Pages

31 March 2012


Saturday, March 31, 2012

The VOICE warekodi Live DvD Album



Usiku wa jana  kuanzia saa tatu usiku katika ukumbi wa Jumba la Makumbusho unaotazamana na chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es salaam. Kundi maarufu la muziki wa injili liimbalo kwa mtindo wa Akapela lijulikanalo kama THE VOICE, lilikuwa likirekodi LIVE DVD Album. Kwa yeyote Yule aliyefika ukumbini hapo atakubaliana na Hosanna Inc kuwa vijana hawa wanavipaji vya tofauti katika kumtukuza Mungu.

Kundi hili linaloundwa na vijana watano ambao kati yao wanne wanatoka katika familia moja,lilianza kuimba nyimbo ya kwanza iliyopokelewa kwa shangwe ukumbini hapo iitwayo KWENYE MAVUNO, kisha wakaimba nyimbo yao maarufu NAJIVUNIA YESU WANGU ambayo waliimba kwa lafudhi ya Kimasai.Kabla The Voice hawajapanda jukwaani Mc wa shughuli hiyo Minister Godwin Gondwe, aliwakaribisha wageni wote waalikwa kisha shughuli akaanza.Hii ni moja kati ya Live DvD album ambayo ikitoka hutakiwi kuikosa.

The Voice wakiwasalimia mamia ya watu waliojitokeza ukumbini hapo
 Jembe!!!, hawa jamaa wako Vizuri,  ndivyo alivyokuwa akikiri Sam Papaa Katikati ya watu hapo  wakati shughuli ikiendelea.

The Voice wakiendelea kumtukuza Mungu ukumbini hapo

Sehemu ya Umati uliohudhuria tukio hilo

Kulia ni Kijana anaitwa Josiah ambaye ni pekee asiye kuwa ndugu wa damu katika kundi hilo,Huyu Mkaka anaimba sauti ya nne ipasavyo.

Live Recording Ikiendelea

Hapa The Voice wakiimba pamoja na mmoja wa wapiga-solo mahiri nchini Bro Sam Yonanyuma mwenye Gitaa


Kiongozi wa kundi la The VOICE Bro Obedi, akimtambulisha mama yao Mzazi(The First Lady of The Voice), kwa umati uliokuwepo ukumbini hapo

Ndoa ya Sphumele Mbambo mmoja wa wanakwaya wa Joyous Celebration


Sphumele Mbambo ni mmoja kati ya wanamuziki mahiri wa Joyous Cerebration,na hapa unaweza kujionena siku maalumu katika Maisha yake alipokuwa akifunga ndoa huku akipata sapoti kubwa kutoka kwa wanakwaya wenzake wa Joyous.

Sphumele Mbambo akiwa Jukwaani

Sphumele Mbamboakiwa na Mumewe

Mmoja wa viongozi na muanzilishi wa Joyous Celebration Jabu Hlongwane kushoto, akiwa na maharusi.  

Maharusi wakiingia kweye gari maalumu


26 March 2012

GLORIOUS CELEBRATION WAJICHIMBIA KAMBINI TENA

Baada ya kufanya kazi ya Bwana maeneo mabalimbali, Glorious Celebration  sasa wameamua kujichimbia kambini kumtafuta Mungu na kujiweka fit katika kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. 

Kiongozi wa GC, Emmanuel Mabisa alisema, sasa wameamua kujificha katika kijiji cha Chanika ambacho kipo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kumtafuta Mungu. 

Bloger na meneja masoko wa kikundi hicho Rulea Sanga, naye alisema, GC wameamua kufanya hivyo ili Mungu aweze kuwatumia na sio kutumia akili zao katika kufanya kazi ya Bwana. Mungu mara nyingi hupenda sana mtu anayejishusha na kufanya kazi yake kama Yeye apendavyo. Ukifanya kazi ya Mungu kwa kujitafutia umaarufu na kutaka kujulikana kwa wanadamu, Mungu hapendezewi kabisa.

