Pages

08 June 2012

Friday, June 8, 2012

Baada Ya Kujitoa Joyous Celebration Ntokozo Mbambo Kuja na "Filled"

                                                            Ntokozo kwenye JC 15.

Mwanadada maarufu South Africa aliyekuwa katika Kundi la Joyous Celebration pamoja na Mumewe Ngubeko Mbatha amekuwa kwenye mazoezi makali na kundi lake linalojiita kwa sasa NtoKozo's Band wapo kambini kwa ajili ya kujifua na launching ya "Filled" inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katikati ya Jiji la Pretoria.
                    Ntokozo's Band Wakiwa kwenye Mazoezi ya Launching ya "Filled" chini ya Ngobeko.

Ntokozo's Band ambayo kwenye Upande wa Muziki linaundwa na Vijana wengi wa Joyous Celebration na Wale walio chini ya Solly ambao wako chini ya Ngubeko Mbatha wamejikita kambini kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kazi ya "Filled" inakuwa katika kiwango cha Kimataifa.
                        Mume wa Ntokozo, Ngubeko Music Director wa Ntokozo Band akiwa Kazini

Mbali na Matayarisho hayo Mwanamuziki huyo pia Ntokozo amepata "Shavu" la Kutangaza katika Radio moja Ya Kikristo nchini South Africa yenye jina la "Rainbow FM...90.7".


Today is the day I start as a co-host on Rainbow FM 90.7, every tuesday & thursday 4pm-7pm ☺ I'm super excited! Please do tune in if you're around Jozi or you can listen online viahttp://www.rainbowfm.co.za/
Kundi la Ntokozo's Band Wakiimba Wimbo wa "Filled"

No comments:

Post a Comment