Pages

08 February 2013

Jesca Honore Kuvunja Ukimya na Albam ya "Nimevunja Ukimya"

Mwanamuziki Mahiri wa Injili aliyejitoa kutoka Kundi la Glorious Celebration ameiambia blog kuwa anatarajia kufanya mambo makubwa 2013 katika tasnia ya Muziki wa Injili hata Tanzania. Mwanamuziki huyu ame-efatha mbele ya Blogger na kueleza mipango yake ya 2013 lakini pia akieleza kuwa Mwezi May Mwaka huu anatarajia kufunga pingu za Maisha na Mtangazaji wa Kituo Cha Tv hapa Tanzania.

Katika kueleza Mipango yake Mwanamuziki Jesca Honore ameeleza kuwa mwezi March, 2013 tarehe 10 anatarajia kufanya Preview Ya Vision yake katika Muziki wa Injili lakini Pia Kuzindua Eneo la Serena Hotel kama sehemu ambayo atakuwa akifanya Muziki Wa Injili Kila Ijumaa sehemu hiyo.

Akizungumza na Blog Hii Jesca Honore amesema anatarajia kuzindua albam yenye jina la "Nimevunja Ukimya" ulio katika mahadhi ya Kwaito na Katika Uzinduzi huo Utakaofanyika Serena Hotel Utaambatana na Preview ya Vision Ya Jesca Honore. Albam hiyo yenye mchanganyiko wa Mahadhi mbalimbali imefanywa katika Viwango Vya Kimataifa.


Mungu akutumie katika huduma yako mpya!!!Hapa Glorious Celebration tunakutakia Mema....md

No comments:

Post a Comment