Pages

05 June 2012

Wanamuziki Wa Injili Ni Wanafiki--Stara Thomas afunguka

Akiwa ametimiza mwaka mmoja na Mwenzi Mmoja Mwanamuziki Wa Injili ambaye hapo awali alikuwa anafanya Secular amefunguka jana na leo katika Radio Clouds pamoja na Praise Power akieleza bila kificho kuwa Wanamuziki wa Injili ni Wanafiki na Wanamakundi.

Mwanamuziki huyo ambaye wiki iliyopita alikuwa ni miongoni Mwa Wanamuziki waliokuwepo katika Friends On Friday ameeleza kupitia vyombo hivyo vya habari hivyo kuwa mara baada ya kuokoka alitegemea support kubwa sana kutoka kwa Wanamuziki Wakongwe na Wale Under ground lakini ajabu amekuta katikati ya Wanamuziki hao Wa Injili Wana Makundi na Unafiki wa hali ya juu.
                                           Papaa Ze Blogger akiteta Jambo na Stara Thomas

Hii si mara ya kwanza kwa mtu mbali na Mwanamuziki huyu wa injili kuongea jambo hilo, Meneja wa Kituo Cha Praise Power George Mpella aliwahi washukia wanamuziki hao wa Injili na Blog ilitupia kama kawaida gonga hapa http://samsasali.blogspot.com/2012/03/iliyobamba-facebookpapa-g-meneja-wa.html

Mtangazaji Mwingine wa Praise Power Uncle Jimmy Temu nae aliwaji funguka kuhusu tabia za Wanamuziki hawa wa Injili.

Je ni kweli Wanamuziki Wa Injili ni Wanafiki??
                                  Mc Luvanda Kushoto, Stara Thomas na Ze Blogger.

Kuna Maswali Blogger anajiuliza, hivi ni kweli Christina Shusho, Pendo Kilahiro na Upendo Nkone (Mapacha Watatu) zinawiva na Rose Muhando??? Ni kweli Beatrice Muhone na Upendo Kilahiro hakijaisha??mbona sijawaona Waki Perform pamoja??Ni kweli Wambura Le Graaaant na Glorious wana beef???Ni Kweli Living Water Worship Team na Next Level CCC Upanga Kuna Tatizo??

No comments:

Post a Comment