Pages

28 May 2012

Lowasa aichangia Upendo Radio Shillingi Milion 10



Rais mstaafu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mbunge wa Moduli Mh Edward Lowasa, jana alikuwa mgeni rasmi katika tamasha maalumu la kuchangia usikivu mzuri wa Radio ya Upendo Fm 107.7 inayomilikiwa na Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT).Tamasha hilo lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubelee liliambatana na harambee ya kuchangia kituo hicho cha redio Mhe Lowasa yeye pamoja na marafiki zake walichangia jumla ya shilingi Millioni kumi.Lengo la kamati iliyoandaa tamasha hilo ilikuwa ni kukusanya jumla ya shillingi Million 220..

Katika Tamasha hilo liliwahusisha nyota wa muziki wa injili kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo Sara k kutoka Kenya,Jenifer Mngendi,Kijitonyama Upendo group na vikundi vingine vingi.

Mh Lowasa akiwa na mwanamuziki kutoka Kenya Sarak K katika tamasha la Upendo Radio siku ya jana

Mchungaji George Fute ambaye ni Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT,Askofu Alex Malasusa akitoa shukrani kwa Mgeni wa Heshima katika hafla hiyo ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh.Lowasa

Jenipher Mngendi akihudumu siku hiyo

Joshua Kiongozi wa kundi la Kijitonyama Upendo Group akimsifu Mungu ukumbini hapo

No comments:

Post a Comment