Pages

20 June 2013


Glorious Worship Team..GWT Kuja Kivingine

Lile Kundi maarufu la Glorious Worship Team almaarufu GWT baada ya kuwa Kambini Muda Mrefu safari hii wanakuja Kivingine, na nyimbo mpya pamoja na sura mpya kwa ajili ya project kubwa iliyo mbele yao.


Kundi hili lililojizolea umaarufu Mkubwa ndani na nje ya Tanzania ambapo ni siku chache zilizopita walikuwa nchini Kenya kwa ajili ya Ziara yao katika Jiji la Mombasa. Kwa sasa Kikosi hicho kiko kwenye mazoezi makali kwa ajili ya Tour Kubwa wanayotarajia kuifanya ndani na nje ya Tanzania na pia kwa ajili ya “GWT Project One, 2013”. 

Project hii ikiwa ni mwendelezo wa GWT Change Project ambapo katika Phase One walikuwa wakibadilisha Jina kutoka GC kwenda GWT na Sasa Wanaingia katika GWT Project One 2013. Katika Project hii kubwa na ya Kimataifa GWT wanakuja na mwonekano mwingine kimuziki na Kiutawala.

Stay tune na Blog pamoja na Chomoza Ya Clouds Tv.
 Daniel Kibambe akienda Sawa na Mazoezi Ya Vocal.
Sura Mpya ndani ya GWT Melisa Kulia...Irene Kushoto ni hatari sana kwenye Vocal
 Majembe Ya Kazi, ImmaBase Kushoto, ImmaSolo pale Kati, Kulia ni OG Mzee wa "Kinanda"
 Hapana Chezea Mazoezi Ya Vocal Mpaka Kichwa kinauma..Pole Davina...Kulia ni Naomi
 Waimbaji wa GWT wakifatilia Maelekezo kwenye mazoezi
 Daniel Kibambe akiwaekeza Davina, Naomi na Mary namna ya Kutembea na "scale" kwenye Kuimba
Sijui Nice anashangaa ama ndo anatuma Vocal.



You might also like:

No comments:

Post a Comment