Ngoja tuone maisha wanayopitia GC wakiwa katika kambi yao iliyoko Chanika
 Daniel Kibambe akipambana na dafu, ili apooze koo
Vijana wakipata mihogo baada ya mazoezi yao. Kutoka kulia ni Emmanuel Malisa, Jesica Honore, Gospel, david na Emmanuel  Matelu

 Emmanuel Malisa akipambana na bonge la muhogo..yote maisha
 Kutoka kushoto ni Angel Benard Lyamba akisoma Neno,  David mna Paul wakitafakari Neno
 Ombeni Godwin katikati akiwa na wenzake
 Duuh....Gospel akiwa amechoka...
 Daniel Kibambe akiwa anafikiria jinsi gani ya kumfurahisha kwa njia ya 
 Kiongozi wa Muziki wa GC, Emmanuel Mabisa akiwa hoi
 Usafi muhimu, Chaka
 Kazi iansonga, Mungu atafanya tu...



Kama binadamu unaweza kuchoka, Nice Marando akionekana kuchoka 
 Angel Benard Lyamba....

mDada wa Yesu, Jessica Honore akiwasiliana na jamaa zake, huku akiwa ameshikilia kipande cha bagia 
Kama binadamu unaweza kuwa na mawazo fulani, Emmanuel Malisa

Monday, March 26, 2012

Kutoka Obligado Mpaka Mwamba Mwamba- Solly Mahlangu

Mwanamuziki anayetamba kwa sasa nchini Africa Ya Kusini na Kibao Chake Cha Mwamba Mwamba, Solly Mahlangu ameeleza namna anavyotumia muda mwingi kutengeneza kazi zake. 


Mwanamuziki huyo amefunguka kwenye you tube na kueleza kuwa hutamia research zaidi kujua "Standards" za kazi duniani ilipo na kutengeneza "Mix grill" ya Ukweli.


Katika Clip hiyo Solly ameeleza Hatua zake Kutoka Obrigado Mpaka Mwamba Mwamba. Albam ya Obrigado ndiyo iliyomvumisha mwanamuziku huyo nguli nje ya mipaka ya South Africa.




Kitu Obligado.



Monday, March 26, 2012

Gospel Star Search Is Back.......

Mwishoni mwa Miaka ya 90 na Mwanzoni ya 2000, Wanamuziki Wa Injili wengi walianza kuibuka katika tasnia ya Gospel Music na kuwapiga kumbo wanamuziki 'Solo Artist" waliovuma sana kipindi cha Nyumba kama Mwl. Mwalubalile, Mzungu Four, Kyande, Munushi na Mwasumbi. Kati ya Wanamuziki hao walioibuka wengi waliibuliwa na mchakato mzima wa Gospel Star Search.

Nakumbuka Siku ya Fainali pale Diamond Jubilee, Mwanamuziki Jesca Honore alivyokamata watu kwa Wimbo wake wa Tenzi na mwisho kutunukiwa Zawadi ya gari kama mshindi wa Kwanza. Gospel Star Search iliwatambulisha kwenye Tasnia Wanamuziki Chipikizi kama Victor Aron, Amoke Kyando, Charles Mallya, Jonsia Ivatas, Raymond, Jesca Honore, Luiza, Angela Benard na wengine wengi ambao mpaka sasa wamekamata Anga la Muziki wa Injili.
    Baadhi ya Wajumbe wa Organizing Committee wa Gospel Star Search 2012-Kutoka Kushoto ni Papaa Ze Blogger, Anna Nelson, Michael Nkya, Harris Kapiga, Ikupa Ngao na Husdson Kamoga

Baada ya kuwa kimya Muda Mrefu Wale waaandaaji wa Tanzania Gospel Music Awards sasa wamekuja na Project ya "Gospel Star Search". Mwenyekiti wa Maandalizi hayo Mchungaji na Mtangazaji wa Clouds Redio Mr. Harris Kapiga (HK One) amefunguka na kuongea na Blog kuhusu mchakato huo.

Blogger: Kaka pole na Mujukumu ya Ibada na Weekend kwa Ujumla.

HK One: Namshukuru Mungu aisee, Weekend imekuwa Njema, Kwaresma ndo inaisha Isha hivyo.

Blogger : Kaka nimesikia tetesi kuwa Gospel Star Search imerudi tena kwa Next Level baada ya kuwa Kimya sana.

