Pages

27 February 2013

Glorious Celebration Kuwa Glorious Worship Team

Kukiwa bado kuna Sintofahamu kubwa imetanda kati ya Waimbaji Waliokuwa wa Kundi la Glorious Celebration na Mmiliki wa Glorious Celebration Company, baadhi ya Waimbaji wa Kundi hilo wamejitoa chini ya Mmiliki huyo na Kuunda Kundi la Glorious Worship Team.

Kwa Miezi Kadhaa kupitia vyombo vya habari na mitandao Jamii kumeibuka sinto fahamu kati ya pande mbili Waimbaji na Mmiliki Wa Kundi hilo Askofu Mwakang'ata. Waimbaji Karibia Wote wa Kundi hilo Wamejitoa chini ya Mmiliki huyo kwa madai Utata Ulioibuka baada ya Mmiliki Huyo Kuamua Bendi Hiyo Kujiendesha Kama Kampuni badala ya Mfumo wa Awali, Pia Blog kwa kuongea Waimbaji Waliojitoa wa Kundi hilo imebainika kuna sababu zaidi ya hizo kwa manufaa ya Mwili wa Kristo sababu hizo hazitawekwa hadharani kwa sasa. Upande Wa Mmiliki wa Bendi Hiyo Askofu Mwakang'ata alieleza mbele ya Christian Bloggers siku ya tarehe 23 Feb, 2012 alipowaita Wanahabari alieleza kuwa kundi hilo liliamua Kuasi liliamua kujitoa baada ya Yeye Kama Mmiliki Kuamua Kuboresha Njia za Kuboresha Mapato Yanayoingia Kupitia Kundi hilo. Ameeleza amekuwa akilihudumia Kundi hilo kwa kutoa fedha za Kanisa na fedha binafsi lakini kundi hilo limekuwa haliingizi fedha kama ilivyokuwa ikitakikana na ndipo alipoamua kuuboresha mfumo huo uliokimbiza Wanamuziki hao "Waasi".

Baba Askofu alitoa maelezo kuwa Glorious Celebration bado ni Mali yake na Glorious Celebration inaingia Kambini Jumanne (kesho) Nje kidogo ya Mkoa wa Dar kwa ajili ya Kujisuka upya baada ya baadhi wa imbaji katika Kundi hilo. Wakati Huo huo Waimbaji Waliojitoa Wamedai Kutokana na Mzozo uliotokea baina yao na Mmiliki Kudai Jina la Glorious Celebration ni male yake wameamua kuboresha kutoka GC na kuwa GWT yaani Glorious Worship Team. Uzinduzi wa Jina hilo na Kutimiza Miaka Miwili Ilifanyika Jana Katika Viwanja Vya Atriums Hotel na Kuhudhuriwa na Umati Wa Watu.

Story Nzima Ya Mahojiano ya Mmiliki na Waimbaji Walioamua kujitoa Itarushwa Katika Kipindi Kipya Cha Tv.....Chini Ya Ze Blogger na Uncle Jimmy Kupitia Kituo Chako Bora Kabisa Cha Clouds Tv.
 OG Akikanyaga Codes za Muziki 
 Kibambe Kama Kawa akikanyga MOTIF
 Hawa Wapigaji Solo na Drums ni Noooouuuuma sana
 Glorious Wakienda Sawa Siku Ya Jana
 Kama Kawa Paul akiongoza Jahazi
 Glorious Kama Kawaa
 Hapo Sasa
 Linah Sanga and Uncle Jimmy wakiwa wanacheza

 Hahah Joel Mlabwa Damu Mpya ya Glorious 
 Kikosi Kile Kile Jina Likingine GWT
 Kikosi Kazi
 Kundi bado Imara GWT

No comments:

Post a Comment