08 April 2013


Tamasha La Pasaka La Konga Nyoyo ndani ya Jiji la Dar-es-Salaam

Pamoja na Mvua Kubwa iliyonyesha leo katika jiji la Dar-es-Salaam Maelfu Ya Wakazi wa Jiji la Dar wamejitokeza katika Tamasha la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Taifa.

Tamasha Pasaka ni Tamasha linalofanyika Kila Mwaka mara moja katika Msimu wa Pasaka ambapo wanamuziki wa nje na ndani ya Tanzania wanakuwa na muda wa pamoja wa Kusifu na Kumwabudu Mungu.

Mwaka 2013 Kauli Mbiu ya Tamasha ni Amani na Utulivu ambapo fedha zitakazopatikana ni maalum kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Katika siku ya leo Mgeni rasmi alikuwa ni Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye mara kadhaa alipata shuruba ya kupigiwa makelele mara kwa mara kutokana na kukatika katika kwa umeme mara kwa mara.

Mwanamuzi Mwalikwa wa Mwaka huu Kutoka Africa ya Kusini ni Sipho Makabane ambaye jioni ya leo amefanya Performance ya nyimbo 10 Mfululizo ndani ya uwanja huo na Kukonga nyoyo za watu waliohudhuria Tamasha la leo. Malkia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando alifanya kile ambacho kilitarajiwa na Wakazi wa Jiji kwa Kuimba wimbo wa Utamu wa Yesu ulioombwa na Mhe. Mgeni rasmi.

Wanamuziki Wengine waliokuwepo siku ya leo ni Christ Ambassadors kutoka Rwanda, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu, Faraja Mtabobwa na Glorious Worship Team.
Waimbaji Wa Christ Ambassadors kutoka Rwanda walishuka Kutoka Jukwaani na kugusa wanakazi wa jiji la dar na wimbo wao "Kwetu Pazuri" 

Mwanamuziki Wa Injili wa Tanzania Upendo Kilahiro akienda sawa Siku Ya Leo

Upendo Nkone akiwa Jukwaaani
Anastazia Mukabwa kutoka Kenya akiwa na Rose Muhando ambao kwa pamoja wameimba wimbo wa "Kiatu Kivue"
 Christ Ambassadors Choir wakiwa tayari kwa ajili ya Kazi. 
Solomoni Mukubwa akiwa anapadna Stejini tayari kwa ajili ya Kuimba siku ya leo

Ephrahim Sekeleti Mwuimbaji Kutoka Zambia akiwa George Mpella na Hudson Kamoga
Glorious Worship Team wakienda Sawa siku Ya Leo
Malkia wa Muziki wa Injili Rose Muhando akiwa Kikazi Zaidi

Ephrahim Sekeleti akienda Sawa Siku Ya leo
Sipho Makabane akiwa kikazi Zaidi siku Ya leo
Sehemu Ya Umati Wa Watu

Rose akiendelea na Kazi huku Waandishi na Walinzi wakiwa wamemzunguka
Sipho akijiandaa kuingia Jukwaani
Pole Pole akisogelea Umati Wa watu
Koti Likawa Zito
Kikazi Zaidi
Hapa wakitengeneza Tangazo la Chomoza
Bon Mwaitege akiwa mbele ya Camera Man Ray wa Clouds Tv.
Sipho akienda Sawa na Wananchi siku ya leo
Watu Nyomiiiii
Wakati Sipho akiimba ni kama ilikuwa Mchaka Mchaka Kulia ni Anastazia, Rose Muhando Upendo Nkone na Solomon wakimpa Support Sipho.
John  Lisu 

Without Caption 

14 March 2013

Kundi la Joyous Celebration Kuzindua JC 17 Wakati wa Pasaka

Wakati wa Majira ya Pasaka kama ilivyo Ada Ya Joyous Celebration Ya South Africa Itazindua albam yake ya 17 Katika Ukumbi wa Big Top Arena Carnival City. Uzinduzi huo Unaosubiriwa kwa hamu na TOTS (Kundi la Mashabiki Wa JC) pamoja na Watu mbalimbali kupitia page ya Facebook imeelezwa kuwa matayarisho yamekamilika.

Baada ya Kufanya Vizuri kwenye albam ya 16 kila mtu amekuwa akitaka kufahamu safari hii JC wametoka Vipi??Uzinduzi huo unasubiriwa kwa hamu sababu katika shooting iliyofanyika hapo awali ilikuwa ni ya aina yake kulinganishwa na JC 16.

 Mthunzi Namba anatariwa Kuwakilisha Vema kwenye Uzinduzi Huo kama wakati wa Shooting anavyoonekana.
 Baadhi Ya Waimbaji Wa JC wakiwa katika Pozi la JC 17
 Dogo aliyechomoza katika JC 15 Ayanda Shanga ameendelea kutamba katika JC 17
Mukhululi Bhehe Mzimbabwe anayefanya Vizuri katika Jc, alichomoza JC 15 bado ameendelea Kukaba.