HK One: Kimya Kingi kina mshindo Mkuu, Ni Kweli Gospel Star Search imerudi tena na Safari hii imerudi Kimataifa Zaidi sababu haiko kama ile ya miaka iliyopita.
Hawa ni Kati walioshiriki Gospel Star Search ya kwanza miaka 7 iliyopita, Kutoka Kushoto ni Jesca Honore aliyeibuka mshindi, anayefuata ni Jonsia Ivatas ambaye kwa sasa ni Mama Mchungaji, Thobias ambaye mwaka jana alipata Tuzo za Mwanamuziki Bora wa Kiume katika Gospel Music Awards na Kulia ni Victor Aron.

Blogger: Hapo ni sawa, Lini unadhani Mchakato wa Kuwasaka na Kuibua vipaji vipya katika Gospel Music utaanza rasmi chini ya Brand "Gospel Star Search".

HK One: Mchakato rasmi unatazamia kuanza rasmi mwezi April na utatuchukua kama muda wa miezi mitatu ili kukamilisha zoezi la kupata Mfalme ama Malkia wa Gospel Music.

Blogger: Je Mchakato huu utashirikisha na mikoa mingine ama ni Dar-es-Salaam peke yake?

HK One: Mchakato huu utaanza kwa Kushirikisha Wilaya Zote Tatu za Mkoa wa Dar-es-Salaam ambapo tutaanzia Temeke, tutakuja Ilala na Mwisho kabisa ni Kinondoni.. Mbali na Dar-es-Salaam, tutaenda mikoani ambapo tumeigawa katika Kanda, baadhi ya kanda hizo ni Kanda ya Kati, Kanda ya Juu Kusini, Kanda ya Ziwa na kanda ya Kaskazini.
Kushoto ni Anna Nelson ambaye ni Mtangazaji wa Tv ya Trenet na Kulia ni Michael Nkya ambaye alikuwa mwalimu wa Kambi iliyopita ya Gospel Star Search

Blogger: Ninaamini katika Gospel wengi watajitokeza kushindania nafasi hizo, je Utaratibu wa Kushiriki Umekaaje?

HK One: Mpaka sasa utaratibu ni kwamba Matangazo yatatolewa na watu wataalikwa na washiriki watapewa namba kwa ajili ya kushiriki katika ushindani huo. Na katika Mchakato huu hatuna Kikomo cha Umri yeyote anayetaka kushiriki basi atakaribishwa.

Blogger: Kuna Ushirikishwaji wa Wadau wengine wa Muziki wa Injili?ama ni kikundi cha watu wachache.\

HK One: Ushirikishwaji Umezingatiwa mfano katika Mikoa shiriki mawasiliano bado yanafanyika ya Wadau wa Muziki wa Injili katika Mikoa hiyo. Na hata "Ma-Judge" ni watu wenye Upeo Mkubwa wa Mambo ya Muziki wa Injili lakini pia wenye Kumjua Mungu Vizuri.

Blogger: Ninawatakia Matayarisho mema na tutakuwa bega kwa bega katika "kufunguka" kwenye jamii.

HK One. Asante Kaka Tukutane tena kwa taarifa zaidi.

Blog Itakuwa inakupa Updates Kila Iitwapo leo, Stay Tune With Ze Blogger.

Monday, March 26, 2012

Kilichojiri Dar es salaam Pentecost Church(DPC) siku ya jana Katika Jumapili ya Kusifu na kuabudu kwa mwezi March


Pastor Safari akiwaongoza Rivers of Life

Tofauti na Umoja wa wakristo wa Madhehebu ya Kiprotestant(CCT),ule wa maaskofu wa kikatoriki, na umoja wa maaskofu wa makanisa ya kipentekoste, Kwa muda mrefu hapa nchini,  ni nadra kukuta umoja wa waimbaji,wainjilisti,wachungaji,mitume na manabii kutoka madhehebu mbalimbali wakikaa pamoja na kufanya jambo katika ufalme wa Mungu pasipo kulivunja  au kutofautiana.

Kanisa la Dar es salaam Pentecost Church(DPC) lililoko Kinondoni jijini Dar es salaam kwa muda mrefu limekuwa na utaratibu wa kuwa na ibada ya kusifu na kuabudu katika kila jumapili ya Mwisho wa Mwezi.Chakujivunia  kama kanisa la Tanzania, ni ile Chemistry inayofanyika mahali hapo(DPC) ambapo watu mbalimbali hufika pamoja pasipo kujali madhehebu kwa nia ya Kumwabudu Mungu kila jumapili ya Mwisho wa Mwezi .

