Pages

11 June 2012

Mch Creflo Dollar afikishwa kituo cha Polisi baada ya Kumjeruhi mwanaye


Pastor Creflo Dolla
Mchungaji maarufu Duniani kutoka nchini Marekani Creflo Dolla jana ijumaa alikamatwa na Polisi nchini humo kwa kosa la kumuumiza mtoto wake alipokuwa akimkataza kutokwenda kwenye party.Creflo Dollar mwenye mke na watoto watano, alikuwa kimkataza mwanaye mwenye umri wa miaka 15 asitoke kwenda kwenye pary.

Katika purukushani hizo Pastor alimjeruhi mwanaye ambaye naye kwa hasira aliamua kuwapigia simu watu wa usalama ambao walifika na kumchukua Pastor Creflo kwa kosa la kumjeruhi mwanaye.

Pastor Creflo baada ya kufikishwa kituoni na kutoa maelezo aliachiwa, alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu sakata hilo mtumishi huyo wa Mungu anayeamini katika mafanikio alisema “mimi kama mzazi nawapenda watoto wangu na siwezi kutumia mikono yangu kuudhuru mwili wa mtoto wangu”.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa mchungaji huyo Bwn Nikki Bonner alisema kesi hiyo itaendeshwa Private kama Baba akimlinda mtoto wake.Nchini Marekani ni kosa kwa mzazi kumpiga mwanaye,pamoja na yote hayo Mch Dollar anatarajia kuhubiri neno kanisani.

No comments:

Post a Comment