Pages

06 May 2012


Sunday, May 6, 2012

Yasemavyo Magazeti ya Kikristo kwa ufupi



Wachungaji wavamia hekalu la Freemasons
Wiki iliyopita Kundi la wachungaji na waumini wa makanisa tofauti nchini Kenya wamevamia hekalu la kundi la siri la Freemason katika mji wa Eldoret na kulazimisha kupiga maombi kwa muda wa nusu saa nzima, wakivunja nguvu za giza na kulipaka hekalu hilo mafuta. 

Mkurugenzi wa huduma ya Kiroho ya Mercy Ministries International Mchungaji Murage Karanja  na Mchungaji  Wellingtone Shiraku wa huduma ya Power House Centre walioongoza uvamizi huo na kufanikiwa kupenya hadi katika madhabahu ya hekalu hilo wakitumia geti kuu huku wakiwa na Biblia mikononi.

Mmoja wa walinzi wahekalu hilo aliyefahamika kwa jina la Alice Ikesi alisema kuwa alipoona kundi kubwa la watu wakiingia eneo la hekalu hilo alikimbia na kufunga mlango kwa ndani.Watumishi hao waliomba wafunguliwe geti waingie katika eneo la ibada la jengo hilo walikataliwa hadi walipo ng`ang`ania ndipo walikuwabaliwa na kuingia hadi kwenye madhabahu ya jengo hilo na kuendeleza maombi.

Mchungaji anusurika kutoswa Baharini
Mchungaji George Mwamakula wa Kanisa la TAG Ruanga mkoani Lindi amenusurika kutoswa baharini alipokuwa akitoka katika kisiwa cha utalii cha Kilwa.Mch Mwamakula alienda katika kisiwa hicho mara baada ya  kumaliza mkutano wa injili na semina ya Neno la Mungu katika kanisa la TAG Kilwa mkoani Lindi ambapo watu wenye vifungo mbalimbali walifunguliwa huku wengine wakimpokea Kristo kama bwana na mwokozi wa maisha yao.

Kisiwa cha Kilwa

Mtumishi huyo aliliambia gazeti la Jibu La maisha kuwa alipokuwa ametoka katika kisiwa hicho alichoenda kuangalia vivutio mbalimbali vya utalii baada ya mkutano na semina kwisha,alipanda boti ambapo abiria wengie walioaminika kuwa ni waalimu wa madrasa waliwaamuru watu wote waliopanda boti hiyo waanze kuswali.Mch Mwamakula aliyekuwa akiomba kimya kimya aligoma kufanya hivyo ndipo walopomwambia watamtosa baharini. Wakiwa wamejiandaa kumfunga na kumtosa baharini Mch huyo hivyo aliwajibu kuwa “mnataka kuua mwili hamwezi kua Roho hivyo kwangu mtakuwa mmeniacha salama” 

Jambo hilo liliwafanya  wataharuki na kukaa kimya kwa muda, wakati wakiendelea kushangaa kwa mbali kidogo tukawa tunakaribia baharini, Mch Mwakakula aliendelea kusema “ Namshukuru Mungu kwa kuwa ni kama aliwafumba macho hata washindwe kutimiza azma yao.

Wekezeni Mbinguni na Sio Harusini
Mwakilishi wa Meya wa jiji la Dar es salaam Dr Didas Masaburi aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Gosheni  lililopo chanika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.Zaidi ya shilingi millioni 34 zilichangwa ikiwa ni ahadi pamoja na fedha taslimu

Dr Masaburi alisema kuchangia kwenye mambo ya sherehe kama harusi ni vyema  lakini ni vyema zaidi endapo watu wakawekeza Mbinguni  ili wapate baraka za Mungu kama ilivyokuwa kwa Ezekiel ambaye alikuwa katika hali ya kufa  lakini alipomkumbusha Mungu  jinsi alivyojitoa katika kumtumikia ikiwa ni pamoja na kumjengea nyumba Ezekiel aliongezewa miaka ya kuishi.

Gazeti la Nyakati
Gazeti Huru la Kikristo la kila Wiki

Mwimbaji maarufu wa Injili atajwa kuwa ni Freemason
Upepo wa nani ni mwanachama wa Fremason umeendelea kuvuma huku mtumishi mmoja wa Mungu maarufu na muimbaji wa nyimbo za injili akitajwa kuwa ni mmoja wa wanachama wa kundi hilo.Kauli hiyo imetolewa na mtumishi wa Mungu ambaye pia ni kiongozi wa huduma ya Gombogambusi ajulikanaye kwa jina la Mwl Allister Albano.Mtumishi huyo wa Mungu aliyasema hayo wakati akifundisha Neno la MUNGU katika mkesha uliokuwa ukifanyika eneo la Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es salaam hivi karibuni.