Katika jumapili ya jana ya tarehe 25/03/2012, baada ya maombi ya kufungua ibada hiyo ya kusifu na kuabudu kabla ya wenyeji Rivers of Life Praise and Worship Team kuanza kumwadhimisha JEHOVA, Vikundi mbalimbali vilipata nafasi ya kuhudumu wakiwemo na Tanzania Praise and Worship Team wanaoongozwa na Mtumishi Paul Mwangosi ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akiongoza Praise Team katika huduma ya MANA inayoongozwa na Mwl C.Mwakasege.

Tanzania Praise and Worship Team walipanda madhabahuni na kuimba nyimbo mbili ikiwemo “Yahwee Wewe ni Mungu wa Ajabu” na baada ya kumaliza zikasikika sauti za warudieeeee!!!!

Tanzania Praise and Worship Team wakiwa Madhabahuni

Baada Tanzania Praise and Worship Team,walipanda jukwaani Vijana wa kundi la THE VOICE wazee wa Acapela.The Voice walianza kuimba wimbo wao uitwao “Kwenye Mavuno” Wimbo huu wa Kwenye Mavuno, kwenye Mavuno, Tutashangilia .... ni wiimbo ya Tenzi ,ila the way walivyo u-fix ki-akapela ni Lazima kwa yeyote anayewasikiliza kukiri kuwa Nyumbani mwa Bwana kuna skills toshelevu.Baada ya wimbo huo ndipo walipoimba wimbo wao maarufu wa “Najivunia Yesu Wangu amenipa uwezo” wimbo ambao wamekuwa wakiuimba kwa takribani miaka kumi na tano na hii ni kwa mujibu wa kiongozi wa kundi hilo.

Baada ya The Voice, Mch Safari alipanda madhabahuni na kufundisha Neno kwa ufupi ambapo alisema kuna watu huenda kwenye matamasha ya kusifu na kuabudu kwa ajili ya kuondoa kama sio kupunguza stress, na wengine huenda kwa ajili ya Mungu kukutana na shida zao,na wapo ambao huenda kwa ajili ya kukutana na jamaa zao.Mch Safari akasema cha msingi tunapaswa  kukutana na Mungu kama Baba yetu na kuwa na deper relashionship with him na sio kuyaweka mbele matatizo.Baada ya Neno kwa ufupi ndipo Rivers of Life wakapanda jukwaani na kuanza na wimbo wa My Redeemer Lives  aliou-lead Pastor Safari mwenyewe.

sehemu ya umati uliokuwepo DPC siku ya jana

 Baada ya Pastor Safari kumaliza kulead My Redeemer Lives, alielekea moja kwa moja kwenye kupiga Keyboard(Korg) ndipo mtumishi wa Mungu Bro BALE alipolead wimbo wa “Yu Hai Jehova”,wakati Bale akilead wimbo huo huku akipiga Keyboard nyingine(Korg), John Lisu alikuwa akipiga lead gitaa.Shangwe zilizidi mara baada ya Bro Bale kuimba wimbo wa “Katikati ya Wafalme hakuna Mungu kama wewe”.Baada ya Bale, alifuata John Lisu na watumishi wengine ambao kwa pamoja walipeleka Sifa na utukufu kwa Mungu.

Wakati  sifa na kuabudu zikiendelea watu wengi walizama kwenye maombi, muda ulipozidi kusogea Pastor Safari alitanabaisha kuwa wale wa mbali wanaweza kuondoka ila tutaendelea kuwepo usoni pa Mungu.Hadi Hosanna Inc inaondoka kanisani hapo majira ya saa moja na robo usiku, watu wengi walikuwa wakibubujika kwenye maombi.Kwa Mwezi ujao ibada hii itafanyika tarehe 28/04/2012.

25 March 2012

NDANI YA VOICE OF AMERIKA MBASHAZ

Mbashaz Watembelea Ofisi Za Balozi na VOA

Siku ya Ijumaa (Kwa Saa za USA) huku Tanzania Ikiwa Leo Jumamosi, Wanamuziki Wa Injili Walio katika Ziara Nchini Marekani Flora Mbasha na Mumewe Emmanuel Mbasha Wametembea Ofisi Za Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani na Kuonana na Balozi na kufanya mazungumzo Ofisini Kwake.

