Pages

03 June 2012

 LIVE Ndani ya “Heaven On Earth” Usiku huu Mzumbe University



Heaven on Earth ni Tamasha la Muziki wa Injili liandaliwalo wanafunzi wa fellowship ya Mzumbe(USCF) kwa lengo la Kumtukuza Mungu, yaani kama wafanyavyo Mbinguni ambapo wazee ishirini na nne hukaa na kumwabudu Mungu ndivyo Tamasha hilo lilivyolenga.Katika usiku wa leo Hapa Mzumbe University kuna vikundi vingi kutoka vyuo mbalimbali vikiwemo

Praise and worship Team kutoka Muhimbili University
Kwaya na Praise Team kutoka Sokoine University (SUA)
New Life Band na vyombo vyao
Miriam Lukindo wa Mauki
Anna Kirava

Katika hali ya kutia hamasa Praise Team ya Sokoine University(SUA) kwa kuuvuta uungu kwa shangwe na vigelegele wao wametinga na MAVUVUZELA Kabisa ambayo kimsingi ni substute flani ya matarumeta.Mc wa event hii ni Blogger Samsasali Its real Heaven on Earth, kama wafanyavyo mbinguni ndivyo hapa Mzumbe University kinachofanyika kwa Utukufu wa Mungu.

USCF Praise Team wakifanya kama mbinguni wafanyavyo

USCF Praise Team wakiimba wimbo wa “Katikati ya Miungu”

Kwaya ya USCF ikiwa Madhabahuni
Muimbaji na mwanafunzi wa Chuo cha Mzumbe Atosha Kirava wa kwanza kushoto akiimba usiku huu, Atosha kwa sasa anasimamiwa na Kampuni ya Msama Promotion

Crew ya New Life Band ikihudumu
Mc wa usiku wa leo Bra Samuel Sasali akiongoza Jahazi

Sehemu ya Umati
Ni saa tisa kasoro dakika saba Praise and Worship team Kutoka Muhimbili University ikihudumu Mzumbe Univ usiku huu

No comments:

Post a Comment