 Kwa mbaaali JC 17 Stage inavyoonekana
 Mojawapo ya Nyimbo za JC 17
 Mapacha watatu Jabu, Lindelani and Mthunzi wakienda sawa kwenye JC 17 hawa ndio waasisi wa JC
Mamaa Mavocal..Sijasanga ndani ya JC 17

Kitu Cha Easter 
Jabu ambaye ameonekana katika JC 17 amejitoa katika kundi hilo na hawa wanaonekana ni baadhi ya waliojitokeza Kumrithi kazi hiyo.
 Nyomi Zaidi Ya Hili Linasubiriwa
 Jabu ambaye JC 17 ndo ilikuwa ya Mwisho kwake
Nobathembu ndani ya JC 17
 Kenny Ndani Ya JC 17
Kama Kawaida ya JC

kwa Habari na Sam sasali the bloger no.1.

27 February 2013

Glorious Celebration Kuwa Glorious Worship Team

Kukiwa bado kuna Sintofahamu kubwa imetanda kati ya Waimbaji Waliokuwa wa Kundi la Glorious Celebration na Mmiliki wa Glorious Celebration Company, baadhi ya Waimbaji wa Kundi hilo wamejitoa chini ya Mmiliki huyo na Kuunda Kundi la Glorious Worship Team.

Kwa Miezi Kadhaa kupitia vyombo vya habari na mitandao Jamii kumeibuka sinto fahamu kati ya pande mbili Waimbaji na Mmiliki Wa Kundi hilo Askofu Mwakang'ata. Waimbaji Karibia Wote wa Kundi hilo Wamejitoa chini ya Mmiliki huyo kwa madai Utata Ulioibuka baada ya Mmiliki Huyo Kuamua Bendi Hiyo Kujiendesha Kama Kampuni badala ya Mfumo wa Awali, Pia Blog kwa kuongea Waimbaji Waliojitoa wa Kundi hilo imebainika kuna sababu zaidi ya hizo kwa manufaa ya Mwili wa Kristo sababu hizo hazitawekwa hadharani kwa sasa. Upande Wa Mmiliki wa Bendi Hiyo Askofu Mwakang'ata alieleza mbele ya Christian Bloggers siku ya tarehe 23 Feb, 2012 alipowaita Wanahabari alieleza kuwa kundi hilo liliamua Kuasi liliamua kujitoa baada ya Yeye Kama Mmiliki Kuamua Kuboresha Njia za Kuboresha Mapato Yanayoingia Kupitia Kundi hilo. Ameeleza amekuwa akilihudumia Kundi hilo kwa kutoa fedha za Kanisa na fedha binafsi lakini kundi hilo limekuwa haliingizi fedha kama ilivyokuwa ikitakikana na ndipo alipoamua kuuboresha mfumo huo uliokimbiza Wanamuziki hao "Waasi".

Baba Askofu alitoa maelezo kuwa Glorious Celebration bado ni Mali yake na Glorious Celebration inaingia Kambini Jumanne (kesho) Nje kidogo ya Mkoa wa Dar kwa ajili ya Kujisuka upya baada ya baadhi wa imbaji katika Kundi hilo. Wakati Huo huo Waimbaji Waliojitoa Wamedai Kutokana na Mzozo uliotokea baina yao na Mmiliki Kudai Jina la Glorious Celebration ni male yake wameamua kuboresha kutoka GC na kuwa GWT yaani Glorious Worship Team. Uzinduzi wa Jina hilo na Kutimiza Miaka Miwili Ilifanyika Jana Katika Viwanja Vya Atriums Hotel na Kuhudhuriwa na Umati Wa Watu.

Story Nzima Ya Mahojiano ya Mmiliki na Waimbaji Walioamua kujitoa Itarushwa Katika Kipindi Kipya Cha Tv.....Chini Ya Ze Blogger na Uncle Jimmy Kupitia Kituo Chako Bora Kabisa Cha Clouds Tv.
 OG Akikanyaga Codes za Muziki 
 Kibambe Kama Kawa akikanyga MOTIF
 Hawa Wapigaji Solo na Drums ni Noooouuuuma sana
 Glorious Wakienda Sawa Siku Ya Jana
 Kama Kawa Paul akiongoza Jahazi
 Glorious Kama Kawaa
 Hapo Sasa
 Linah Sanga and Uncle Jimmy wakiwa wanacheza

 Hahah Joel Mlabwa Damu Mpya ya Glorious 
 Kikosi Kile Kile Jina Likingine GWT
 Kikosi Kazi
 Kundi bado Imara GWT
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...