27 February 2013

Glorious Celebration Kuwa Glorious Worship Team

Kukiwa bado kuna Sintofahamu kubwa imetanda kati ya Waimbaji Waliokuwa wa Kundi la Glorious Celebration na Mmiliki wa Glorious Celebration Company, baadhi ya Waimbaji wa Kundi hilo wamejitoa chini ya Mmiliki huyo na Kuunda Kundi la Glorious Worship Team.

Kwa Miezi Kadhaa kupitia vyombo vya habari na mitandao Jamii kumeibuka sinto fahamu kati ya pande mbili Waimbaji na Mmiliki Wa Kundi hilo Askofu Mwakang'ata. Waimbaji Karibia Wote wa Kundi hilo Wamejitoa chini ya Mmiliki huyo kwa madai Utata Ulioibuka baada ya Mmiliki Huyo Kuamua Bendi Hiyo Kujiendesha Kama Kampuni badala ya Mfumo wa Awali, Pia Blog kwa kuongea Waimbaji Waliojitoa wa Kundi hilo imebainika kuna sababu zaidi ya hizo kwa manufaa ya Mwili wa Kristo sababu hizo hazitawekwa hadharani kwa sasa. Upande Wa Mmiliki wa Bendi Hiyo Askofu Mwakang'ata alieleza mbele ya Christian Bloggers siku ya tarehe 23 Feb, 2012 alipowaita Wanahabari alieleza kuwa kundi hilo liliamua Kuasi liliamua kujitoa baada ya Yeye Kama Mmiliki Kuamua Kuboresha Njia za Kuboresha Mapato Yanayoingia Kupitia Kundi hilo. Ameeleza amekuwa akilihudumia Kundi hilo kwa kutoa fedha za Kanisa na fedha binafsi lakini kundi hilo limekuwa haliingizi fedha kama ilivyokuwa ikitakikana na ndipo alipoamua kuuboresha mfumo huo uliokimbiza Wanamuziki hao "Waasi".

Baba Askofu alitoa maelezo kuwa Glorious Celebration bado ni Mali yake na Glorious Celebration inaingia Kambini Jumanne (kesho) Nje kidogo ya Mkoa wa Dar kwa ajili ya Kujisuka upya baada ya baadhi wa imbaji katika Kundi hilo. Wakati Huo huo Waimbaji Waliojitoa Wamedai Kutokana na Mzozo uliotokea baina yao na Mmiliki Kudai Jina la Glorious Celebration ni male yake wameamua kuboresha kutoka GC na kuwa GWT yaani Glorious Worship Team. Uzinduzi wa Jina hilo na Kutimiza Miaka Miwili Ilifanyika Jana Katika Viwanja Vya Atriums Hotel na Kuhudhuriwa na Umati Wa Watu.

Story Nzima Ya Mahojiano ya Mmiliki na Waimbaji Walioamua kujitoa Itarushwa Katika Kipindi Kipya Cha Tv.....Chini Ya Ze Blogger na Uncle Jimmy Kupitia Kituo Chako Bora Kabisa Cha Clouds Tv.
 OG Akikanyaga Codes za Muziki 
 Kibambe Kama Kawa akikanyga MOTIF
 Hawa Wapigaji Solo na Drums ni Noooouuuuma sana
 Glorious Wakienda Sawa Siku Ya Jana
 Kama Kawa Paul akiongoza Jahazi
 Glorious Kama Kawaa
 Hapo Sasa
 Linah Sanga and Uncle Jimmy wakiwa wanacheza

 Hahah Joel Mlabwa Damu Mpya ya Glorious 
 Kikosi Kile Kile Jina Likingine GWT
 Kikosi Kazi
 Kundi bado Imara GWT

21 February 2013

"Filled" Ya Ntokozo Mbambo Yafanya Vizuri Katika Soko


Kupitia Facebook Page Ya Mwanamuziki Wa Injili Kutoka South Africa..Ntokozo Mbambo ambaye amejitoa katika Kundi la Joyous Celebration Mwaka Jana na Kutengeneza Albam yake ya Kwanza akiwa Nje ya Kundi hilo amefunguka na kusema albam hiyo ya Filled Imefanya vizuri katika mauzo yake.

Kupitia Page hiyo imeeleza kuwa mpaka sasa Copy 25,000 zimeshaondoka sokoni kwa kununuliwa na watu mbalimbali. Kwa hesabu nyepesi ya Copy ni shilingi 5000 ya Kitanzania, basi Mwanamukizi huyu ametengeneza Jumla ya Shilingi 125,000,000 kupitia uuzaji wa Copy hizo. Hii ni changamoto kwa Wanamuziki na Serikali yetu ya Tanzania katika Kulinda na Kusambaza kazi za Wasanii.

Thokozo Mbambo ni Mke wa Aliyekuwa Music Director wa Joyous Celebration Mr. Nqobeko aliyejitoa kwenye kundi hilo wiki chache baada ya Mke wake kujitoa.

