Pages

21 February 2013

Wanamuziki Wa Injili Tanzania Waimba Wimbo Wa Kuiombea Amani Tanzania



Wanamuzi mbalimbali Wa Injili Tanzania wamejikusanya na kutengeneza Wimbo Mmoja wa Kuimbea Amani Tanzania. Wimbo huo wenye Jina La "Mungu Iponye Tanzania" umewakutanisha Wanamuziki Mbalimbali wa hapa Nchini.

Blog ikifanya mahojiano na mmoja wa Waratibu wa Project hiyo David Robert ameeleza kuwa Wimbo huo umewakutanisha Wanamuziki Mbalimbali Tanzania kwa ajili ya Kumuomba Mungu kwa ajili ya Amani.

"Siku Moja nikiwa na Bahati Bukuku Likatujia Wazo Kwanini Tusifanye Wimbo Wa Kuombea Amani Tanzania, It was very strong in our hearts, then tukaanza utaratibu wa Kuwatafuta Wanamuziki na Kuwasiliana nao walipo, Ilipata Muitikio Mkubwa sana, Rose Muhando, Bahati Bukuku, Florah Mbasha na wengine wengi unaowajua tukakaa pamoja tuka record, na Jana ndio tumemaliza shooting ya wimbo Huo, kwa sasa tunasubiri tu Kukamilika Kisha tutauweka Wakfu wimbo huo"..Haya yalikuwa ni baadhi ya Maneno Ya David Robert.
Papaa Ze Blogger na Zavid Robert

No comments:

Post a Comment