25 June 2012


Monday, 25 June 2012

WAIMBAJI NYOTA WA GOSPEL NCHINI WAKUTANA VIWANJA VYA JANGWANI JIJINI DAR ES SALAAM


Askofu mkuu wa E.A.G.T Dkt. Moses Kulola akihubiri hapo jana viwanja vya Jangwani.

Waimbaji nyota wa muziki wa gospel nchini na nchi jirani ya Kenya ni miongoni mwa waimbaji na kwaya mbalimbali zinazohudumu kwenye mkutano mkubwa wa injili uitwao ''JUNE CRUSADE''unaofanyika katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam ulioandaliwa na kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT).

Baadhi ya waimbaji hao wanaoshirikiana  bega kwa bega na muhubiri mkuu wa mkutano huo askofu mkuu wa kanisa hilo Dkt. Moses Kulola ni pamoja na Rose Muhando, Bahati Bukuku, Flora Mbasha, Martha Mwaipaja, J'sisters,Bonny Mwaitege na waimbaji wengine kutoka nchini Kenya wapo Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa pamoja na Faraja Ntaboba kutoka nchini Congo ambaye kwasasa yupo nchini Tanzania,pia kwaya mbalimbali kutoka makanisa ya E.A.G.T jijini huku askofu Kulola akiwa ameambatana na kwaya ya Bugando kutoka jijini Mwanza.

Mkutano huo ulioanza jana unatarajia kuihitimishwa Julai mosi unarushwa mojamoja na Wapo Radio Fm  ambayo unaweza kuisikiliza kupitia ndani ya blog hii. Licha ya mkutano huo pia askofu Kulola jumamosi alizindua rasmi kanisa la Jesus Village lililo chini ya jimbo la Kinondoni la kanisa hilo tukio ambalo lilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo.


Jacqueline Mshama pamoja na mdogo wake Jesca hapo jana waliwakilisha wenzao kwakusimama kama J'sisters kumsifu Mungu viwanjani hapo. 

Baadhi ya umati wa watu uliojitokeza viwanjani hapo.

Mchungaji Florian Katunzi  wa E.A.G.T City Centre, ambaye ndiye muongozaji wa mkutano huo akiangalia mambo yanavyoendelea.

Askofu wa jimbo la Kinondoni E.A.G.T akiwa katika hali ya maombi.


 UFUNGUZI WA KANISA LA JESUS VILLAGE ULIOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI ILIYOPITA.CHANGANYIKENI DAR ES SALAAM.
Askofu Dkt. Moses Kulola akizindua rasmi kanisa hilo huku mchungaji Mgonja akishuhudia na maelezo yakitolewa na mchungaji Katunzi.

Mchungaji PrayGod Mgonja akisoma Risala kwa askofu mkuu Moses Kulola.

Mke wa askofu Kulola akitoa ahadi yake ya laki tano kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa kanisa hilo.

Brigedia jenerali mstaafu Hemed akiombewa baraka na askofu Kulola.



Kutoka kushoto mchungaji Marego, askofu Willy Matingisa na askofu Bruno Mwakibolwa wakifurahia


MAELFU WAJITOKEZA TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU MKOANI KIGOMA


New Life Band wakimsifu Mungu viwanja vya mwanga community mkoani Kigoma hapo jana.

Bendi kongwe katika muziki wa gospel nchini New ya Life Band yenye makao makuu yake jijini Arusha,  hapo jana iliweza kubariki maelfu ya wakazi wa mkoa wa Kigoma waliohudhuria tamasha lao la kusifu na kuabudu lililofanyika katika viwanja vya Mwanga Community mkoani humo.

Band hiyo kama ilivyopania kuweka mabadiliko na kuamsha huduma ya uimbaji na kuwaeleza waimbaji kiwapasacho kutenda, imezishirikkisha kwaya mbalimbali  na wachungaji kutoka makanisa ya mkoani humo hali ambayo ilileta umoja na kuujenga mwili wa Kristo. Baadhi ya kwaya zilizohudhuria tamasha hilo ni pamoja na Kasulu Vijana kwaya FPCT a.k.a Mke mwema, Eden kwaya KKKT Kigoma, kwaya Katoliki ya mtakatifu Joseph pamoja na kwaya nyingine.

Baada ya kumalizika kwa tamasha hilo, bendi hiyo inatarajia kuanza kambi ya vijana itakayofanyika kuanzia kesho tarehe 26 hadi julai mosi, Bigabiro Mission Kigoma ambapo mwimbaji Upendo Nkone, Mariamu Nkwabi wataungana na bendi hiyo katika huduma ya uimbaji huku kambi hiyo ikiongozwa na neno ''Kijana na ulimwengu wa mabadiliko'', wakihitimisha kambi hiyo bendi hiyo itakwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya tamasha kubwa la kusifu na kuaabudu wakishirikiana na kwaya mbalimbali za mkoa huo.


Wana kwaya wa Kasulu vijana (Mke mwema) wakiimba kwenye tamasha hilo.

