Pages

28 May 2012

Kanisa Lililolipuliwa Zanzibar laanza Kujengwa Tena

Baada ya Watu Wasio Julikana Kulipua kanisa la Kariakoo Visiwani Zanzibar usiku wa Kuamkia Jumapili ya Jana, Waumini wa Kanisa hilo siku ya Jana Wametumia kwa Ajili ya Kulikarabati Kanisa hilo kwa Kueleza Kuwa "Watapambana Lakini Hawatafanikiwa".

Siku ya Jana Blog iliwasiliana na baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo na baadhi ya waumini na Kusema pamoja na yote yaliyotokea bado Mtetezi Wao yuko hai. Mmoja wa walioteta na Blog amesema "Tunahitaji Maombi yenu zaidi tukitambua kuwa Vita si yetu ila Vita ni ya Bwana".

Nae Mmoja wa Viongozi Wa Kanisa hilo aliiambia Blog "Pamoja na Kulipua na yale yanayoendelea Watu wamesema wako tayari kujitolea kwa ajili ya Kanisa hilo kurudi katika hali ya Kawaida, na Ibada Zitaendelea kama kawaida wakati Ukarabati ukiendelea, Kwa Ujumla hali si Shwari huku Unguja sababu Leo hii Kanisa Lingine Limeripuliwa, hii ni Vita Ya Uislam dhidi ya Ukristo, Mungu bado yuko Upande wetu".

 Ujenzi Wa Kanisa Lililolipuliwa Ukiwa unaendelea chini ya Waumini Wa Kanisa Hilo
 Waumini wakiziba Mwanga wa Jua ili kuruhusu Ibada Ya Shukrani Kuendelea ndani ya Kanisa

 Gari ya Bishop Dickson Kaganga likiwa katika Muonekano wa sasa
 Ndani Ya Gari
 Waumini Wakiwa Nje kuendelea na shughuli za nguvu Kazi

 Eneo la Mlangoni Pa Kanisa
 Pamoja na Hayo Waumini walianza Kazi Ya Ujenzi Siku Ya Jana
Kazi ya Kuziba Madirisha Kwa Muda Ikiwa Inaendelea.

No comments:

Post a Comment