04 April 2012

Christina Shusho na Rose Muhando Mchuano Mkali ndani Ya Groove Awards


Yule Mshindi wa Tuzo za Groove Awards kwa upande wa Wanaume, Na pia Mshindi katika Easter Africa Gospel Music Awards, na Pia Mshindi katika Africa Gospel Music Awards Daddy Owen amejitoa katika Kinyang'anyiro cha Groove Awards 2012 ili kuweza kupisha Chipukizi kuweza kuchukua Tuzo hizo Mwaka 2012.

Pamoja na Daddy Owen Kujitoa Jina lake limeendelea kupigiwa kura na mashabiki wake wakimtaka Mkali Huyo wa Gospel Africa Mashariki Kurudi Ulingoni kutoa Changamoto.Daddy Owen anayetamba na Kibao Chake Cha "Dakika Tatu" amekuwa gumzo katika mashindano hayo mwaka huu.


Mwaka Jana katika Mashindano hayo kwa wanamuziki Kutoka Tanzania mshindi aliibuka Christina Shusho na kutwa taji hilo, mwaka huu katika Category ya Wanamuziki Kutoka Tanzania yuko Rose Muhando, Bon Mwaitege, Bahati Bukuku, Christina Shusho na Neema Mushi. Mpaka sasa Mchuano Mkali katika Kura upo kwa Rose Muhando pamoja na Christina Shusho katika Kundi la Tanzania.


MALE ARTIST OF THE YEAR
Man Ingwe Mshiriki mmojawapo katika Category Male Artis
  • Daddy Owen
  • Eko Dydda
  • Holy Dave
  • Jimmy Gait
  • Juliani
  • Man Ingwe
                   Sarah Kierie alimaarufu Sakah K akiwakilisha Female Artist

