Pages

12 May 2012

Mch Anny Fernandes Kuzindua Album yake ya KABURI LIMEPATA HASARA


Mch Anny Fernandes akiwa na Mumewe mtume Venon Fernandes

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la World Agape Ministry mama Anny Fernandes jumapili hii 13.05.2012 atakuwa akizindua album yake ya nyimbo za injili katika kanisa la World Agape Ministry lililoko Mbezi jogoo jijini Dar es salaaam. Sambamba na uzinduzi huo siku hiyo itaendeshwa ibada maalumu ya SHUKRANI na pia itakuwa ni siku  maalumu kwa ajili ya  WAMAMA kanisani hapo.Mama Fernandes ni mke wa Mtume  Venon Fernandes ambaye ndiye kiongozi mkuu wa kanisa hilo na mmiliki wa kituo cha television cha Agape Network Television(ATN).

Mama Fernandes ambaye ni maarufu sana kwa kufundisha Neno la Mungu na kuielekeza jamii misingi ya kuboresha ndoa na Malezi ya familia, anakuwa ni mtumishi mkubwa wa pili kwa mwaka huu kuja na album ya nyimbo za injili.Tofauti na mama Fernades hivi karibuni Mh Nabii Geordavie alitangaza kuja na album ya nyimbo za injili ambazo mpaka sasa zinachezwa katika vipindi mbalimbali vya redio za kikristo na zinapatikana pia katika mtandao unaweza kusikiliza kwa kufatiliaa hii Link hapa chini.

No comments:

Post a Comment