Pia wanamuziki hao wametembelea katika Ofisi za Voice Of America a.k.a VOA na kufanya mahojiano katika kipindi cha Redio na TV katika Kituo hicho.
  Balozi Mwanaidi Maajar akiwa na Flora Mbasha Ofisini kwake siku ya Leo
                                              Marekani Kuzuri hii ni Suti ya 21 naona Emma anabadili tu
 Toto la Kizungu likishangaa Mwili Jumba na Pamba za Emmanuel Mbasha
 Msije Mkasema hatujafika VOA ushahidi hapo Juu
Flora na Emmanuel Mbasha ndani ya VOAsiku ya Leo

24 March 2012

Saturday, March 24, 2012

What Makes A Lady Attractive Yaingia Sokoni



Leo Tarehe 24 March, 2012 saa 4:53 Asubuhi nimemaliza kukisoma kitabu Chenye jina la “What Makes A Lady Attractive” Kilichoandikwa na Mwandishi rafiki yangu Rose Mushi.

Kitabu hiki ambacho kimetoka mwezi February, 2012 sambamba na kitabu cha “Brothers In Relationships” vinakamilisha idadi si chini ya vitabu vitano vilivyoandikwa kwa Mkono wa Mwanadada huyu Rose Mushi.

Nilifahamiana na Rose Miaka michache iliyopita wakati Mimi nikiwa Chuo Kikuu Yeye akiwa Sekondary Mkoani Morogoro mmoja wa viongozi wa Ukwata katika Mkoa wa Morogoro, wakati huo akiwa Sekondari alishakuwa ameandika Kitabu chake cha Kwanza. Baada ya kuingia Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam na kuwa Miongoni mwa viongozi wa USCF tawi la Mlimani bado Rose amekuwa akiandika Vitabu. Kwa sasa Rose ni Mwajiriwa wa Taasisi moja ya Kidini hapa jijini Dar-es-Salaam na kwa Sasa Kitengo chake kimepewa Project Moja kubwa ambayo mwanadada huyo anaisimamia.

Katika Kitabu Cha “What Makes a Lady Attractive” Mwandishi amejaribu kuongelea mambo mbali yanayoendelea katika ulimwengu wa akina dada wakijaribu kuongeza ulimbwende wao ambapo kwa sasa tumesikia wengine wakichubua, wakisuka nywele za Wamasai, wengine wakishinda Mwenge na Kwenye Masaloon kutengenezwa ili kuongeza “Attractiveness”. Kali kuliko sasa hivi kuna machine za Kichina za kusimamisha matiti watu wanataka kwa udi na uvumba ku-maintain mivuto yao ya Ujana.

Utangulizi

Katika Sura ya Utangulizi Mwandishi ameonesha ni kwa namna gani Wasichana kama sio Wanawake wamekuwa na “Hofu Isiyo Rasmi” ya kutaka kuwa na mvuto wa namna moja ama nyingine kwa kuongeza shape, ulimbwende, rangi, makalio na hata matiti angalau waingie katika kundi la “Wanawake Wenye Mivuto”. Watu wanatumia muda mwingi kutengeneza Mwonekano wan je ili kuleta mivuto. Kichekesho kilichopo hata wale wanaonekana ni Wazuri, wenye Shapes na Mivuto ya nje sio wanaoolewa.

Mwandishi ameandika kujitengeneza tu muonekano wan je sio mwisho, ni sawa sawa kupaka rangi kaburi nje lionekane zuri kumbe ndani ni mifupa mitupu. Mwanamke kuwa mzuri wa muonekano bila kuwa na kanuni za “Wife Material” ni sawa sawa kuwa na Liabilities ndani badala ya Asset.  Ameeleza katika utangulizi kuwa kuna mambo yakifanyika basi “Mvuto is Un KWepable”.
                    Papaa Ze Blogger Interviewing Rose Mushi kwenye moja ya Events za FoF
Sura Ya Kwanza: “The Place Of Character” Inner Beauty”
Mwandishi katika Sura ya Kwanza ameongea Kuhusu “Tabia”. Mwandishi ameeleza Character is the totality of somebody which defines mtu hata kama amevaa na anamuonekano wa namna gani. Mwandishi ameaeleeza Wanawake wengi wangine wamejikita katika muonekano wan je na kusahau yale mambo yanayowafanya wao kuwa wao. Maana kama ni mavazi kuna saa utayavua, kama ni nywele kuna siku utazinyoa, kama ni kucha utazikata, kama ni wingi kuna saa utalivua lakini Tabia Iko pale pale unalala nayo unaamka nayo unaishi nayo kila siku. Tabia zako ndizo zinazokufanya Watu waseme wewe ni nani.