Baadhi ya wachungaji na watumishi mbalimbali waliofika katika tamasha hilo wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea.

Wanakwaya wa Mt. Joseph katoliki Kigoma wakimsifu Mungu wakati wa tamasha hilo.

wapiga ala wa kwaya ya Mt. Joseph kanisa katoliki wakiwajibika.

Eden Choir kutoka Lutheran Kigoma wakimsifu Mungu.





Monday, June 25, 2012

Papaa Kumuwakilisha Christina Shusho Nchini Uingereza



Zikiwa zimebaki Siku 5 tu yaani tarehe 30 June, 2012 Ili kufikia tamati ya upigaji kura kwa ajili ya Kumuwezesha Mwanamuziki Pekee wa Kike Tanzania Christina Shusho kushinda katika Category mbili alizochaguliwa kuingia. Mwanamuziki huyo amefunguka katika Radio Ya Watu Clouds FM, na Kueleza kuwa Yamkini akatuma Mwakilishi siku ya Kugawiwa tuzo hizo siku ya tarehe 7 Mwezi 7, 2012 nchini Uingereza.


Christina Shusho Mwanamuziki Pekee wa Tanzania aliyechaguliwa kuingia katika Category 2. Zikiwa kama ifuatavyo.


1.  Mwanamuziki Bora Kutoka Africa Mashariki
2. Mwanamuziki Bora Wa Kike Barani Africa.
              Shusho Kushoto, Papaa Ze Blogger Katikati na Kulia ni Mtangazaji Pastor Harris Kapiga


akihojiwa na Mtangangazaji mahiri Pastor Harris Kapiga katika Kipindi cha Gospel Track  hivi karibuni kupitia Radio ya Clouds FM yenye kusikika ulimwengu Mzima Mwanamuziki huyo amefunguka na kusema, kutokana na Majukumu yanayomkabiri kwa sasa huenda akamtuma Mwakilishi ambaye ni Papaa Ze Blogger kwenda Kumuwakilisha katika Tuzo hizo katika nchi ya Uingereza.

Watanzania tunayo sababu ya Kumpigia Kura Mwanamuzi huyu wa Injili ili kuweza Kutwaa tuzo hizo 2.

Ili kuweza Kumpigia Kura Shusho Sasa hivi Bonyeza ...http://www.ballotbin.com/voterReg.php?b=29492

21 June 2012


Thursday, 21 June 2012

KWA TAARIFA YAKO- JE UNAJUA MWIMBAJI NGULI WA HILLSONG AUSTRALIA ALIHAMA KANISA?

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina ukweli utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


Darlene Zschech.  
KWA TAARIFA YAKO kama hujui ni kwamba mwanamama ambaye amekuwa katika huduma kwa muda mrefu na kundi la gospel la Hillsong Australia aitwaye Darlene Zschech alijitoa ndani ya kanisa hilo yeye na mumewe Mark na kuhamia kanisa jipya huko huko nchini Australia liitwalo Church Unlimited ambalo lipo nje kidogo ya mji wa Sydney.

Mwimbaji huyo ambaye ametumika kwa miaka 25 ndani ya kanisa la Hillsong Australia lililochini ya mchungaji Brian Houston na mkewe Bobbie Houston, alijiunga rasmi na kanisa hilo jipya mnamo mwezi January 23 mwaka jana na kuanza kazi rasmi pamoja na mumewe kama mchungaji kiongozi wa kanisa hilo ambalo liko chini ya Australian Christian Churches(ACC) ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Assemblies of God. Akizungumzia kuhamia katika kanisa jipya mwimbaji huyo alisema ''Our aim was to find God’s choice, those who would lead us into the incredible destiny God has for our house,” the church stated. “God is faithful! 

Kwa upande wa mchungaji Brian Houston wa mega church Hillsong Australia alikaririwa akiwatakia utumishi mwema mwimbaji huyo na mumewe Mark ''I feel good about it ... and our church leaders and elders feel good about it because Mark and Darlene have really sown into our church for a long, long time,'' alisema Brian

Darlene akizungumza alipotembelea jijini London kanisa la HTB mwishoni mwaka jana.
Hata hivyo licha ya mwimbaji huyo na mumewe kuhama imeelezwa kwamba bado watakuwa wakishiriki katika matukio ya sifa na kuabudu zikiwemo recording za kundi la Hillsong kutokana na mchango wake alioutoa ndani ya kundi hilo ambalo kwasasa linawaimbaji lukuki akiwemo mtoto wa mchungaji huyo aitwaye Joel Houston anayesimamia tawi la kanisa hilo jijini New york nchini Marekani, waimbaji kama Brooke Fraser, Annie Garrett na wengineo, ambapo kundi la The Sowers la nchini lilipofanya ziara nchini Australia mwanzoni mwa mwaka jana waliweza kufika mpaka kanisa linaloongozwa na mwimbaji huyo. Wimbo ''Shout to the Lord'' uliotungwa na Darlene ndio ulioanza kulitangaza jina la Hillsong kwenye medani ya muziki wa injili duniani. 



