Pages

11 April 2012

Tamasha La Pasaka Latikisa Mji Wa Dodoma

Kama ilivyotabiriwa baada ya Tamasha la Pasaka kutikisa Jiji la Dar-es-Salaam, tamasha la Muziki wa Injili lenye jina la Tamasha la Pasaka limetikisa Mji wa Dodoma ambapo ni mara ya Kwanza Kwa Tamasha la Pasaka Kufanyika. Miaka yote Tamasha la Pasaka Hufanyika Dar-es-Salaama na Mwanza lakini mwaka huu imefanyika Dar-es-Salaam na Dodoma.

Wapenzi wengi wa Muziki wa Injili walijitokeza katika Tamasha hilo. Kama ilivyo Ada Mwanamuzi Rose Muhando amebamba katika Mkoa huo ambao ndipo yalipo Maskani Yake Ya Kudumu tangu enzi za Kitimutimu kundi maarifu lililomkuza Rose Muhando.

 Baadhi Ya Wanamuziki wa The Glorious Band Wakienda Sawa Katika Tamasha la Pasaka Mkoani Dodoma.
 Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi na Mkuu wa Wilaya Ya Dodomo Bi. Betty Mkwasa Wakisebeneka Siku Ya Jana Katika Tamasha La Pasaka.
 "Mwambie Yesuuu Mwambieeee, Mwambie Yesu Mwambieeee" Upendo Nkone akienda Sawa Na Mashabiki wa Muziki wa Injili.
 Sehemu Ya Watu waliojitokeza Jumatatu Ya Pasaka 
 Upendo Kilahiro Mamaa Zindonga akiwa ametokeza Jukwaani Kuimba baada ya Kumaliza Glorious Band.
 Efrahim Sekeleti Kutoka Zambia akihudumu katika Tamasha la Jumatatu ya Pasaka Mkoani Dodoma.
Malkia Wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando akiwa kwenye Uwanja Wa Nyumbani.

No comments:

Post a Comment