FEMALE ARTIST OF THE YEAR
  • Emmy Kosgei
  • Gloria Muliro
  • Kambua
  • Mercylinah
  • Mercy Wairegi
  • Sarah Kiarie
                                 Kambua Mmoja wa Washitiki Wa Groove Awards 2012
GROUP OF THE YEAR
  • Adawnage
  • B.M.F
  • Kelele Takatifu
  • M.O.G
  • Maximum Melodies
  • Tetete
NEW ARTIST/NEW GROUP OF THE YEAR
  • Dan Gee
  • Everlyne Wanjiru
  • Kelele Takatifu
  • Maximum Impact
  • Willy Paul
  • Zipporah Eric
SONG OF THE YEAR
  • Exponential Potential – Juliani
  • Furifuri – DK & Jimmy Gait
  • Ghetto – Ekodydda
  • Liseme – Sarah K
  • My call – MOG
  • Ololo – Emmy Kosgei
WORSHIP SONG OF THE YEAR
  • Liseme – Sarah K
  • Nakutazamia – Mercy Wairegi
  • Niongoze – Mercylinah
  • Nisizame -Tumaini
  • Umetenda mema – Kambua
  • Waweza – Everlyn Wanjiru
ALBUM OF THE YEAR
  • Ebenezer – Mercylinah
  • Kibali – Gloria Muliro
  • Liseme – Sarah k
  • Ololo – Emmy Kosgei
  • Pulpit kwa Street – Juliani
  • Utamu wa maisha – Daddy Owen
              Mwanamuziki Wa Kiume Pekee kutoka Tanzania anayewakilisha  Tanzania katika Groove Awards.
HIPHOP SONG OF THE YEAR
  • Exponential Potential – Juliani
  • Ghetto – Eko Dydda
  • Mara hiohio – Bantu & Holy Dave
  • Mmh baba – Kriss Ehh baba
  • Ni msoo – Kelele Takatifu &Holy Dave
  • Press on – Izo & Holy Dave
AUDIO PRODUCER OF THE YEAR
  • Billy Frank
  • Gittx
  • Jacky B
  • John Nyika
  • Papa Emile
  • Saint P
VIDEO PRODUCER OF THE YEAR
  • Eagle Films
  • Eyeris
  • J Blessing
  • Prince cam
  • Sakata
  • Washamba Unlimited
Malkia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando anayechuana Vikali na Christina Shusho katika Groove Awards 2012.
VIDEO OF THE YEAR
  • Exponential Potential – Juliani
  • Holy Ghost fire – BMF
  • My Call – MOG
  • Safari – Adawnage
  • Umetenda Mema – Kambua
  • Am Walking – Alemba & Exodus
COLLABO OF THE YEAR
  • Fresh and Clean – Kevo Juice& Jimmy man
  • Furifuri – DK &Jiimmy Gait
  • My call – MOG & Julaini
  • Ni msoo – Kelele Takaifu & Holy Dave
  • Am Walking – Alemba & Exodus
  • Welwelo – Mr Seed& Danco
RAGGA/REGGAE SONG OF THE YEAR
  • Birthday – BMF
  • Fill me – Mr T & Samukat
  • Love came me way – Verbal
  • My Call – MOG Ft. Juliani
  • Number 1 – Kevo Yout
  • Am Walking – Alemba & Exodus
Kati ya Nyimbo za Sara K zilizoingia katika Kinyang'anyiro mwaka huu ni wimbo wa "Liseme"
DANCE GROUP THE YEAR
  • Alabaster
  • Altamin
  • Detour
  • Iced
  • Saints
  • Zionists
GOSPEL RADIO SHOW OF THE YEAR
  • Gospel Sunday – Milele FM
  • Pambazuka – Citizen Radio
  • Route 104 – Hope FM
  • Shangila – Hope FM
  • Trinity Connect – Homeboyz Radio
  • Tukuza – Radio Maisha
GOSPEL TV SHOW OF THE YEAR
  • Angaza – KBC
  • Crossover 101 – NTV
  • Gospel Garage – K24
  • Kubamba – Citizen TV
  • Tukuza – Radio Maisha
  • Rauka – Citizen TV
Christina Shusho anayefanya vizuri katika Muziki Wa Injili katika Anga za Kimataifa anachuana Vikali na Rose Muhando katika Grooves Awards.
RADIO PRESENTER OF THE YEAR
  • Allan T – Homeboyz Radio
  • Amani Aila – Hope FM
  • Anthony Ndiema – Radio Maisha
  • Eudias – Radio Jambo
  • James Okumu – Hope FM
  • Mike Gitonga – Radio 316
DJ OF THE YEAR
  • DJ Krowbar
  • DJ Jonny Celeb
  • DJ Mo
  • DJ Sadic
  • DJ Sanch
  • DJ GeeGee
CENTRAL SONG OF THE YEAR
  • Nissi – Lois Kim
  • Agiginyani – Shiro wa GP
  • Marurumi – Wakabura Joseph
  • Mahindi Momu – Charles King’ori
  • Munduiriri – Carol Wanjiru
  • Muturire – Jane Muthoni
Huu Ni Wimbo wa "Nakutazamia" wa Mercy Wairegi Uliongia katika Kinyang'anyiro Cha Mwaka huu
EASTERN SONG OF THE YEAR
  • Ameru – Rosemary Njagi
  • Elote – John Mbaka
  • Jicho Pevu – Phylis Mutisya
  • Ngiti Sya Kisala – Scholla Mumo
  • Nzui Mbai – Jeremiah Mullu
  • Uu Ni Mwaka Wakwa – Peace Mullu
NYANZA SONG OF THE YEAR
  • Batimayo – Douglas Otiso
  • Jaherana – Dr. Patrick Oyaro
  • Kendo Nisango – Geraldine Odour
  • Kinde kinde – Pastor Marvelous
  • Okumbana – Naomi Otiso
  • Ruoth Opaki – Tetete
RIFT VALLEY SONG OF THE YEAR
  • Bong’o Longit- Gilbert Chesimet
  • Inet kei- Lilian Rotich
  • Kamura Tanet – Edina Kosgei
  • Kararan Chamet – Moses Sirgoi
  • Narue Tengek- Gilbert Segei
  • Ololo- Emmy Kosgei
PWANI SONG OF THE YEAR
  • Ameniita – Ambrose Dume
  • Ayeiya – Kimsa
  • Ebenezer – Mercy D Lai
  • Heshima – Anastacia Mukabwa
  • Upanga – Mtawali
  • Sela Sela – Rozina Mwakideu
WESTERN SONG OF THE YEAR
  • Bolela Yesu – Gloria muliro ft Man Ingwe
  • Buyansi – Wepukhulu
  • Omusango Kwanje – Jeff King Ft. Man Ingwe & Rufftone
  • Luhya Medley – Masinza
  • Yesu Anyala – Judith Wandera
  • Yesu ni Omuyeti – Naomi Nyongesa
ARTIST OF THE YEAR (UGANDA)
  • Coopy Bly
  • Exodus
  • Holy Keane Amooti
  • Kingsley & Philla
  • Marc Elvis
  • S4J
ARTIST OF THE YEAR (TANZANIA)
  • Bahati Bukuku
  • Bonny Mwaitege
  • Christina Shusho
  • Neema Mwaipopo
  • Neema Nushi
  • Rose Muhando
ARTIST OF THE YEAR (RWANDA)
  • Aline Gahongayire
  • Beauty for Ashes
  • Dominic Nic
  • Eddy Mico
  • Lilian Kabaganza
  • Patient Bizimana
Lilian Kabaganza from Burundi Mmoja wa walioingia katika Kinyang'anyiro
ARTIST OF THE YEAR (BURUNDI)
  • Allelua Music
  • David Nduwimana
  • Fabrice Nzeyimana
  • Mutesi Anne Marie
  • Samuel Nvuyekure
  • Senga Dieudonne
ARTIST OF THE YEAR (SOUTH SUDAN)
  • Daniel Lasuba
  • Jazi Rock
  • Mary Boto
  • Lam Lungwar
  • Silver X
  • Star Eagles

Wednesday, April 4, 2012

Joyous Celebration Kuachilia JC 16 Siku Ya Kesho.