Mtumishi huyo alienda mbali zaidi na kusema yapo makanisa jijini Dar es salaam maeneo ya Kibamba,Mbezi Luis,Tabata,Mwenge na kadharika kuwa wachungaji wake ni wanachama wa kundi hilo.Nyakati ilipomtafuta mwimbaji aliyetajwa kuwa ni fremasons hakupatikana kwa siku tatu.Mmoja wa wachungaji aliyetajwa kuwa mwanachama wa kundi hilo alipohojiwa kuhusu  ukweli wa uvumi huo, yeye aliuliza endapo anayemtuhumu ameona mwenyewe kama mwanadamu au ameoyeshwa na Mungu,kisha akaendelea kusema  nadhani huyo anayenituhumu anataka freemason waje hapa kanisani ili tuwape Neno wamjue Yesu Kristo.

Wakristo wamlaani mchungaji aliyechoma moto Quran
Mchungaji Terry Jones anayechunga kanisa moja mjini Gainesville ,Florida nchini Marekani amechoma moto kitabu cha dini ya kiislam yaani Quran, tukio hilo limelaaniwa vikali na makundi mengi ya kikristo likiwemo shirika la kikristo la World Evangelical Alliance(WEA). Shirika hilo limesema tendo hilo sio la kibiblia kwa kuwa hakuna andiko linalotutaka wakristo tufanye hivyo.

Mchungaji Jones anapinga vikali kitendo cha serikali ya Iran cha kumweka kizuizini Mchungaji Youcef Naderkhani anayetuhumiwa na serikali ya nchi hiyo kwa kueneza ukristo  tendo ambalo kwa serikali ya nchi hiyo ya Iran ni kosa kubwa.



Msemakweli
Gazeti la kikristo la kila wiki


Askofu Mkuu Nchini Apinga Vikali Uzazi wa Mpango!

Dr Moses Kulola

Wakati serikali ikiendeleza mikakati ya kutoa Elimu juu ya uzazi wa mpango, Askofu mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania(EAGT) Dr Moses Kulola  amepingana na sera hiyo na kusema ni kuingiliana na maamuzi ya Mungu.Amesema hakuna sababu yeyote ya serikali kuweka mikakati ya elimu ya kufunga kizazi kwani hiyo ni kazi ya Mungu mwenyewe.Alisema kuwa kuna kila sababu ya kuikemea  mipango hiyo kwani suala la kudai pawepo na uzazi wa mpango ni kuwa na hofu inayosababishwa na shetani jambo ambalo ni hatari kwa Taifa.

Hayo aliyaeleza alipokuwa akiongea na wasomi wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) katika ibada ya shukrani iliyofanyika katika kanisa la EAGT siloam Ipagala Mkoani Dodoma.Askofu kuloa ana jumla ya watoto kumi na hakuwahi shindwa kuwasomesha.


Kuweni Makini na Manabii- Mch Amnoni Mwakitalu
Wakristo mkoani Mbeya wametakiwa kuwa makini na baadhi ya Manabii wanaotoa unabii pasipo kufuata misingi ya Neno la Mungu ili kuepusha kuharibu imani za waumini wao.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni, mchungaji huyo wa kanisa la Tanzania Assemblies of GOD lililopo Ilomba jijini Mbeya alisema, ongezeko kubwa la Manabii pamoja na wahubiri ambao baadhi yao hawafuati misingi ya Neno la Mungu huaribu imani za watu kwa kuwaingizia imani potofu.

Alieleza watumishi wa MUNGU watatambuliwa na jamii kwa namna wanavyoishi na namna wanavyofundisha na aliwataka waishi maisha ya utakatifu.Pia aliwataka wachungaji na Manabii kufanya miujiza inayotokana na nguvu za Mungu ili kuweza kuondokana na utata uliopo miongoni mwa watu kushindwa kuamini miujiza inayotendeka kwa kuwa shetani naye anaweza kutenda miujiza Luka 21:5 Mathayo 24:23 

No comments:

Post a Comment