Katika Sura ya Kwanza ameandika Tabia 15 za Mwanamke ambazo akiziishi sio akizijua zitamuongezea mvuto kwenye Jamii ama kwenye ndoa.

Sura Ya Pili. “The Place Of Physical” Outer Beauty
Mwandishi ameanza kuandika sura hiyo kwa kuanza na swali “Does My Physical Life and appearance really matter?akaendelea kuuliza Je Muonekano wa Kawaida hata kabla mtu hajajua tabia yako inaweza kumvuta mtu? Kati ya vitu vinavyowatofautisha wanaume na wanawake ni “Muonekano wa Nje”. Muonekano wa Nje unaweza kuwavuta watu ama kuwafukuza watu ama kutiliwa mashaka pia. Mwandishi katika Sura hii ameandika mambo matano ambayo hayo yakienda sambamba nay ale ya Sura ya Kwanza basi Mvuto wa Mwanamke utabaki kuwa hapo kila iitwapo leo.

Sura ya Tatu. The Place Of Self Image
Katika Sura hii Mwandishi Rose Mushi ameandika ambavyo unapaswa wewe mwenyew kujikubali kabla hujakubaliwa na Watu. Mtu yeyete mwenye mgogoro wa Nafsi mara zote hupelekea mabadiliko ya Tabia na Mabadiliko ya Mwonekano wan je. Mtu aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Mwandishi anaeleza kuwa kila mtu ameumbwa kwa jinsi ya tofauti na upekee. Kwanza ni lazima ujikubali lazima ujue kuwa wewe ni zaidi ya kila mtu lazima akili yako na ufahamu wako uanze kujikubali ili ukubaliwe.

Mwandishi anaandika anaeleza Tabia 8 zinazojitokeaza kati ya nyingi pale mtu anapotokea kuto kujikubali “What Happens When You Don’t Like Yourself”. Kisha anamalizia Sura hiyo kwa Kutoa Tiba nini kifanyike au mambo gani mtu uyafanye ili uweze kutengeneza “Self Image”.  Mambo 7 yametajwa ambayo unaweza kuyafanya ili uweze na wwe ni Bora. Kabla hujaonwa kuwa ni Bora lazima kwanza ujione wewe ni Bora. Maana aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.

Sura ya Nne. The Place Of God.

Kujitengeneza mambo yote Sura ya kwanza mpaka ya Tatu bila “roho” yako kuwa uhusiano na Mungu ni kazi bure. Uhusiano wa Mwanamke na Mungu una matter sana. Huwezi kuwa na Uhusiano na Mungu ukishakuwa na ndoa yako kama kwenye usichana wako unatumia akili zako mwenyewe. Biblia inasema Zaburi 3:11 Msingi Ukiharibika Mwenye Haki atafanya nini. Msingi unaoujenga kwenye ndoa na mahusiano ukiharibika hakuna matokeo mazuri ya baadae pasipo msaada wa Mungu. Rose Mushi ameshusha sindano nne za nguvu katika kutengeneza Mtu wa ndani kwa mdada ili kuwa mwanamke mwenye mvuto. Maana mambo yote lazima yaishe kwenye Ulimwengu wa Roho kabla hayajaja kwenye ulimwengu wa mwili.

Sura ya Tano. Place Of Communication Skillis.
Rose amejaribu kuonesha namna gani mdada kwa kuwasiliana kwa njia ya mazungumzo anaweza kuwa attractive. Katika sura hii ameandika siri iliyopo katika Kicheko Cha Mwanamke. Wanawake wengi sana wamekuwa wakijizuia kucheka kwa sauti wakiamini Kucheka kwa sauti kutawaudhi wanaume. Anaeleza kuwa kuna Siri kubwa sana Mkaka akamchekesha mdada na mdada akacheka kwa sauti ya kusikika anasema “ The Sound Of a Woman Laughing Is Such a great Sound for men to hear”. Pia ameeleza kuwa Facial Expression and Body Language just form 60% of Communication, Je 40% ziko wapi?.

