Pages

12 May 2012

ZIARA YA UPENDO KILAHIRO NCHINI CANADA YAZIDI KUPENDEZA


Upendo Kilahiro akiwa na pastor Peter Youngren wa TICC.

Mungu azidi kuonekana katika ziara ya mwimbaji nyota wa gospel nchini Upnedo Kilahiro ambaye yupo nchini Canada kwa ziara ya mwezi mmoja,Upendo ambaye si mara yake ya kwanza kuwa nchini humo ameendelea kupokelewa vyema na jumuiya wa watanzania,waafrika pamoja na watu weupe wa nchini humo katika matamasha na huduma mbalimbali ambazo ameendelea kualikwa kwa ajili ya kumuinua Mungu.

Moja ya mialiko ambayo Upendo amebariki wengi ni katika kanisa la Toronto International Celebration ambako watu wengi walishangazwa na kipaji alichopewa na Mungu katika uimbaji na namna anavyoweza kuchezea sauti yake ushahidi ambao unapatikana pia kwenye video ambayo imerekodiwa na mmoja wa waumini waliokuwepo ibadani hapo na kurushwa kwenye ukurasa wa facebook wa mwimbaji huyu,Pia alipata nafasi kufanya huduma na mmoja wa wahubiri mashuhuri duniani Peter Youngren.Pia jana asubuhi amefanyiwa mahojiano kupitia kituo cha runinga cha GRACE TV, mahojiano ambayo yanatarajiwa kurushwa mwishoni mwa mwezi huu nchini humo.

Ratiba ya mwimbaji huyo ambaye wiki iliyopita aliweza kutembelea ubalozi wa Tanzania nchini Canada,jumamosi hii atakuwa katika kanisa la River Jordan Ministries huku jumapili akitazamiwa kuhudumu mahali pengine.Mwimbaji huyo ameendelea kuwashukuru Watanzania wanaoendelea kuwakumbuka waimbaji akiwemo yeye kwenye maombi ili Mungu aendelee kuonekana katika huduma yao.Upendo kwasasa anatoleo jipya liitwalo ''FICHO LANGU'' kanda ambayo imerekodiwa viwango vya kimataifa ikiwa imechanganywa vionjo mbalimbali ikiwemo kizulu,kizungu bila kusahau kiswahili.
Upendo Kilahiro akifanyiwa mahojiano kwenye GRACE TV jana asubuhi.

Tangazo la tamasha atakalo hudumu jumamosi hii.
                          
Hapa akiwa na balozi wa Tanzania Canada Mh, Massinda alipomtembelea ofisini.
PATA WIMBO ''SALAMA ROHONI'' KATIKA ALBUM HILO NALO LITAPITA BY KILAHIRO

Msomaji wetu tunaendelea kukukumbusha kuwapendekeza waimbaji wetu wa gospel katika tuzo za Africa gospel awards zinazotarajiwa kutolewa mwezi julai mwaka huu huko nchini Uingereza siku zimebaki chache za kufanya hivyo,cha kufanya ingia kwenye hii tovuti www.africagospelawards.com ukiingia humo bonyeza sehemu iliyoandikwa Nominees kisha mpendekeze mwimbaji huyo katika kipengele gani unataka agombee mfano;-

1. GROUP/CHOIR OF THE YEAR
2. MALE ARTIST OF THE YEAR
3. FEMALE ARTIST OF THE YEAR
4. BEST ARTIST OF THE YEAR EAST AFRICA
5. EVENT OF THE YEAR

Jina la mwanamuziki mwenyewe
kazi yake aliyofanya kwa mwaka 2011 April -2012April na sababu ya kumchagua kisha tuma kwenda nominations@africagospelawards.com. BARIKIWA SANA.

No comments:

Post a Comment