Darlene akikumbatiana na mwimbaji wa The Sowers.

Darlene Zschech akizungumza jambo wakati wa tamasha la The Sowers group toka Tanzania.

The Sowers wakiwajibika kumsifu Mungu walipotembelea kanisa linaloongozwa na Darlene.

Baadhi ya umati wa watu waliohudhuria tamasha hilo lililofanywa na The Sowers group kanisani kwa Darlene.
           DARLENE AKIANZISHA MOJA YA NYIMBO NDANI YA HILLSONG AUSTRALIA.

HAPA HILLSONG ILIWASHIRIKISHA WAIMBAJI NYOTA KAMA RON KENOLY KATIKA RECORDING YAO, HAPA WAKIIMBA SHOUT TO THE LORD.


Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tuonane wiki ijayo

Thursday, June 21, 2012

Ndani Ya Loyola High School Weekend Hii

Time ni Saa 3 asubuhi Mpaka Saa 10 Jioni.

20 June 2012

Kanisa lina Mengi ya kujifunza baada ya DNA kutangaza kurudi kufanya secular Music


DNA
Kwa afrika Mashariki na kati jina DNA(Denis Kagia) sio geni masikioni mwa wafuatiliaji wa muziki, DNA ni mwanamuziki kutoka nchini Kenya aliyetambulika na kupata sifa nyingi baada ya kutoa nyimbo yake ya BANJUKA,mwaka juzi DNA alitangaza kuwa ameokoka.Kwa waliokuwa wanamfatilia kwa kina utagundua DNA alisema wazi kuwa baada ya kuokoka anayafurahia maisha ya wokovu kwa kuwa yamemtenganisha na Pombe na sigara vitu ambavyo alishindwa kuachana navyo hadi alipookoka.Baada ya kuokoka DNA alianza kufanya muziki wa injili huku akifanya kazi ya utangazaji katika moja ya vituo vya redio vya kikrsto nchini Kenya.

Wiki iliyopita DNA akiongea na waandishi wa habari alitangaza rasmi kuwa ameamua kurudi na kufanya muziki wa DUNIA yaani aliokuwa akiufanya mwanzo kabla ya kuokoka na atabase kufanya all clubbing heats na tayari ameshafanya nyimbo mmoja iitwayo “Maswali ya Polisi”.Sehemu kubwa ya wakenya waimbaji na wafuatiliaji wa muziki wa injili nchini humo wameonekana kuuponda uamuzi huo na wengine kuubeza au kumbeza DNA mwenyewe.
Kwa Kanisa, suala la DNA linatoa uwanja mpana wa kujikagua na kujikumbusha kuwa wokovu ni NEEMA,leo DNA ameamua alichoamua na kanisa linasonga mbele sio kwa sababu mimi na wewe{Kanisa} ni wasafi sana kuliko yeye bali KWA NEEMA ya Bwana tunasonga mbele.

Kanisa linapozidi kukaa chini na kumhukumu DNA pasipo kumuombea huku ni kupoteza FOCUS ya safari yetu ya wokovu.Kwa kuwa kimsingi DNA sio wa kwanza kufanya hivyo na hatakuwa wa mwisho ila uamuzi wake unatupa wasaa wa kuangalia vitu gani ambavyo vinatusababisha wewe na mimi(kanisa) tuendelee na wokovu na kisha kuzidi kuvishikilia.
Kanisa halina budi kulichukulia suala la DNA kama darasa, na hapa ninamaanisha wapo wanamuziki wengi NGULI nchini na duniani ambao KRISTO atawaokoa,kuteleza kwa DNA kunatoa darasa huru katika kuwaelekeza hao Maceleb watakaookoka namna ya kudumu katika wokovu na nini wakiepuke ili wasirudi nyuma. Leo hii kuna namba kubwa ya maceleb waliookoka na mpaka leo wanaendelea na wokovu wakiwemo K-Basil,Renee Lamira,Chuck Norris (filamu),Cosmas Chidumule,Mzee Makasy,Mc Hummer,Stara Thomas na wengine wengi.

Mwisho ni vizuri Kanisa endapo litatumia muda mrefu katika kuwafundisha waongofu wapya namna ya kuliishia NENO na kudumu katika maombi, hii itasaidia katika kujenga internal strength ya mtu wakati anatoka na kujitangaza.Kwa uzoefu wangu nimegundua watu wengi maarufu ambao baada tu ya kuokoka na kukaa muda mfupi kwenye wokovu (i mean sio chini ya miaka miwili), wanapofanya kanisani kile walichokuwa wakikifanya huko duniani huwa hakina nguvu, na hii ni kwa kuwa vita yake ni kubwa kuliko nguvu ya Mungu aliyoiunda katika kulifanikisha hilo jambo      VICTOR-HOSSANAINC
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...