03 November 2012


Friday, November 2, 2012

Mungu Asipokujibu Maombi Yako Muulize Ni Kwa Nini Hajakujibu



SABABU NYINGI AMBAZO MUNGU HAJIBU MAOMBI
ZIPO NYINGI LAKINI NAKUONYESHA AMBAZO NI ADIMU

Mwl. Christopher Mwakasege

1.     KUTAKA KUJIBIWA MAOMBI YAKO NJE YA NJOZI AU NJE YA MAONO YA MUNGU
Habakuki 2: 1 – 3 … Bwana akanijibu, akasema iandike njozi hii  ukaifanye kuwa wazi sana katika …
  • Wakati Habakuki anaomba ondoa uovu/ udhalimu/ haki imepotoka, Mungu amenyamaza, halafu anaenda kuomba kwa nini Mungu hakujibu malalamiko yake ndipo Mungu akajibu!
  • Mungu hakujibu kutatua malalamiko yake ila Mungu alijibu malalamiko yake (Vs. 2 - 3)
Lile neno njozi kwa kiingereza limeandikwa vision na kwa Kiswahili lingefaa kuwa maono.
  • Mungu alikuwa anamwambia Habakuki badilisha aina ya uombaji wako,usiombe kwa kuangalia mazingira yanavyoonekana ila omba kwa kuangalia njozi
NJOZI za aina 3:
a). Njozi yake mwenyewe
b). Njozi ya eneo ambalo analiombea
c). Njozi ya maeneo ambayo habakuki alikuwa ana mazoea ya kukaa au kupita
Habakuki alikuwa anaelewa Mungu alikuwa na maana gani maana hakuna alipomwambia aina gani ya njozi aliandike!
Ndani ya hiyo mistari miwili yapo mambo 7 ambayo sitayataja hapa ila nitayataja kesho, leo  acha nieleze kidogo juu ya njozi/maono / vision. Maana kila mtu hapa atatoa tafsiri yake

MAANA YA NJOZI/ MAONO/ VISION
NJOZI/ MAONO/ VISION NI KUSUDI LA MUNGU LINALOFUNULIWA NDANI YA MTU KWA NJIA YA MFUMO WA PICHA, ni kusudi la Mungu linalowekwa ndani yako linapofunuliwa linakuwa maono/ vision.
Na linapofunuliwa linakupa kuona angalau vitu 3 au kimoja wapo au vyote vitatu kwa pamoja:

1. Kukupa sababu ya kuumbwa kwa kitu/ kuwepo kwa kitu,
Sababu ya kuwepo kampuni/ nchi / ndoa, cho chote kile na unapopewa sababu na ikifunuliwa ndani yako ile sababu inakuwa vision.
Bangi ni mbaya kwa sababu hatujui makusudi ya Mungu kuiumba. Hivyo serikali imepewa na Mungu kuweka sheria ya kuhakikisha kuwa bangi haitumiki vibaya mpaka pale tutakapojua matumizi mazuri ya bangi.
Ajali nyingi za mabasi ni kwa sababu ya utengenezaji wa mabasi, mabasi yana chases yake na magari ya kubeba mizigo yana chases. Unakuta mtu ananunua kichwa cha lorry na anachonga basi, ukilitazama kwa nje unaona linapendeza na linapokimbizwa na kukata kona gari linamshinda dereva kwa sababu halikuundiwa kukata kona likiwa na watu lakini likiwa na mizigo halafu tunasema ni shetani.


2. Kukupa picha ya mwishoni wa jambo ukiwa mwanzoni, maono yanakupa mwisho wa jambo ukiwa mwanzoni mwake. Na unapoona mwisho wake unapata ndani yako msukumo, na mtu asiyeona mwisho wa jambo anaweza kukatishwa tamaa maana hajaona mwisho wake lakini yule aliyeona mwisho wake hauwezi kumkatisha tamaa hata iweje!
Kabla nyumba haijawa nyuma inakuwa nyumba ndani ya mtu. Mchoraji anaweza kuweka kwenye computer na anaonyesha kilichondani yake na hata ukimwambia kuwa hii nyumba haiwezi kujingwa hawezi kukuelewa kwa sababu hameiona

3. Kusudi la Mungu linakupa ‘motive’ (kujua)
Wakati wa kesi za mauaji mahakamani wanachunguza sababu za kuua, i.e wakati hukumu inatolewa wanaangalia sababu ya kuuna na inapokuja kuwa aliua pasipo kukusudia adhabu yake ni tofauti. Kusudi la Mungu kukupa maoni ni kukupa kujua sababu ya kuwepo

WATU WENGI SANA WANACHANGANYA KATI YA WITO NA MAONO

Waefeso 4: 11 – 16  … mitume/ manabii/ waalimu/ wachungaji … KWA KUSUDI LAKE
Unamuuliza mtu wito wake anaeleza maono yake!
  • Kuitwa kuwa nabii, mtume, mwalimu hilo sio KUSUDI ni WITO
  • 2Timotheo 1: 8 – 9 … akatuita kwa mwito mtakatifu … KWA KADRI YA MAKUSUDI YAKE YEYE.
  • USIPOJUA KUSUDI LAKE HUTAJUA MAONO YAKO
  • Mungu aliponiita kuwa mwalimu anakusudi la kuniita kuwa mwalimu.
  • Unapoombea uinjilisti/ uchungani unaombea wito lakini hujaombea MAONO/ KUSUDI LA MUNGU
  • Mungu hawezi kukupa nje ya maono/ kusudi la kukuitia, ukiwa unaomba mkumbushe Mungu ndani ya maono/kusudi alilokuitia na mengine yote atakutimizia. Fedha hazijawa connected na maono! Mungu anakupa pesa kama una maono ya ile pesa/ huduma.
  • Mungu hawezi kumlipa mtu kwa kazi ya hasara
  • Wachungaji wanapata hali ngumu kifedha kwa sababu wanadhani wito ni maono na wanataka Mungu  awape pesa kwa ajili ya wito wakati Mungu anataka atoe pesa kwa ajili ya MAONO

Matendo 13: 36  … akiisha kutumikia SHAURI/KUSUDI LA BWANA…
Si kusudi la Israel/ kusudi la baba yake/ si kusudi la serikali ila KUSUDI LA MUNGU i.e alijua kusudi la Mungu.
  • Kampuni inaweza kuwepo na ukatumikia wito ukasahau kutumikia kusudi la Mungu

Kutoka 25: 1 – 9  … wamjengee HEMA ambalo Mungu atakaa ndani!
  • Kazi ya hema sio kukaliwa na watu ila Mungu
  • 2Samweli 7: 1 – 5 hekalu sio nyumba ya ibada ila NYUMBA YA MUNGU; Kwa sababu Mungu yupo ndani ndio maana ibada inafanyika – kama Mungu hayupo ndani ibada inafanyika ya nini?
  • Ukiacha kufuata kusudi la Mungu usithubutu kuulizia ulinzi wa kusudi la Mungu
  • Mtu aliye ndani ya kusudi na aliye nje ya kusudi wanapata vita vilivyosawa lakini ulinzi unatofautiana

 Mwl. Christopher Mwakasege

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...