Pages

10 June 2012

Sunday, June 10, 2012

Tamasha la John Shaban Magomeni TAG Next Next Level

Mamia Ya Wakazi wa Jiji la Dar-es-Salaam  siku ya Leo walijitokeza kwa Wingi Katika Tamasha la Muziki wa Injili la Ku-m-Support Mwanamuziki Nguli wa Muziki wa Injili John Shaban lililofanyika Jioni Ya Leo Katika Kanisa la TAG Magomeni.

Tamasha hilo lililosukumizwa pia na Wanamuziki Wakongwe kama Cosmas Chidumule, Makasy, John Komanya, Nelly, Stara Thomas, Upendo Kilahiro, Victor Aron na baadhi ya Kwaya Kutoka Jiji la Dar-es-Salaam.

Shughuli nzima ya siku ya leo ilikuwa ikiongozwa na na Mshehereshaji Mashuhuri Mwana Mama Christina Matai. Mgeni Rasmi wa siku ya leo ni Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara.

Tamasha hilo lililokuwa maalum kwa ajili ya Kusifu na Kuabudu na Maombi kwa ajili ya Taifa Letu la Tanzania.
 John Shaban, Stella Joel na Mhe. Mgeni Rasmi Mhe. Waziri
 Mchungaji wa Kanisa la TAG Magomeni Pastor Kanemba akiwa na Mkewe siku ya Leo Kwenye Tamasha.
 Mwanamuziki Stara Thomas akifurahia kilichokuwa kikiendelea Katika Tamasha la siku Ya Leo
 Wakongwe wa Mzuiki wa Injili Nchini Cosmas Chidumule na Mzee Makasy Wakiwa leo kwenye Tamasha.
 Bishop John Komanya kushoto na Kulia ni Upendo Kilahiro ndani ya Tamasha 
 Watu Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 Nelly akiwa Jukwaani Kikazi zaidi siku ya Leo
Bloggers wakiwa Kikazi zaidi siku ya Leo, Kushoto ni Victor, Kati ni Papaa Ze Blogger na Kulia ni Tunu wakiwa Kikazi zaidi siku ya Leo.

No comments:

Post a Comment