Pages

24 March 2012

Saturday, March 24, 2012

What Makes A Lady Attractive Yaingia Sokoni



Leo Tarehe 24 March, 2012 saa 4:53 Asubuhi nimemaliza kukisoma kitabu Chenye jina la “What Makes A Lady Attractive” Kilichoandikwa na Mwandishi rafiki yangu Rose Mushi.

Kitabu hiki ambacho kimetoka mwezi February, 2012 sambamba na kitabu cha “Brothers In Relationships” vinakamilisha idadi si chini ya vitabu vitano vilivyoandikwa kwa Mkono wa Mwanadada huyu Rose Mushi.

Nilifahamiana na Rose Miaka michache iliyopita wakati Mimi nikiwa Chuo Kikuu Yeye akiwa Sekondary Mkoani Morogoro mmoja wa viongozi wa Ukwata katika Mkoa wa Morogoro, wakati huo akiwa Sekondari alishakuwa ameandika Kitabu chake cha Kwanza. Baada ya kuingia Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam na kuwa Miongoni mwa viongozi wa USCF tawi la Mlimani bado Rose amekuwa akiandika Vitabu. Kwa sasa Rose ni Mwajiriwa wa Taasisi moja ya Kidini hapa jijini Dar-es-Salaam na kwa Sasa Kitengo chake kimepewa Project Moja kubwa ambayo mwanadada huyo anaisimamia.

Katika Kitabu Cha “What Makes a Lady Attractive” Mwandishi amejaribu kuongelea mambo mbali yanayoendelea katika ulimwengu wa akina dada wakijaribu kuongeza ulimbwende wao ambapo kwa sasa tumesikia wengine wakichubua, wakisuka nywele za Wamasai, wengine wakishinda Mwenge na Kwenye Masaloon kutengenezwa ili kuongeza “Attractiveness”. Kali kuliko sasa hivi kuna machine za Kichina za kusimamisha matiti watu wanataka kwa udi na uvumba ku-maintain mivuto yao ya Ujana.

Utangulizi

Katika Sura ya Utangulizi Mwandishi ameonesha ni kwa namna gani Wasichana kama sio Wanawake wamekuwa na “Hofu Isiyo Rasmi” ya kutaka kuwa na mvuto wa namna moja ama nyingine kwa kuongeza shape, ulimbwende, rangi, makalio na hata matiti angalau waingie katika kundi la “Wanawake Wenye Mivuto”. Watu wanatumia muda mwingi kutengeneza Mwonekano wan je ili kuleta mivuto. Kichekesho kilichopo hata wale wanaonekana ni Wazuri, wenye Shapes na Mivuto ya nje sio wanaoolewa.

Mwandishi ameandika kujitengeneza tu muonekano wan je sio mwisho, ni sawa sawa kupaka rangi kaburi nje lionekane zuri kumbe ndani ni mifupa mitupu. Mwanamke kuwa mzuri wa muonekano bila kuwa na kanuni za “Wife Material” ni sawa sawa kuwa na Liabilities ndani badala ya Asset.  Ameeleza katika utangulizi kuwa kuna mambo yakifanyika basi “Mvuto is Un KWepable”.
                    Papaa Ze Blogger Interviewing Rose Mushi kwenye moja ya Events za FoF
Sura Ya Kwanza: “The Place Of Character” Inner Beauty”
Mwandishi katika Sura ya Kwanza ameongea Kuhusu “Tabia”. Mwandishi ameeleza Character is the totality of somebody which defines mtu hata kama amevaa na anamuonekano wa namna gani. Mwandishi ameaeleeza Wanawake wengi wangine wamejikita katika muonekano wan je na kusahau yale mambo yanayowafanya wao kuwa wao. Maana kama ni mavazi kuna saa utayavua, kama ni nywele kuna siku utazinyoa, kama ni kucha utazikata, kama ni wingi kuna saa utalivua lakini Tabia Iko pale pale unalala nayo unaamka nayo unaishi nayo kila siku. Tabia zako ndizo zinazokufanya Watu waseme wewe ni nani.

Katika Sura ya Kwanza ameandika Tabia 15 za Mwanamke ambazo akiziishi sio akizijua zitamuongezea mvuto kwenye Jamii ama kwenye ndoa.