Matayarisho kwa ajili ya Launching Ya Joyous Celebration 16 yamekamilika na Siku Ya Kesho ndani ya Ukumbi wa  Pretoria State Theatre Jioni Moto utawashwa kwa ajili ya launching hiyo.

Mashabiki wa Joyous kutoka Nchi mbalimbali nje na ndani ya Africa wamekwisha kuwasili na Watanzania 


wanne ambao blog imenasa taarifa zao wanaenda kushuhudia Live Launching hii ya 16 ya Joyous 


Celebration katika Mji wa Pretoria.

Watanzania hao Walioondoa Siku ya Jana Kuelekea Pretoria wamesema Walidhamilia mwaka huu lazima 


wakaone Uzinduzi huo na wamesema watakapo rejea nchini watakuja na mzigo mzima Mzima wa Joyous 16.

Blog Inawatakia Matayarisho mema. 

Siyabonga.
       Viongozi wa Joyous Celebration wakiwa kwenye eneo la Tukio kwa ajili ya Setting ya Sound 
Baadhi ya Matukio Katika Joyous 16.


                                             Jabu Akiongoza Kama Kawaida.
 Huu Wimbo Umebamba sana hasa pale "Knock Knock"
 Waimbaji wa Joyous Wakiwa Kazini
 Hapa Si Mchezo
Hii ni aina nyingine Ya Kwaito Inapatikana katika JC 16

You might also like:

03 April 2012

YVONNE CHAKA CHAKA AWASHIRIKISHA SOWETO GOSPEL CHOIR KWENYE ALBUM YAKE MPYA



Chaka chaka akiwa na mumewe Dr Mandlalele Mhinga.

Mwimbaji wa siku nyingi nchini Afrika ya kusini mwanamama Yvonne Chaka chaka yuko studio kwahivi sasa akijiandaa kutoa labum mpya ambayo kwa taarifa zilizopatikiana mpaka sasa katika album hiyo amewashirikisha waimbaji wengine kama Soweto gospel choir ambao juzi walikuwa studio(kwa kundi lililosalia afrika kusini wengine wako ziarani nchini Marekani) na mwimbaji huyo akiwa amewashirikisha katika nyimbo mbili,pamoja na mwanamuziki mwingine maarufu aitwaye Bono wa kundi la U2.

Chaka chaka ambaye amejizoelea mashabiki wengi barani Africa na duniani kutokana na muziki wake,itakumbukwa kwamba alipotembelea nchini Tanzania miaka ya karibuni alitangaza kwamba ameokoka na amekuwa ni mtu wa kanisani kumwabudu Mungu pamoja na kila kitu anachofanya anamtegemea Mungu,mpaka sasa haijajulikana ni nyimbo ngapi zitakazokuwemo kwenye album hiyo na ni nyimbo za aina gani, ingawa tayari amewashirikisha waimbaji kama Soweto gospel choir hata hivyo si kigezo album hiyo kuwa ya dini,ukweli utajulikana itakapotoka au yeye mwenyewe atakapotoa taarifa rasmi.

Chaka chaka ambaye mwishoni mwa mwezi January mwaka huu aliweza kuandika historia kwakuwa mwanamke wa kwanza kutoka Africa kupata tuzo ya World Economic Forum (WEF) iitwayo crystal award kutokana na juhudi zake katika kupambana na malaria pamoja na kazi nyingine za kijamii kwa ujumla,mwimbaji huyo ambaye enzi za utoto wake alikuwa mtoto wa kwanza mweusi kuonekana kwenye runinga ya taifa, south african television ambayo kwasasa inafahamika kama SABC,amekuwa na mafanikio mengi katika maisha yake ya muziki ambapo yeye na mumewe Dr Mandlalele Mhinga wanamiliki kampuni ya magari ya kifahari ya Limousine huko nchini kwao na shughuli nyingine

02 April 2012

TBC Ikirusha kutangazwa kwa Joshua Nassari Mbunge Mteule Arumeru Mashariki



Mtoto wa Mchungaji Joshua Nasari aibuka kidedea Arumeru Mashariki


Dr Wilbroad Slaa akiwa na Joshua Nasari wakati wa kampeni jimboni Arumeru Mashariki

Joshua Nasari ni mtoto wa tano kati ya watoto nane wa Mchungaji Samuel Nasari ambaye ni mchungaji wa kanisa dogo la Kiroho lililoko wilayani Arumeru.Hivi karibuni Joshua Nasari alikuwa akiiwakilisha Chama cha Demokrasia  na Maendeleo(CHADEMA) katika uchaguzi wa kuwania kiti cha Ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki uliomalizika siku ya jana na hatimaye Joshua kutangazwa Mshindi wa uchaguzi huo.

