Pages

07 February 2013

7,2, 2013

Mpiga Drums Nambari One Wa Joyous Celebration Ajitoa



Mwaka Jana Mapema kabisa Wanamuziki Maarufu Mume na Mke walijitoa katika Kundi Maarufu la JC mwaka huu majira yale yale Mpiga drums nambari wa Joyous Celebration mwenye jina la Siyabulela Satsha ametangaza Kujitoa katika kundi hilo na baada ya Mkataba wake Kumalizika.


Joyous Celebration imekwisha kutoa nafasi ya Kazi ya Jembe hilo ambalo taarifa za Awali zinasema anakwenda kufanya kazi pamoja na Wanamuziki wengine waliokuwa katika kundi hilo na Kujiondoa mapema mwaka jana.


Kumekuwa na mapendekezo kadhaa ya dogo aliyeonekana katika JC 15 miaka miwili iliyopita kuziba gap la mpiga drums huyo. Oyanda ambaye amekuwa akifanya mazoezi na JC kwa muda mrefu ambaye pia ni mmoja wa wanaosadikika kuchukua fomu kwa ajili ya nafasi hiyo anapewa nafasi kubwa zaidi ya kuwa mbeba mikoba hiyo. Changamoto kubwa ni umri alionao Mwanamuziki huo ambapo kwa sasa anamiaka 12-13 na bado yuko shuleni.


No comments:

Post a Comment