Sura Ya Sita. Habits That Can Chase People  Away From You.
Tabia 8 zinazoweza wakimbiza wanaume kwenye maisha ya wanawake zimeelezwa katika Sura Ya Mwisho ya Kitabu hiki Cha “What Makes a Woman Attractiveness”

Kitabu Hiki ni Msaada Mkubwa sana Kwa Wakina Dada wa Kizazi Cha Leo.

Ukiitaji Kitabu Hiki Waweza Wasiliana na Rose Mushi kwa 0717190413 ama Wasiliana na Mimi kwa namba 0713 494110.

 Wiki Ijayo nakuja na Uchambuzi wa Kitabu Kingine 

Africa Lets Worship (Aflewo) Is Back In DSM ---Mass Choir Waingia Kambini

Kwa Mara ya Kwanza Event Ya Aflewo Kwa nchi ya Tanzania ilifanyika Mwaka Jana katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. Aflewo ni Kifupi cha Maneno Africa Lets Worship ambapo event hiyo ilizaliwa nchini Kenya, Ikafunga safari mkapa Tanzania na Mwaka jana imefanyika Rwanda na event kama hiyo ilifanyika Nigeria.

Usiku wa Aflewo ni Usiku wa Kusifu na Kuabudu na Kuomba ambapo ikifika mwaka 2020 inchi zote Africa ziwe zina Mkesha wa Aflewo.

Baada ya  Mwaka jana kuanza Vizuri katika Ukumbi wa Diamond Mwaka huu Mazoezi kwa ajili ya Team itakayoongoza Kusifu na Kuabudu Usiku huo imeshaingia Kambini. Mazoezi ya Mass Choir Kwa sasa yanafanyika katika Kanisa la DPC kila Ijumaa.

Aflewo Mwaka huu itafanyika tarehe 4 May, 2012 katika Ukumbi wa Kanisa la CCC Upanga.

Usiku wa Leo Mazoezi yameendelea tena katika Ukumbi wa Kanisa la DPC. 

Kama Kawaida Blog iliingia kazini kwa ajili ya kuleta News.
            Mass Choir Wakiwa Kikazi Zaidi, Jane Makoye anaonekana kwnye Microphone akiwa deeep
                                                            Hapa sasa Watu Waki-Desa Nyimbo 
                                                                 Watu Nyomi

                                                                    Wakaka Kikazi Zaidi
                                  Hawa Nahisi Sauti ya Pili ukisikiliza kwa makini ila inabidi usikilize Kiroho
                                                                                 Twende Sawa
                               Music Director wa Aflewo Samuel Mzee wa Next Level akiongoza kazi

                                                             Umakini Jambo la Muhimu sana
                                                            Inatia Moyo Mass Choir
 Music Director akiimba huku akipiga kinanda na Music Arranger John Lisu akishika Kipaza
                                   Ipyana huu Mdomo ni Kuimba au Njaaa???
 John Lisu Akifundisha Wimbo Usiku Wa Leo Kwenye Mazoezi Ya Aflewo.
                                                                     Kuimba Kazi Aiseee
                                   Huku watu hawafundishwi Kuimba ila Nyimbo
  Sasa wewe Nancy Ni uwepo ama Usingizi? Halafu wewe Lily Unafanya Mazoezi au Unarecord nyimba kwa BlackBerry Nyeupe Yako hahahahaha
                Pastor Safari akiongoza Mass Choir Mwaka Jana kwenye Aflewo
                                                        Mass Choir Ya Tanzania
 Mbele mwenye Tshirt ya Orange ni Papaa Ze Blogger aliyekuwa Mc Wa Event
                                                         Mass Choir Ya Kenya ndani ya Aflewo.
                                                   Mwaka Jana Fulu fulu Uwepo
                                Umati wa Watu Mwaka Jana ndani ya Diamond
                                                   Watu walioacha Kupiga Wakaongea na Baba
You might also like: