana na nyimbo alizoimba kwakutunga yeye mwenyewe nazile za kukopi kutoka kwa waimbaji wengine duniani  akiwa pamoja na kundi la Joyous Celebration ambako kwasasa ndiye mnoaji wa sauti wa kundi hilo huku mumewe akiwa mtayarishi wa muziki wa kundi hilo akishirikiana na kiongozi wa kundi hilo Pastor Mthunzi Namba


Mrs Mbatha alikuwa kwenye kiwango chake cha uimbaji

Khaya Mthethwa mmoja kati ya waimbaji wa Joyous akiimba kwahisia 



katika uzinduzi wa jana Ntokozo alisindikizwa na waimbaji wenzie wa kundi la Joyous ambao wengine walikuwa wapigaji na  back up vocalist na wengine wakiwa watazamaji, kabla ya uzinduzi huo ambao dalili za kuwa lingefanikiwa zilionekana mapema baada ya ticket kuwa sold wiki moja kabla ya recording yenyewe,ambapo Ntokozo aliisimamia recording yake kwa neno kutoka matendo 2;2, ambapo alinukuliwa akisema '' I have something to say through music which is inspired by God. I'm a believer in NOT just in releasing for that sake of releasing an album'' alisema.


Kutoka kushoto Hlengiwe,Kuki(mwimbaji wa zamani wa joyous)pamoja na Zodwa mahlangu sauti ya pili matata ndani ya Joyous 



Nqubeko akiwa anamsifu Mungu wakati wa recording

Ntokozo akimuangalia mumewe wakati akiimba kwenye drums kijana Siyabulela wa joyous akiwa busy huku jicho akiwakodolea wapendanao


Ntokozo pamoja na mumewe Nqubeko mwaka jana walishinda tuzo za sabc crown gospel kwa category za best producer na classic of all time,ambapo mumewe naye anatarajia kuachia dvd yake wakati wowote kutoka sasa ambapo audio yake inayojulikana kwa jina la forever i'll worship inafanya vyema sana nchini humo

Kutoka kushoto Hlengiwe,Mahalia,Lihle pamoja na Sibongiseni



Kitu Live Hiki

Kwenye Joyous ya 15-2

Source: Gospel Kitaa Blogspot.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...