Pages

07 June 2012

Manny Pacquiao kuongoza Bible study kabla na baada ya pambano lake la jumamosi.


Manny Pacquiao
Bondia maarufu duniani na mbunge wa bunge la Ufilipino Mh Manny Pacquiao(33) amesema kwamba kabla ya kuingia kwenye pambano lake la jumamosi ijayo ambalo atakuwa akitetea mkanda wake, yeye pamoja na wenzake watakuwa na Bible study na baada ya pambano hilo pia watafanya Bible study. Manny Pacquiao aliyasema hayo kupitia Ring Tv mara baada ya kuwasili MGM Gland huko Las Vegas.

Mbunge na mtumishi huyo amesema pamoja na bible study wanatarajia kuwa na gospel concert baada ya pambano hilo.Kwa mujibu wa Pacquiao mwenyewe amekiri kuwa pambano lake la jumamosi ni gumu lakini anayo amani moyoni kwakuwa anaye Mungu.

Manny Pacquiao kulia katika moja ya mapambano yake na akitoka anaenda kumsifu Mungu, Mungu wetu ni mpana kuliko tunavyo fikiri

No comments:

Post a Comment