Haya ni Maneno aliyoyasema masaa machache yaliyopita.'
"God has done it again! Just six months after releasing "Filled", the album has gone GOLD! I just got confirmation from Universal that we have sold over 25 000 copies of the album! Thank you all so much for your love and support - "To God be the glory!"
...for those of you who are still planning on getting it. Remember you can get the CD or DVD at your local music store, or follow this link and download it here, or alternatively on iTunes"
.


Wanamuziki Wa Injili Tanzania Waimba Wimbo Wa Kuiombea Amani Tanzania



Wanamuzi mbalimbali Wa Injili Tanzania wamejikusanya na kutengeneza Wimbo Mmoja wa Kuimbea Amani Tanzania. Wimbo huo wenye Jina La "Mungu Iponye Tanzania" umewakutanisha Wanamuziki Mbalimbali wa hapa Nchini.

Blog ikifanya mahojiano na mmoja wa Waratibu wa Project hiyo David Robert ameeleza kuwa Wimbo huo umewakutanisha Wanamuziki Mbalimbali Tanzania kwa ajili ya Kumuomba Mungu kwa ajili ya Amani.

"Siku Moja nikiwa na Bahati Bukuku Likatujia Wazo Kwanini Tusifanye Wimbo Wa Kuombea Amani Tanzania, It was very strong in our hearts, then tukaanza utaratibu wa Kuwatafuta Wanamuziki na Kuwasiliana nao walipo, Ilipata Muitikio Mkubwa sana, Rose Muhando, Bahati Bukuku, Florah Mbasha na wengine wengi unaowajua tukakaa pamoja tuka record, na Jana ndio tumemaliza shooting ya wimbo Huo, kwa sasa tunasubiri tu Kukamilika Kisha tutauweka Wakfu wimbo huo"..Haya yalikuwa ni baadhi ya Maneno Ya David Robert.
Papaa Ze Blogger na Zavid Robert

12 February 2013

John Lisu Aachilia Rasmi "Uko Hapa" Ndani Ya CCC

Mwanamuziki Wa Injili Tanzania anayepiga Muziki wa Live, John Lisu Leo amezindua albam yake ya Pili yenye Jina la "Uko Hapa" Mwanamuzi Huyo ambaye alifanya uzinduzi katika Kanisa Maarufu la CCC na Kuhuduriwa na maelfu ya Wakazi wa Jiji la Dar.

Uzinduzi huo uliosindikizwa na Wanamuziki wengine wa Injili kama Cosmas Chidumule, The Voice, Pastor Safari, Glorious Celebration na Next Level lilikuwa ni Tamasha la Aina yake.

John Lisu akiongea na Blog anasema "anamshukuru Mungu kwa idadi ya watu waliojitokeza, anamshukuru Mungu pia kwa uwepo wake uliowagusa watu katika Uzinduzi huo.

John Lisu amezindua albam yake ya pili ya audio yenye jumla ya nyimbo 11 na itaanza kupatikana kuanzia siku ya leo.
 Mdau wa Blog Hii Pascal akiwa na Mkewe Dativa wakiwa ndani ya Ukumbi wa CCC
 Kwa Mbaliiii
 Bishop Dr. Ranwell Mwenisongole akifungua rasmi tamasha hilo
 Swahiba akiwa mbele ya Mojawapo wa Kazi zake alizomfanyia Lisu, Prosper Mwakitalima ndiye aliye Print Tshirt, Banners na Tickets, Pia ndiye aliye buni.
 Daniel akiwa na Amani wakienda Sawa
 Music Director, Sam Yona
 Waimbaji Wakienda Sawa
 John Lisu akiongoza Kikosi kwa ajili ya Kazi
 Habari Ndo Hii
 Waimbaji Wa John Lisu wakienda sawa
 Watu wakienda sawa
Mke Wa John Lisu akipiga mojawapo ya nyimbo leo jioni.

10 February 2013


Sunday, February 10, 2013

NABII T.B.JOSHUA ATABIRI USHINDI TIMU YA NIGERIA SUPER EAGLE NA AFCON 2013....NA HII YATOKEA KWELI!!!!!



Mtumishi wa Mungu kama ilivyo kawaida yake ya kutabili jambo na linatokea. Amekuwa akitabili matukio makubwa sana dunia kama kifo cha Michael Jackson na mengine mengi ambayo ukitaka kujua ingia katika blog zake na YOUTUBE.

Safari hii, Mungu alimuonyesha ushindi katika ya timu ya Taifa ya Nigeria Super Eagle na timu ya Afrika kusini ya Burkina Faso ambazo zilikuwa zikipambana katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Afrika kusini.

Rumafrica imekuletea dondoo kwa lugha ya Kingereza kamazilivyotolewa katika mitandao mbalimbali
 
Nabii T.B. Joshua

PROPHECY: “How Nigeria Will Win AFCON2013 Final” – TB Joshua

The General Overseer of The Synagogue Church Of All Nations, Prophet Temitope Balogun Joshua, says Nigeria’s Super Eagles would defeat Burkina Faso in Sunday’s final of the Africa Cup of Nations in South Africa.

