Pages

25 June 2012

MAELFU WAJITOKEZA TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU MKOANI KIGOMA


New Life Band wakimsifu Mungu viwanja vya mwanga community mkoani Kigoma hapo jana.

Bendi kongwe katika muziki wa gospel nchini New ya Life Band yenye makao makuu yake jijini Arusha,  hapo jana iliweza kubariki maelfu ya wakazi wa mkoa wa Kigoma waliohudhuria tamasha lao la kusifu na kuabudu lililofanyika katika viwanja vya Mwanga Community mkoani humo.

Band hiyo kama ilivyopania kuweka mabadiliko na kuamsha huduma ya uimbaji na kuwaeleza waimbaji kiwapasacho kutenda, imezishirikkisha kwaya mbalimbali  na wachungaji kutoka makanisa ya mkoani humo hali ambayo ilileta umoja na kuujenga mwili wa Kristo. Baadhi ya kwaya zilizohudhuria tamasha hilo ni pamoja na Kasulu Vijana kwaya FPCT a.k.a Mke mwema, Eden kwaya KKKT Kigoma, kwaya Katoliki ya mtakatifu Joseph pamoja na kwaya nyingine.

Baada ya kumalizika kwa tamasha hilo, bendi hiyo inatarajia kuanza kambi ya vijana itakayofanyika kuanzia kesho tarehe 26 hadi julai mosi, Bigabiro Mission Kigoma ambapo mwimbaji Upendo Nkone, Mariamu Nkwabi wataungana na bendi hiyo katika huduma ya uimbaji huku kambi hiyo ikiongozwa na neno ''Kijana na ulimwengu wa mabadiliko'', wakihitimisha kambi hiyo bendi hiyo itakwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya tamasha kubwa la kusifu na kuaabudu wakishirikiana na kwaya mbalimbali za mkoa huo.


Wana kwaya wa Kasulu vijana (Mke mwema) wakiimba kwenye tamasha hilo.

Baadhi ya wachungaji na watumishi mbalimbali waliofika katika tamasha hilo wakifuatilia yaliyokuwa yakiendelea.

Wanakwaya wa Mt. Joseph katoliki Kigoma wakimsifu Mungu wakati wa tamasha hilo.

wapiga ala wa kwaya ya Mt. Joseph kanisa katoliki wakiwajibika.

Eden Choir kutoka Lutheran Kigoma wakimsifu Mungu.





No comments:

Post a Comment