Pages

26 March 2012


Monday, March 26, 2012

Kilichojiri Dar es salaam Pentecost Church(DPC) siku ya jana Katika Jumapili ya Kusifu na kuabudu kwa mwezi March


Pastor Safari akiwaongoza Rivers of Life

Tofauti na Umoja wa wakristo wa Madhehebu ya Kiprotestant(CCT),ule wa maaskofu wa kikatoriki, na umoja wa maaskofu wa makanisa ya kipentekoste, Kwa muda mrefu hapa nchini,  ni nadra kukuta umoja wa waimbaji,wainjilisti,wachungaji,mitume na manabii kutoka madhehebu mbalimbali wakikaa pamoja na kufanya jambo katika ufalme wa Mungu pasipo kulivunja  au kutofautiana.

Kanisa la Dar es salaam Pentecost Church(DPC) lililoko Kinondoni jijini Dar es salaam kwa muda mrefu limekuwa na utaratibu wa kuwa na ibada ya kusifu na kuabudu katika kila jumapili ya Mwisho wa Mwezi.Chakujivunia  kama kanisa la Tanzania, ni ile Chemistry inayofanyika mahali hapo(DPC) ambapo watu mbalimbali hufika pamoja pasipo kujali madhehebu kwa nia ya Kumwabudu Mungu kila jumapili ya Mwisho wa Mwezi .

Katika jumapili ya jana ya tarehe 25/03/2012, baada ya maombi ya kufungua ibada hiyo ya kusifu na kuabudu kabla ya wenyeji Rivers of Life Praise and Worship Team kuanza kumwadhimisha JEHOVA, Vikundi mbalimbali vilipata nafasi ya kuhudumu wakiwemo na Tanzania Praise and Worship Team wanaoongozwa na Mtumishi Paul Mwangosi ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akiongoza Praise Team katika huduma ya MANA inayoongozwa na Mwl C.Mwakasege.

Tanzania Praise and Worship Team walipanda madhabahuni na kuimba nyimbo mbili ikiwemo “Yahwee Wewe ni Mungu wa Ajabu” na baada ya kumaliza zikasikika sauti za warudieeeee!!!!

Tanzania Praise and Worship Team wakiwa Madhabahuni

Baada Tanzania Praise and Worship Team,walipanda jukwaani Vijana wa kundi la THE VOICE wazee wa Acapela.The Voice walianza kuimba wimbo wao uitwao “Kwenye Mavuno” Wimbo huu wa Kwenye Mavuno, kwenye Mavuno, Tutashangilia .... ni wiimbo ya Tenzi ,ila the way walivyo u-fix ki-akapela ni Lazima kwa yeyote anayewasikiliza kukiri kuwa Nyumbani mwa Bwana kuna skills toshelevu.Baada ya wimbo huo ndipo walipoimba wimbo wao maarufu wa “Najivunia Yesu Wangu amenipa uwezo” wimbo ambao wamekuwa wakiuimba kwa takribani miaka kumi na tano na hii ni kwa mujibu wa kiongozi wa kundi hilo.

Baada ya The Voice, Mch Safari alipanda madhabahuni na kufundisha Neno kwa ufupi ambapo alisema kuna watu huenda kwenye matamasha ya kusifu na kuabudu kwa ajili ya kuondoa kama sio kupunguza stress, na wengine huenda kwa ajili ya Mungu kukutana na shida zao,na wapo ambao huenda kwa ajili ya kukutana na jamaa zao.Mch Safari akasema cha msingi tunapaswa  kukutana na Mungu kama Baba yetu na kuwa na deper relashionship with him na sio kuyaweka mbele matatizo.Baada ya Neno kwa ufupi ndipo Rivers of Life wakapanda jukwaani na kuanza na wimbo wa My Redeemer Lives  aliou-lead Pastor Safari mwenyewe.

sehemu ya umati uliokuwepo DPC siku ya jana

 Baada ya Pastor Safari kumaliza kulead My Redeemer Lives, alielekea moja kwa moja kwenye kupiga Keyboard(Korg) ndipo mtumishi wa Mungu Bro BALE alipolead wimbo wa “Yu Hai Jehova”,wakati Bale akilead wimbo huo huku akipiga Keyboard nyingine(Korg), John Lisu alikuwa akipiga lead gitaa.Shangwe zilizidi mara baada ya Bro Bale kuimba wimbo wa “Katikati ya Wafalme hakuna Mungu kama wewe”.Baada ya Bale, alifuata John Lisu na watumishi wengine ambao kwa pamoja walipeleka Sifa na utukufu kwa Mungu.

Wakati  sifa na kuabudu zikiendelea watu wengi walizama kwenye maombi, muda ulipozidi kusogea Pastor Safari alitanabaisha kuwa wale wa mbali wanaweza kuondoka ila tutaendelea kuwepo usoni pa Mungu.Hadi Hosanna Inc inaondoka kanisani hapo majira ya saa moja na robo usiku, watu wengi walikuwa wakibubujika kwenye maombi.Kwa Mwezi ujao ibada hii itafanyika tarehe 28/04/2012.

No comments:

Post a Comment