Katika Matokeo ya uchaguzi huo Joshua Nasari aliyezaliwa Mwaka 1985 alikuwa akipambana kwa ukaribu kabisa na mgombea wa kiti hicho kupitia chama cha Mapinduzi Ndugu Sioi Sumari.kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi, Joshua Nassari ameibuka mshindi baada ya kupata kura 32,972 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka CCM Bw. Sioi Sumari aliyepata kura 26,757.

Matokeo kwa Vyama vingine sita vilivyoshiriki ni kama ifuatavyo
DP -77 NRA - 35 AFP - 139 UPDB - 18 TLP - 18 SAU - 22

Kwa mujibu wa Bw. Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.

Joshua Nasari akiwa ameshikilia Biblia

 

Dr Daniel Kulola ahudumu katika Campus Night ya chuo kikuu cha Bugando


Siku ya ijumaa iliyopita katika chuo kikuu cha Tiba jijini Mwanza kiitwacho Bugando University College of Heath Science (BUCHS), kulifanyika usiku maaalumu wa kusifu na kuabudu ulioambatana na mafundisho na maombezi.Katika usiku huo wanachuo wa kikristo kutoka vikundi vyote chuoni hapo kutoka UKWATA,TAFES,CASFETA na HUIMA walikuwa pamoja kwa lengo la kumtukuza Mungu.

Mtumishi wa Mungu Dr Daniel Kulola alikuwepo mahali hapo na alifundisha Neno la Mungui pamoja na kufanya maombezi na kuwaleta watu kwa Kristo.Tofauti na Mtumishi Daniel Kulola, Praise and worship Team kutoka TAFES SAUT ilikuwepo na ikahudumu katika usiku huo.

Tafes Praise Team ikihudumu

Praise ikiendelea

Kulia ni mtumishi Dr Daniel kulola akiwa na mwenyekiti wa Tafes mkoa wa Mwanza mtumishi Madaha

Aminaaaaa

Wanafunzi wakiyakabidhi maisha yao kwa Yesu

01 April 2012

Sunday, April 1, 2012

Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) Yazindulia Rasmi

Mchungaji Kiongozi Wa Kanisa la VCC ametangaza rasmi kuwa Jina la Kanisa Hilo kuanzia leo Tarehe 1 April, 2012 litakuwa likitambuliwa kama VCCT yaani Victory Christian Centre Tabernacle. Hayo aliyasema katika Uzinduzi wa Hema ya Kuabudiwa iliyozinduliwa rasmi katika maeneo ya Kawe-Mbezi Beach.


Tent hilo liliagizwa kutoka South Africa na Kufungwa na Wataalam Kutoka South Africa lina uwezo wa Kuingiza watu 1000 kwa mara moja limezinduliwa leo katika Ibada Maalum iliyofanyika katika Hema hiyo ya Kukutania.


Mbali na Rivers Of Joy ambayo ni Praise Team Ya VCCT, ibada hiyo pia ilinogeshwa na waimbaji wengine kama The Reapers, The Voice na Jennifer Mgendi.


Ibada hiyo iliyojaa Shamra Shamra kutokana na Ibada hiyo kujawa na furaha ya kuwa kwenye Hema ya Aina yake ilisababisha watu wengine kutoka machozi baada ya kuona vile Mungu alivyowavusha kutoka hatua moja kwenda nyingine.


Waumini wa VCCT wakishangilia siku ya leo kwneye Ibada hemani
Praise Team Rivers Of Joy ikiwa inajipanga kwa ajili ya Kuongoza Ibada
Mama Mchunagji Joyce Nkone ambaye ni Assistant Pastor wa VCCT akienda sawa kwenye Ibada ya leo.
Dr, Rev Huruma Nkone akienda sambamba kwenye Ibada
Ndani ya Hema siku ya leo
Dr. Rev Huruma Nkone
 Dr. Huruma Nkone akihojiwa na Waandishi wa habari
 Kitu Ndani Ya Hema
 The Reapers Choir Wakiwa hemani siku ya Leo
 Jennifer Mgendi akiwa kwenye Ibada VCCT
The Voice wakiwa sawa ndani ya Hema leo
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...