Sura Ya Pili. “The Place Of Physical” Outer Beauty
Mwandishi ameanza kuandika sura hiyo kwa kuanza na swali “Does My Physical Life and appearance really matter?akaendelea kuuliza Je Muonekano wa Kawaida hata kabla mtu hajajua tabia yako inaweza kumvuta mtu? Kati ya vitu vinavyowatofautisha wanaume na wanawake ni “Muonekano wa Nje”. Muonekano wa Nje unaweza kuwavuta watu ama kuwafukuza watu ama kutiliwa mashaka pia. Mwandishi katika Sura hii ameandika mambo matano ambayo hayo yakienda sambamba nay ale ya Sura ya Kwanza basi Mvuto wa Mwanamke utabaki kuwa hapo kila iitwapo leo.

Sura ya Tatu. The Place Of Self Image
Katika Sura hii Mwandishi Rose Mushi ameandika ambavyo unapaswa wewe mwenyew kujikubali kabla hujakubaliwa na Watu. Mtu yeyete mwenye mgogoro wa Nafsi mara zote hupelekea mabadiliko ya Tabia na Mabadiliko ya Mwonekano wan je. Mtu aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. Mwandishi anaeleza kuwa kila mtu ameumbwa kwa jinsi ya tofauti na upekee. Kwanza ni lazima ujikubali lazima ujue kuwa wewe ni zaidi ya kila mtu lazima akili yako na ufahamu wako uanze kujikubali ili ukubaliwe.

Mwandishi anaandika anaeleza Tabia 8 zinazojitokeaza kati ya nyingi pale mtu anapotokea kuto kujikubali “What Happens When You Don’t Like Yourself”. Kisha anamalizia Sura hiyo kwa Kutoa Tiba nini kifanyike au mambo gani mtu uyafanye ili uweze kutengeneza “Self Image”.  Mambo 7 yametajwa ambayo unaweza kuyafanya ili uweze na wwe ni Bora. Kabla hujaonwa kuwa ni Bora lazima kwanza ujione wewe ni Bora. Maana aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.

Sura ya Nne. The Place Of God.

Kujitengeneza mambo yote Sura ya kwanza mpaka ya Tatu bila “roho” yako kuwa uhusiano na Mungu ni kazi bure. Uhusiano wa Mwanamke na Mungu una matter sana. Huwezi kuwa na Uhusiano na Mungu ukishakuwa na ndoa yako kama kwenye usichana wako unatumia akili zako mwenyewe. Biblia inasema Zaburi 3:11 Msingi Ukiharibika Mwenye Haki atafanya nini. Msingi unaoujenga kwenye ndoa na mahusiano ukiharibika hakuna matokeo mazuri ya baadae pasipo msaada wa Mungu. Rose Mushi ameshusha sindano nne za nguvu katika kutengeneza Mtu wa ndani kwa mdada ili kuwa mwanamke mwenye mvuto. Maana mambo yote lazima yaishe kwenye Ulimwengu wa Roho kabla hayajaja kwenye ulimwengu wa mwili.

Sura ya Tano. Place Of Communication Skillis.
Rose amejaribu kuonesha namna gani mdada kwa kuwasiliana kwa njia ya mazungumzo anaweza kuwa attractive. Katika sura hii ameandika siri iliyopo katika Kicheko Cha Mwanamke. Wanawake wengi sana wamekuwa wakijizuia kucheka kwa sauti wakiamini Kucheka kwa sauti kutawaudhi wanaume. Anaeleza kuwa kuna Siri kubwa sana Mkaka akamchekesha mdada na mdada akacheka kwa sauti ya kusikika anasema “ The Sound Of a Woman Laughing Is Such a great Sound for men to hear”. Pia ameeleza kuwa Facial Expression and Body Language just form 60% of Communication, Je 40% ziko wapi?.

Sura Ya Sita. Habits That Can Chase People  Away From You.
Tabia 8 zinazoweza wakimbiza wanaume kwenye maisha ya wanawake zimeelezwa katika Sura Ya Mwisho ya Kitabu hiki Cha “What Makes a Woman Attractiveness”

Kitabu Hiki ni Msaada Mkubwa sana Kwa Wakina Dada wa Kizazi Cha Leo.

Ukiitaji Kitabu Hiki Waweza Wasiliana na Rose Mushi kwa 0717190413 ama Wasiliana na Mimi kwa namba 0713 494110.

 Wiki Ijayo nakuja na Uchambuzi wa Kitabu Kingine 

No comments:

Post a Comment