T.B Joshua, who warned Eagles’ coach, Stephen Keshi to avoid conceding a late minute goal in their AFCON Group C opener against the Burkinabe, told P.M.NEWS that Nigeria’s case in the Nations Cup final this year is like the biblical Jacob who wrestled with God, saying that “on Sunday we’ll tell God unless He gives us our heart’s desire we’ll not let Him go”.

“The cloud is darker over Nigeria’s Super Eagles, but with God we’ll scale through. If it were not to be the final, anything could have happened. The first match we played with Burkina Faso, it was just by the grace ofGod that it ended in a draw.
Click for Full Image Size
“On Sunday, our opponents will play defensively because they will be looking outfor penalty shootout at the end of the game. They will also play through three of their strikers upfront; one of them very tall and huge player and two others. “What I’m seeing I don’t want to say it because it would be too frightening, but I want to assure that we’ll scale through the challenge on Sunday.”

The prophet who established a football club,My People FC to groom young players, however, warned the Eagles not to allow Burkina Faso to score first in the final, sayingthat “if this happened the Burkinabe would fall back to defend the goal, which will be very dangerous for our team. I still repeat that no matter the situation, we’ll scale through.

“The Burkina Faso that we played in the group stage will not be the same team we’ll play on Sunday, even though some of their players are out of the squad due to injuries. They are still a team. But I hope for celebration.”

Joshua said as the giant of Africa, Nigeria last won the Nations Cup 13 years ago, which was too long ago for a great football nation like Nigeria.

“I think God should give us this cup to make the youths of this country happy. Winning this cup at this time of religious intolerance and violence will calm down the youths. I want to appeal to all Nigerians to pray for Eagles’ victory. I would have told you the scoreline but I would rather delay it till Sunday morning in order not psychologically distract the players and their coaches and not to demoralise the losing team.”

Prophet Joshua concluded that he would notwant Keshi and his team to come to his church to celebrate their victory after the match because he is not the only one praying for the Eagles to win.

“My voice may be the one louder among the men of God in the country but this doesn’t mean that the team should come to my church to celebrate.

I would rather prefer that they celebrate their victory with all Nigerians,” he said.

08 February 2013

Jesca Honore Kuvunja Ukimya na Albam ya "Nimevunja Ukimya"

Mwanamuziki Mahiri wa Injili aliyejitoa kutoka Kundi la Glorious Celebration ameiambia blog kuwa anatarajia kufanya mambo makubwa 2013 katika tasnia ya Muziki wa Injili hata Tanzania. Mwanamuziki huyu ame-efatha mbele ya Blogger na kueleza mipango yake ya 2013 lakini pia akieleza kuwa Mwezi May Mwaka huu anatarajia kufunga pingu za Maisha na Mtangazaji wa Kituo Cha Tv hapa Tanzania.

Katika kueleza Mipango yake Mwanamuziki Jesca Honore ameeleza kuwa mwezi March, 2013 tarehe 10 anatarajia kufanya Preview Ya Vision yake katika Muziki wa Injili lakini Pia Kuzindua Eneo la Serena Hotel kama sehemu ambayo atakuwa akifanya Muziki Wa Injili Kila Ijumaa sehemu hiyo.

Akizungumza na Blog Hii Jesca Honore amesema anatarajia kuzindua albam yenye jina la "Nimevunja Ukimya" ulio katika mahadhi ya Kwaito na Katika Uzinduzi huo Utakaofanyika Serena Hotel Utaambatana na Preview ya Vision Ya Jesca Honore. Albam hiyo yenye mchanganyiko wa Mahadhi mbalimbali imefanywa katika Viwango Vya Kimataifa.


Mungu akutumie katika huduma yako mpya!!!Hapa Glorious Celebration tunakutakia Mema....md

07 February 2013

7,2, 2013

Mpiga Drums Nambari One Wa Joyous Celebration Ajitoa



Mwaka Jana Mapema kabisa Wanamuziki Maarufu Mume na Mke walijitoa katika Kundi Maarufu la JC mwaka huu majira yale yale Mpiga drums nambari wa Joyous Celebration mwenye jina la Siyabulela Satsha ametangaza Kujitoa katika kundi hilo na baada ya Mkataba wake Kumalizika.


Joyous Celebration imekwisha kutoa nafasi ya Kazi ya Jembe hilo ambalo taarifa za Awali zinasema anakwenda kufanya kazi pamoja na Wanamuziki wengine waliokuwa katika kundi hilo na Kujiondoa mapema mwaka jana.


Kumekuwa na mapendekezo kadhaa ya dogo aliyeonekana katika JC 15 miaka miwili iliyopita kuziba gap la mpiga drums huyo. Oyanda ambaye amekuwa akifanya mazoezi na JC kwa muda mrefu ambaye pia ni mmoja wa wanaosadikika kuchukua fomu kwa ajili ya nafasi hiyo anapewa nafasi kubwa zaidi ya kuwa mbeba mikoba hiyo. Changamoto kubwa ni umri alionao Mwanamuziki huo ambapo kwa sasa anamiaka 12-13 na bado yuko shuleni.


NABII FLORAH MTUMISHI WA MUNGU!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...